USALAMA WA MAJI YA KUNYWA YENYE JINA LA KIBIASHARA DEWMamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imebaini uwepo wa taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na simu za mikononi za kukataza watu wasinunue wala kunywa maji yaliyofungashwa kwenye chupa yenye jina la kibiashara Dew kutokana na madhara ya kiafya yaliyosababishwa na maji hayo katika nchi za Nigeria na Ghana.TFDA imefanya ukaguzi na ufuatiliaji wa maji hayo katika soko la Tanzania kupitia ofisi za kanda za TFDA na haijabaini uwepo wa maji ya aina hiyo. Hivyo basi, Mamlaka inasisitiza kuwa taarifa hizo ni za uvumi na zinalenga kupotosha umma. Aidha ikumbukwe kuwa tukio kama hili liliwahi kujitokeza mwaka 2011 na taarifa kusambazwa kwa mfumo uliotumika sasa. Hata hivyo , baada ya kufanya ufuatiliaji na ukaguzi iliridhika kuwa hakukuwa na ukweli wowote. Aidha Mamlaka inapenda kuutarifu umma kuwa maji aina ya Dew Drops Drinking water yanayotengenezwa na kiwanda cha Dew Drops Ltd, kilichopo mkoani Rukwa yamesajiliwa na TFDA kwa mujibu wa sheria na hivyo wananchi wasiwe na hofu kuhusu usalama wa maji hayo.Vilevile, inatoa wito kwa wananchi iwapo watagundua kuwepo kwa maji aina ya Dew watoe taarifa katika Ofisi ya Afya ya Wilaya au Mkoa, Ofisi za Kanda za TFDA zilizopo Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma na /au Ofisi za Mamlaka ya Chakula na Dawa Makao Makuu zilizopo eneo la External-Mabibo, Dar es salaam kwa ajili ya ufuatiliaji.Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitiaanuani ifuatayo; Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Chakula na Dawa S.L.P 77150 Dar es salaam Simu na.255 22 2450512,2452108,0685701535.0658445222 Fax. Na. 255 22 2450793 Barua pepe: info@tfda.or.tzTovuti:TFDA - Home
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.