Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,623
- 8,427
Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji ‘Mo’ kutoka katika Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL) ametajwa kuwa `Kinara wa Uchumi’ barani Afrika, akishika nafasi ya kwanza ya tuzo miongoni mwa kundi la wafanyabiashara vijana 100 waliotambuliwa na Taasisi ya Choiseul ya Paris nchini Ufaransa.
Kwa miaka mitatu mfululizo, taasisi hiyo imekuwa ikitambua na kuanika orodha ya vijana 100 vinara wa biashara Afrika, wanaotarajiwa kung’ara miaka ijayo, na mwaka huu, Dewji ndiye aliyeibuka kinara.
Kwa tuzo za mwaka huu, Choiseul ilishindanisha wafanyabiashara hao wa Afrika kwa vigezo vya uraia katika mojawapo ya nchi 54 za Afrika, waliokuwa na umri wa miaka 40 au chini ya hapo hadi Januari Mosi, 2016, lakini walio na nguvu kibiashara, huku wakichangia kwa kasi maendeleo ya uchumi wa Afrika.
“Nina furaha na ninajiona mwenye bahati kubwa, kutambuliwa kwa kazi yangu ya kuinua uchumi wa kampuni ninayoiongoza, uchumi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla, katika kipindi chote nilichojikita katika biashara, nimepata mafanikio makubwa, na kupitia MeTL, nitaendelea kuwa sehemu ya mapinduzi ya kiuchumi barani Afrika kupitia sekta binafsi.” Amesema Dewji.
Aidha, aliuelezea ushindi huo kuwa ni kielelezo cha jinsi Tanzania na watu wake wanavyopigana kuinua uchumi wao na Afrika kwa ujumla.
Tangu alipoanza kuiongoza MeTL mwaka 1999 ikiwa na utajiri wa dola milioni 30 (Sh bilioni 63), kampuni hiyo imepata mafanikio makubwa ndani na nje ya Tanzania, na kufikia mwaka 2014 ilikadiriwa kuwa na utajiri wa dola za Marekani bilioni 1.3 (Sh trilioni 2.7).
Hakuna shaka kwamba kutokana na umri wa miaka 41 tu alionao bilionea huyo kijana zaidi barani Afrika, kuna uwezekano mkubwa wa kuzidi kupaa katika mafanikio kupitia biashara zake katika nchi 11 Afrika, zikiwemo za benki, viwanda vya sukari, nguo, mashamba makubwa ya biashara, ikiwa ni pamoja na katani, chai, korosho na kadhalika.
Chanzo: Hivi Sasa