Dereva wa basi alivyoniulia mke wangu kipenzi Sara

Andres

JF-Expert Member
Dec 4, 2013
501
791
Siku moja nikiwa nimetoka kwenye shughuli zangu kama miaka miwili hivi iliyopita, mida ya jioni jioni kwa wakazi wengi wa Kimara tusio na magari basi bodaboda au tax za kuchangia ndio usafiri wetu kwa wale tulio mbali na barabara kuu.

Kama ilivyo ada mzee mzima nikaingia kwenye tax za kuchangia, gari ilivyojaa tukaanza kasafari ketu. Hazikupita dk 5 dereva akapewa ishara na watu wa nje kuwa upepo wa tairi umeisha, dereva akatushusha na safari ikaishia hapo tukaingia kwenye usafiri mbadala tuliopewa na Mungu, miguu yetu. Kwangu nilichukulia kawaida tu, lakini haikuwa hivyo kwa jamaa mmoja ambaye yeye alilalamika sana na kudai kwamba dereva hakuwa makini ilibidi awe ameshaangalia gari yake, akaenda mbali zaidi na kusema kuwa asilimia 99 ya ajali husababishwa na madereva.

Kwakweli hapo sikumuunga mkono lakini sikumbishia maana ndo maoni yake na huwa sipendagi mabishano. Tukiwa tunatembea akaniambia unajua kwanini nimekwambia vile, nkamwambia sijui akanionyesha mikono yake iliyokuwa inamishono kuanzia juu mpaka chini, afu akaanza kusema;

Siku moja nikiwa mkoani Shinyanga kwenye shughuli zangu, mke wangu Sara na mwanangu walikuwa kwa wakwe zangu Mbeya, Tukuyu. Baada ya kumaliza mishe zangu huko nikasafiri kwenda Mbeya kumpitia mke wangu na mwanangu halafu sote turejee kwenye makazi yetu Dar es Salaam.

Nakumbuka siku ya safari ya kutoka Mbeya kuja Dar, tulikata tiketi ya basi fulani, saa kumi na mbili asubuhi basi lilikuwa pale tukuyu na mimi na mke wangu pia, kwa vile mimi ni mtu wa vyombo kidogo nikaingia kwenye ka mgahawa nakuanza kupata viroba viwili vitatu, nikiwa pale kuna jamaa naye pembezoni mwangu naye alikuwa anapata vinne vitano, huyu bwana alikuwa balaa, alikuwa anakunywa viroba aina ya Double Punch kwa watu wa Mbeya wanavifahamu ni viroba kutoka malawi, ni vikali sana alcohol zaidi ya 40%, Jamaa alikuwa anavigonga kama hana akili nzuri, zaidi ya vitano namuangalia na nilimkuta keshaanza tayari.

Muda wa safari kuanza ulipofika nikarudi kwenye gari na kumkuta sara wangu na mwanangu aliyekuwa na miezi 9 wakati huo wamekaa kwenye siti ya kwanza kabisa nyuma ya siti ya dereva. Wakati safari inaanza macho yangu yakakutana na sura ya dereva, La Haula! Ndio yule jamaa aliyekuwa anavigonga vile viroba pale mgahawani , moyo ukalia paa. Nikamsimulia mke wangu sara, lakini tukajipa moyo atakuwa amekunywa kidogo tu anayoweza kuhimili na safari yetu ikaanza.

Huyu jamaa alikuwa anatupeleka mputa mputa hatari, kufika mida ya kuchimba dawa kwenye saa mbili hivi, abiria wote tukashuka kwenda kuchimba dawa. Wakati narudi kwenye gari yule dereva akawa anagonga viroba vingine kumbe alinunua vingine akatembea navyo mfukoni mwake, Aisee! Nilivyomuona sikuweza kuvumilia nikamuuliza ndugu yangu si unajua umebeba roho za binadamu humu sio mifugo, wakati tunaondoka tukuyu nilikuona unakunywa viroba tena vingi nikanyamaza, sasa hivi tena unakunywa vingine huoni unahatarisha maisha yetu? Yule dereva akapatwa na jazba akaanza kunifokea na mimi nikaanza kumjibu, kiufupi ukawa mzozo mpaka abiria wengine wakaingilia.

Nikawaelezea mkasa mzima ulivyokuwa, wakati huo dereva ananirushia maneno kwamba nisimfundishe kuendesha gari, kufika au kutokufika salama ni majaliwa ya mwenyezi Mungu kwani wote wanaopata ajali walikuwa wamekunywa? Mzozo ukawa mkubwa wakati huo Sara wangu ananisihi niache kubishana, na abiria wengi wakawa upande wa dereva.

Dereva alidai hajaanza kunywa pombe leo, wala kuendesha leo kwahiyo nisitake kuwa mjuaji, kwakweli nilijisikia vibaya sana hasa kuona kwamba abiria wengi wanamsupport dereva, nikamwambia mke wangu kama vipi tushuke tu hapo hapo porini tutajua nini cha kufanya kuliko kuendeshwa na mlevi. Mke wangu, akanisihi tu nivumilie tu tukiona haendeshi vizuri tutashuka kwenye vituo vikubwa vya mbeleni na sio porini pale.

Nikakubaliana na sara wangu safari ikaendelea ikaanza tena, hazikupita dakika 20 yule jamaa aka overtake kwenye mteremko mkali halafu mbele kuna gari linakuja, akajaribu kulikwepa nachokumbuka nilijiona kama napaa afu mikono inaburuzika chini, tulipata ajali mbaya, gari lilipinduka mara kadhaa, nikavunjika vunjika mikono yangu pale, abiria wengi walifariki pale pale na wengine kuumia vibaya, mke wangu kipenzi Sara alipoteza maisha yake pale pale, na mtoto wetu alikutwa amekaa kwenye kichaka pembeni kama vile ni mtu alimbeba na kumueka pale.

Kwakweli nililia sana nikiwa hospitali, nikaahidi kula sahani moja na yule dereva siku nikipona, kwa takribani miezi sita nilimtafuta yule jamaa bila mafanikio hatimaye nikaamua kusamehe tu maana hawezi kunirudishia Sara wangu lakini tangu hapo madereva nawaona maadui kwangu.

Akiwa anamalizia kinihadithia mimi nikawa nimeshafika home kwangu na yeye bado anaendelea mbele, machozi yalikuwa yakimtoka aiseee, tukaagana na mpaka leo hatujaonana tena, ila aliniambia mwanae anaishi naye mwenyewe kana miaka 2 hivi.
 
Mi kuna kitu kiliwah kunitokea nilikuwa na wife cntasahau.
Nilikuwa mjin kwenye mishe mishe flan sasa nikapak gar pale kwenye msikit wa wa shia. Nikiwa kabla cjashuka kwenye gar nikamwambia wife tulitoe hili gar hapa tukalipaki sehem nyingine cna iman na hiz nyumba wanazojenga mafundi wa kibongo. Huwez kuamini ile naitoa gar naipaki sehem nyingine aisee lile gorofa lilishuka pale pale nilipopak gar b4. Daaa wife akasema tukatoe zaka huyu ni Mungu amesema nasi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom