DHAHABU na Mafuta ya Mawese yanatafutwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DHAHABU na Mafuta ya Mawese yanatafutwa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Steven Sambali, Jul 6, 2012.

 1. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #1
  Jul 6, 2012
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Wana JF,

  Kuna kampuni hapa Poland wameomba niwaulizie upatikanaji wa bidhaa hizi, yaani Dhahabu na Mafuta ya mawese.

  Sijui kama mpango utafanikiwa ila kama kutatokea maelewano basi kuna biashara kubwa inaweza kufanyika kati yao na Muuzaji huko Tanzania.

  Jamaa wanataka mtu au kampuni itakayoweza ku-suply 100kg ya dhahabu kwa mwezi na tani 12 za mafuta ya mawese kwa mwezi.

  Kama unamfahamu mtu au wewe mwenyewe ni mfanya biashara hiyo basi wasiliana nami kwa maelezo zaidi kwa kuni-PM hapa JF au kwa kutumia email yangu ya SSAMBALI@HOTMAIL.COM.
  Simu yangu ni +48-503535735.


  ANGALIZO: Jamaa watafanya biashara na mtu mwenye kampuni tu na kila kitu lazima kiwe kihalali. Wanafahamu sana jinsi watu wanavyolizwa hapo Tanzania kufanya biashara na watu wenye kampuni za mfukoni. Makubaliano yakifanyika basi pesa zote zitapitia BANK tu.
   
 2. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #2
  Jul 9, 2012
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mpaka sasa hivi ni dada mmoja tu kaniandikia ingawa na yeye kaingia mitini.

  Bado narudia ombi langu hapo juu. Unaweza kuwa si wewe ila unamfahamu mtu anayeweza kuchangamkia hii biashara. Mawese nafahamu Kigoma yapo mengi ila sijawahi kufuatilia uuzwaji na utengenezaji wake.

  Naendelea kusubiri email zenu.
   
 3. GodfreyTajiri

  GodfreyTajiri JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 846
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 60
  kama dhahabu haitoki tanzania haihitajiwi?
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,165
  Trophy Points: 280
  Kila la heri Mkuu..Sikujua kama Wapoland nao wanayahusudu mawese....Miaka michache mawese yanaweza kuwa bidhaa inayotafutwa na wengi duniani.
   
 5. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  I hope so.... BAK. Maana jamaa zangu kule kigoma wanatandikwa na umaskini utadhani sio Watanzania.

   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,165
  Trophy Points: 280

  Mkuu M_Kishuri umaskini unawaadhiri Watanzania wengi sana nchini na si Kigoma tu pekee yake.
   
 7. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  [​IMG] [​IMG][​IMG]

  Nilikutana na comment ya mtu moja mtandaoni na ambaye alikuwa na haya ya kusema kuhusu Palm Oil Industry in Tanzania:

  Graham says: June 29, 2011 at 9:25 pm
  Tanzania imported cooking oil from Indonesia in the past and perhaps that is still happening. I'm very much in favour of the country producing its own cooking oil and fuel. There is much underused land in Tanzania because most farmers are too poor to use machinery which could greatly increase their productivity.
  In the slow transition to modernisation it will be agriculture which will raise incomes for the huge proportion of the population which suffers from poverty. Has any study found what energy cost is involved in biofuel production in the African tropical zone? I think we would be pleased if the production of fuel there created less pollution than more industrialised methods which are common in the temperate zones of the world.
  Food security for poor people will be enhanced if they are involved in palm oil production for cash. The status quo for poor farmers is not a healthy option so I hope that palm oil production will result in great benefits for the majority of Tanzanians. Careful planning will be needed.

  Mkuu Saambali, tafadhali tembelea hii link hapa unaweza kupata ufunuo zaidi: Tanzania | Oil palm in Africa
   
 8. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mi naona katika hili suala mawese yanakuja tu by the way, nachokiona hawa wapoland wanataka dhahabu tu mawese ni ya kuzugia.Kama vipi si uwaunganishe na Barrick
   
 9. W

  Wimana JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 2,453
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 145
  Dhahabu 100 kg kwa mwezi wape email yangu na tuingie ubia wachimbe wenyewe.
  K
  uhusu mawese, hizo tani ni nyingi sana kwa mwezi, uzalishaji wetu si mkubwa hivyo.
   
 10. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #10
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mkuu GodfreyTajiri,

  Ntawauliza hao jamaa kama watasema hawajali inatoka wapi basi ntakujulisha. Kwa sasa siwezi kusema lolote.
   
 11. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #11
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mkuu BAK,

  Si kuwa wanataka kwa ajili ya kula ila wanataka kama BI-DIESEL.

  Kuna hii kampuni Giant ya mafuta hapa Poland na hadi nje ya mikapa inaitwa PKN ORLEN (PKN Orlen - Wikipedia, the free encyclopedia) ambao kipato chao (faida) kwa mwaka wanacheza na kitu kama US $ 1 Bilion.

  Hawa jamaa si wazalishaji tu wa mafuta ila katika kutimiza masharti ya Umoja wa nchi za Ulaya, basi kila mafuta yanayouzwa, lazima yawe na Bio-Diesel kiasi fulani, kama sikosei kwenye 5% au zaidi. Sasa katika kujiandaa na masharti hayo, wanafanya utafiti wa mafuta mengi ya Bio-Disel.

  Waliomba mafuta ya NAZI ila jamaa ambaye ndiyo anaongea nao moja kwa moja ambaye ni kutoka Msumbiji, kavutia kwao Msumbiji. Ila kwa sababu ni jamaa yangu karibu, nimefanya kulazimisha na mie awatafutie soko jamaa zangu kwa mafuta mawese. Ni kiwanda kikubwa sana na huwa wanaagiza mafuta machafu na kuanza kuyasafisha wenyewe kwenye mitambo yao. Hivyo basi technical know how wanayo na hapo huweza kwa urahisi sana kuchanganya na Bio-Diesel ili kupunguza hewa chafu duniani.

  Tutaangalia bei na matatizo mengine yatakayozuka kama itawezekana kufanya biashara au lahh.

  Kwa kuongezea tu: Mafuta ya JETROPHER haya nayo wanatafuta. Nafikiri wanatafuta ya aina tofauti na kuyafanyia utafiti kwenye magari
   
 12. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #12
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mkuu m_kishauri,

  Asante kwa link. Ntawatembelea hao jamaa na nione ni kwa kiasi gani ntaweza kusaidia jamaa na ndugu zangu hapo Tanzania. Kupata kwao itakuwa kupata kwangu.

  Tupo pamoja kwa sana tu.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 13. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #13
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mkuu Bornagain,

  Umepishana na ukweli kidogo kwenye maelezo yako. Kama nilivyoandika kwa BAK, mafuta ya Mawese, Jetropher na labda yatatafuta na mengine ni kwa ajili ya kiwanda cha kusafisha na kuuza mafuta kikubwa cha Poland kiitwacho PKN ORLEN (kilicho mji wa Plock). Hawa wanataka mafuta kwa ajili ya kuongezea kwenye Diesel na Petrol kama Bio-Diesel. Ni masharti ambayo yapo Poland kuwa mafuta yote wanachanganye na mafuta ya Bio-Diesel kwa asilimia kadhaa.

  Dhahabu ni Kichaa fulani tu mwenye hela zake ndiyo anatafuta. Mafuta ni Kampuni ya Serikali inatafuta na Dhahabu ni MTU BINAFSI anatafuta.

  Kuwasiliana na Barick, mhhhh.... Watakuambia uzifuate kwao CANADA. Pia lengo hapa zaidi ni kuwafaidisha Wazawa.
   
 14. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #14
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mkuu Winama,

  Kuchimba hata mie niliwaambia ila wakasema hawana muda huo. Pia inabidi waanze kusomea na watalaamu wengi kuifanya kazi hiyo. Yeye ni mtu ana deal na dhahabu yenyewe na si kuchimba.

  Ni sawa na fundi seremala umwambie aende msituni akakate Magogo. Unaweza kukuta hata miti yenyewe ilivyo haifahamu maana yeye kazoea uona Magogo au mbao tayari.

  Anyway, kama kutatokea mabadiliko yoyote basi ntakujulisha.
   
 15. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #15
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mkuu Godfrey,

  Tuwasiliane basi maana naona kimya.

  Jamaa wamesema kwa kuanzia inaweza kuwa hata 10kg. Kuna uwezekano wa kuwekeana mkataba kwa kusply tuseme kwa mwaka mmoja hadi mwili. Hivyo mwenye nguvu yake achangamkie huu ulaji.
   
 16. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #16
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  kwa moyo huu wananchi tutajikomboa wenyewe kutoka kwenye lindi la umasikini,
  nimeona wakulima wakubwa wengi humu jukwaani wakianza kufikiria kuanzisha project ambazo pia zitawanufaisha wanakijiji na mimi pia nimekwishauiga huo mfano. Kuhusu swala la bio-fuel, hii ni moja ya plan zangu za baadae lkn mimi nitadeal na jatropha & cassava.. kinachokwamisha kuanza project ni soko lenye faida/future c'se gharama za kulima muhogo wa ugali, kuukausha, kuhifadi, kuusafirisha na kuuza kwa maeneo ya kanda ya ziwa ni hasara tupu compared na nguvu/costs zilizotumika kulimia.

  kuhusu swala la kufikisha quantity inayohitajika si tatizo iwapo wanakijiji watashirikishwa na kuuza cassava/jatro sehemu moja.
  swali:
  -hawa bio fuel industries huwa wananunua products zikiwa ktk hali gani kutoka kwa mkulima? tukishafahamu haya tunaweza kujipanga kufikia mahitaji ya viwango vinavyohitajika [tuanze na cassava]

  -bei zinakwenda vipi kwa tani 1 [cassava]?
   
 17. c

  cannulla Member

  #17
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 14, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 15
  mkuu nimekutumia mail na nmejarb kukupigia namba yako iko busy,,,mi nina uhakika wa kusupply mawese hizo tan tatizo kampun sina nambie nifanyeje
   
 18. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #18
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mkuu Narubongo, asante sana kwa majibu na maelezo ya kupeana Moyo Watanzania.

  Kuhusu Muhogo (Cassava) nafikiri kuna habari ilishaanzishwa hapa juu ya kuzalisha Rectified Spirit au Ethanol. Hawa jamaa sidhani kama watahitaji kununua Muhogo na waanze kuutengeneza Ethanol ila wanaweza kuwa wananunua Ethanol moja kwa moja kama sikosei. Wanahitaji Almost ready product na sanasana iwe kuisafisha kidogo tu.

  Hata mafuta ya mawese au Jetropher ni kuwa lazima wataisafisha zaidi na ndiyo waichanganye na mafuta mengine ya DIESEL au Petrol. Hivyo, sidhani kama itawezekana wao kununua Muhogo na waanze kuubadilisha hadi uwe Ethanol.

  Hebu soma hii thread na uwasiliane na huyu jamaa. Ningelikushauri ukiweza basi muunganishe nguvu na jamaa ili walau muanzishe kiwanda kidogo cha kuzalisha Ethanol pamoja maana kama sikosei, Tanzania hakuna.

  SOMA HAPA: https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/39210-project-funding-sources.html

   
 19. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #19
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mkuu, samahani sana kwa hilo.

  Nimerudi nyumbani usiku sana na nikakaa kwenye Lapotop hadi kama saa kumi usiku hivi. Nilipoenda kulala nikaweza simu kwenye Silence. Nimeona Missed call yako hapa +25571*****135 kama sikosei ndiyo namba yako.

  Mkuu kama una kiasi hicho ila huna kampuni, basi itabidi kukuunganisha kwa bwana mdogo wangu hapo Dar ambaye ana kampuni tayari ya kufanya Export na Import. Hana matatizo na kijana mwaminifu. Itabidi kutumia kibali chake kwa kuanzia na mwisho ikibidi basi kampuni yako mwenyewe unaanzisha.

  Ni jambo linalowezekana na lisikupe shida kabisa. Tatizo tu ni hawa jamaa hatuwezi kuwaambia "hakuna kampuni" na wanafanya biashara na mtu asiye na kampuni. Ingelikuwa kampuni ya mtu binafsi ni sawa maana waongea na mwenye mali moja kwa moja ila hii ni kampuni ya Serikali.

  Ngoja niwasiliane na jamaa kujua ni vitu gani inabidi kwanza uvilete maana kwa uhakika watataka kwanza Sample kama sikosei hazizidi lita tano na wataangalia Chemical contents zake na wakishaziafiki utaanza mchezo wa bei sasa. Mambo yote yakikamilika, basi Mzigo wa kwanza unaanza kutumwa.
   
 20. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #20
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mkuu ngoja niwasiliane na wafanyabiashara wa mawese kigoma tuone kama wanaweza kupata hizo tone za wese kwa mwezi,je commision yangu ni % ngapi tukifanikisha hyo dili?
   
Loading...