Devotha Minja wa ITV Morogoro

Devotha Minja wa ITV Morogoro

hivi jamani naomba niulize kidogo kwani kule Tandahimba alikoshinda mgombea wa CHADEMA kuna wachaga wengi kuliko makabila mengine?maana mara chama cha wachaga mara ukanda,mi nafikiri chuki mnazopandikiza hazina mantiki
Si kweli...

Tandahimba hajashinda Mbunge wa CHADEMA...

Ameshinda AHMED KATANI wa CUF
 
ccm wanaongelea ukanda,ukabila na udini, watu wenye akili ndogo wanawashangilia hawajui madhara yake kwani huku ni kuwagawa watanzania, angali Paris wanavyouwawa, na wanashindwa kujilinda kwa sababu ya mgawanyiko wa kiimani, wenye imani moja wanawaficha na kuwasaidia wahalifu kuwauwa wenye imani nyingine bila kujua huko wanakoenda kufanya huo uhalifu kuna ndugu zao,athari za kuwagawa watu ni mauaji ya Mashaka, ubaguzi wa aina yeyote unapaswa kupingwa kwa nguvu zote. vita vya watanzania ni wizi wa rasilimali unaofanywa na ccm,elimu mbovu, uonevu, usalama mdogo, Hakuna atakayekua salama ikiwa hatuna amani kila chama,dini, kikundi au mtu binafsi afikirie kabla ya kufanya anachotaka kufanya au kusema.
 
mkuu menichekesha kweli kweli, umesahau na ufuo saro kule kanda wa pwani.

Ufoo Saro mwelekeo wake haueleweki vizuri yaonekana ni ccm zaidi. Darubini bado zipo kazini itategemea uchunguzi wa sasa utakavyoonyesha.
 
Ninachokiona ndani ya CHADEMA ni ubaguzi, mimi nimeshuhudia na nafahamu mengi ndani ya CHADEMA, sisemi hivyo kwa Devtha Minja kuteuliwa kuwa mbunge wa viti maalum la hasha! ila mfumo mzima wa uongozi wa CHADEMA inaangalia ukabila, ukanda na mahusiano kimapenzi. Watu au mwanachama wa kawaida ni vigumu kufahamu mambo yanayoendelea ndani ya CHADEMA. Ili kujua nini kipo ndani ya chama ingia mwenyewe ushuhudie.
CHADEMA ya sasa si ile ya zamani.
 
Kwa hiyo Spencer Lameck abadilishwe jinsia sio??. Sisi tunaongelea viti maalum wewe unakuja na jini uchochezi na kuleta uozo hapa.

nimefurahia sana jibu lako, haya ndiyo majibu wanayoyastahili wasioelimika na wapenda majungu.
 
nadhani kuna umuhimu wa kubadilika. kuwa mchaga hakumnyimi haki ya kuwa kiongozi katika nchi hii.tusiwe na wivu kwa sababu baadhi yao wamefanikiwa sana. najua ni propaganda za kuiangusha chadema ila ninachosema tutafute propaganda nyingine, wachaga wana haki ya kula hii keki ya taifa. acheni ubaguzi

wamekuwa wachaga wengi sana kwenye uongozi wa chadema bana! Hii inatia shaka hata kama hatupendi ukabila.
 
Kosa halihalalishwi na kosa lingine jibu hoja.
Kwa majibu haya na mtazamo huu mnamtia matatani mmiliki wa kituo alichokuwa anafanyia kazi huyo aliyeteuliwa.

Devota Minja aligombea viti maalum. Kitendo cha kuchaguliwa na mkoa kinampa sifa ya kupeteuliwa kuwakilisha mkoa. Siamini kuwa kabila lake ndilo lililomfanya ashinde katika uchaguzi wa mkoa. Bila shaka mnajaribu kupiga majungu tu
 
nawapongeza saaaana chadema kumteua uyu dada ubunge viti maalum anastaili kwakweli maana alikua jasiri kureport habari ambazo zingemtia matatani
tutammiss sana wapenzi wa itv

Vibara wa ukawa kwenye mitandao wanaiambia ccm isilipe fadhira lakini wao viti maalumu aslimia 70% ni wale wao kuwa wanawasaidia ndani ya ccm na nje ya ccm,pamoja na wake summaye mademu wa viongozi na waandishi wa mengi,
 
Sasa Devota Minja aligombea viti maalum au anazawadiwa tu?Mimi napata shida nikisikia mtu kapewa viti maalum bila kugombea na waliogombea na wenye uwezo hawajapata.Kama Kagera Pamoja na Kuwa na idadi Kubwa ya wapiga kura na mkoa unaounga mkono upinzani tunapata kiti kimoja tena anapata mtu Yule Yule ambaye hata hatujawahi ona mchango wake bungeni.Kagera kuna kina mama wenye uwezo mkubwa na wasomi Kama kina Jane Pesha Kila Mara utasikia ooh wamekosa Kidogo Sijui namba yake ilikuwa inafatia baada ya majina yaliyochaguliwa .Yaani hata 2010 na 1015 ni the same story.Hawa kina Devota Minja kureport tu habari Za uchaguzi wameshazawadiwa ubunge.Waliogombea tangu 2010 na kushiriki shughuli Za Chama wanawekwa kwenye waiting list Kila uchaguzi.Hata haipendezi.Kagera wakipatikana makamanda wa ukweli wananchi wengi wanapenda siasa Za ushindani na mabadiliko .Hata 2010 upinzani kwa kiti cha uraisi ulipata kura nyingi kazidi CCM.Mwaka huu hujuma zilikuwa nyingi imesababisha kura nyingi Za uraisi kupungua Ila kiukweli Kagera ni wana mageuzi.Sasa watu wakishaanza kuona Siasa Za upendeleo Kama ilivyofanyika kwenye viti maalum watakata tamaa na kuanza kupigia CCM.
 
Massawe alikwenda mkoa wa Kagera kama mkuu wa mkoa! ule mkoa alijitahidi uweze kubadilika na kuanza harakati za kuleta maendeleo, lakini kutokana na malumbano ya kisiasa akashindwa na kuhamishwa kabisa na MaCCM, sasa huyu jamaa na uchagga wake, mbona alipigania maendeleo ya Kagera wakati ni mchagga?, CCM achana na mambo ya kutajana ukabila!, tuangalie maendeleo.
Yaani Upuuzi wa Udini na Ukabila unaoenezwa na CCM, utatugharimu.
Wamepiga vita Wahaya na kuwaita majina ya ajabu ajabu, wameenda kwa Wanyakyusa, hivyohivyo!
ushauri wa bure? CCM CHUKULIENI CHANGAMOTO NA ILI IWE FULSA, SIO MNAKAA NA KULALAMIKA UKABILA, UKABILA!
 
Back
Top Bottom