Developers wa Tanzania Tunashindwa wapi??

ray57

Senior Member
Oct 29, 2013
102
45
Nimelala nikaamka na akili zangu za usiku, nikawaza sanaa, Kwa nini app, system,site nyingi za Tanzania huwa zinazaliwa na kufa kwa muda mfupi? Kwa nini hazitoboi? kwa nini hazipati nafasi ya kujikita juu na kujiendesha?
Hapa kutakuwa na sababu nyingi sanaa zinazopelekea kuwa na haya matatizo yanayojitokeza kwa Developers wetu nchini.
Kwa ufupi nikapata shida kama chache zinazoleta maafa kwa Developer wengi na Product zao.

1. Kuna Developers kweli wanajua ku code na ukimwambia nataka hiki basi utakipata, kama wapo kama hawa au upo wewe basi jua Shida ya kutambua nini Jamii inataka nini na Business inaendaje mtaani, maana mwisho wa siku product yako hutumii mwenyewe inatumika na jamii. Developer wengi wana code ideas zilizopo kichwan mwao na wanashindwa kujua nje jamii inataka nini thats why ukipush system yako/app kwenye market inakufa faster tuuu.


2. Ubunifu hakuna, Elimu ya Science na Technologia ya Nchi yetu inafundisha vijana ku copy na ku paste. Ku drive sample code katika compiler zao tuu. Meisho wa siku ukimleta katika kazi halisi mizigo hua haitembei. Ukipita mtaani utasikia wengi wanajua Java,php,Python, Jquery na madudu ya ajabu ukiwaweka kwenye meza wanajua ku input data na ku output tuu. Elimu haitufanyi kubase on real issues za kijamii. Kama wewe ni Mwanafunzi jifunze sasa kufanya na kusolve real problems zinazokuzunguka kwa code zako.

3. Serikali na Makampuni binafsi zinashindwa kutoa changamoto zilizopo. Michango yao haipo. Ujanja ujanja ni mwingi. Wenzetu Kenya sasahiv kila kitu unafanya online hata kununua Unga dukani unaweza lipia kwa Mpesa, Sheli zote unalipa kwa mpesa, yani unaweza zunguka siku nzima huna shiring mfukoni ila ukala na kusafiri kwa Kulipia vitu vyote online, Goverment support na Makampuni binafsi yako njema kusupport. Ila ukirudi Tanzania limitation kila kona. Wataalamu wa online intergration mtakuja niambia urahisi wa haya mambo kwetu huku ukoje na kwa nini hakuna hizi mambo.


Wewe kama Mdau wa Technologia hii ya sasa Changamoto gani unaziona? Kwa nini Tuna shindwaaa kwenda na Technology nchini.
Tuachane na MAmbo ya kutengeneza Blog za udaku na app za kuwaibia raia pesa zao.
Tuzungumze nini kifanyike ili jamii inufaike na wewe kama developer uweze kuendelea.



Matusi, Kejeli, Zinaruhusiwa Kuwa huru na mchango wako ndio pona ya mwezako kesho.
 
Hata ulaya startup nyingi hazitoboi. Ni kama nature law hivi. Ila walofanikiwa wako vizuri
 
Hata ulaya startup nyingi hazitoboi. Ni kama nature law hivi. Ila walofanikiwa wako vizuri
Sasa kitu kizuri ni kujua ni sababu zipi zinafanya zitoboe na zipi zinafanya zisitoboe.... kujua ugonjwa ni njia moja wapo ya kujua utatafutaje tiba na kupambana nao.
 
Ku-code ni jambo moja na kujua exactly jamii inataka nini ni jambo lingine. Programmers wengi wana-code vitu vya kichwani mwao bila kuzingatia jamii itapokeaje App husika.

Big companies zinaajiri watu wa vipaji tofauti ili kuzuia hasara kama hizi za ku-code/ progamme Apps ambazo jamii haizihitaji! Ndio sababu, kampuni nyingi kubwa zina Directors wa Technology and Innovation ambao hata sio watu wa IT....but wana uwezo mkubwa sana wa kuoanisha uvumbuzi na mahitaji ya jamii...plus huge coordinating capabilities.
 
Changamoto kubwa ni pesa. Kwasababu kuna watu wanafikiria kudevelop project kubwa ambazo zitachukua miezi au hata miaka kabisa lakini ni nani atawawezesha kwa kipindi chote hicho mpka project iishe.Kwahiyo inapelekea kudevelop system za kawaida tu ili wapate pesa za kujikimu kila siku iendayo kwa mungu
 
Mimi naona kila comment ina ukweli sana,Ila nakubaliana sana na Hardwood , kwa sababu sio upande wa coding to, biashara zote, kama hujui how to sell, hakuna kitu unafanya! In person naweza kukuambia, kati ya Mtaji, Idea nzuri, Uwezo wa kucode, gov support na vingine kati ya hivyo, chenye nguvu au ujuzi wa maana kuliko wote hapo ni Interpersonal Skills. Ikimaster interpersonal skills unaweza kupata mtaji, ukawashawishi watu wakusaidie, ukapata wateja wengi na connection ambazo zitakupeleka mbali sana.
Hizo skills na vitu vingine kama pesa ni vya muhimu sana ila ukiwa navyo ukakosa interpersonal skills hufiki popote.
Mimi nimewahi kumsaidia mtu project yake kwa miezi 11, hajanilipa chochote..sasa hivi amepata investors na anaweza kunilipa, ila kama asingekuwa na good interpersonal skills,nisingepoteza muda wangu kufanya kazi bure.
My challenge to you guys, hadi inafika 2019, jitahidi kujifunza interpersonal skills kuliko kucode au kuomba mkopo,ongea na watu, jichanganye, usipende cheap sana(?), then fanya project yako.
mwisho wa siku hata uwe unajua vipi, bado unahitaji team.
i'm done
 
Tatizo project nyingi za kibongo zinafanywa kwa haraka nakupelekea kuruka baadhi ya SDLC (System Development Life Cycle) mara nyingi coder wengi huangalia design phase, na implement phase na kusahau phase muhimu kama planning and analysis
 
Unajua katika hii field developers wengi tunakaa wenyewe kama wenyewe tu bila kuwa na timu. Hackers ndo hua wanakaa waobkama wao tu. Lkn developer inabidi awe ndani ya timu ambapo kuna watu ambao ni good coordinators na idea providers. Mfano mzuri ni huu

Katika Apple compang steve jobs hakujua hata coding. Jobs hakuwahi hata kuandika even a piece of code for Apple projects sema yy alikua na mwenzake aitwae steve wozniack huyu wozniack alikua ni mchawi wa coding, hadi alifukuzwa shule kisa kuhack web ya college na kutengeneza bombing plank iliowastua wengi hapo college. S

Sasa baada ya wozniak kuteam na jobs unaambiwa wozniak alikua anagive up several times kwa sababu he was coding big things ambavyo havileti faida. Mpaka kuna kipindi wozniack aliuza hisa zake almost zote lkn jobs akazinunua.

So my point ni kwamba unaweza kuwa the best coder ila ukakosa kipato kwa sababu tu hauna mtu wa kukupa ideas. Steve jobs alikua tu anatoa ideas khs Projects za apple kama ipod, iphone na ipads hadi jamaa anajulikana kama iGenius ila hata hakuwahi kufanya coding yyt hapo apple sema tu ni uwezo wake wa kufikiri na kufanya coordination

........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom