Dereva Trekta Kanipora mpenzi

Sijaelewa kwa nini umependa kum-identify kama dereva trekta, hakuna namna nyingine ungeweza kumtambulisha na ujumbe ukafika?
 
Hahaha! Ndo dunia hii, cha msingi uvumilivu tu pengine aliye chaguo lako bdo hujampata.
 
NAWAHAKIKISHIENI duniani hakuna jambo jipya, mambo yanajirudia rudia kwa staili tofautitofauti tu. Kuna jambo limenitokea na baada ya kutafakari nimekubali kuwa hakuna jipya duniani nawaambieni.

Kuna binti mmoja hapa kijijini kwetu nilimpenda sana, kwa kweli nilikuwa nimeshapanga lazima nimuoe. Na yeye mwenyewe analijua hilo maana tumeshaongea mara nyingi sana pale kisimani tulipokuwa tukikutana wakati akija kufua au kuteka maji. Najua alikuwa akijua kuwa nampenda sana maana nilikuwa najitahidi kumpa vizawadi mbalimbali.
Nikipata elfu mbili nampa, siku moja nilikwenda mjini nikamnunulia Sketi na kitop, hata nyimbo nilikuwa siku nyingine namuimbia wakati anafua, kwa kweli ilikuwa raha sana, hata wenzie wote kijijini nao walijua kuwa tunapendana.

Mwezi uliopita nimeshangaa nimeenda kisimani kumngojea, kweli kaja, lakini salamu yenyewe kajibu kwa shida. Nimejitahidi kumuuliza tatizo hakujibu lolote la maana, kakataa hata nisimtwishe ndoo ya maji kichwani jambo ambalo tulikuwa tukilifanya kila mara kwa mapenzi makubwa.
Ghafla wakati najitahidi kumbembeleza aniambie tatizo ni nini, akafika jamaa mmoja ambaye ni mgeni kijijini maana sijawahi kumuona, alipomuita jina mpenzi wangu sura ya mpenzi wangu ikalipuka kwa furaha, wakaendelea na salamu zao utadhani mimi sipo, sikuamini. Nikaondoka polepole machozi yakinilengalenga.

Nikamfuata rafiki yake wa karibu na kumuuliza kinaendelea nini? Jibu alikuwa nalo, kumbe yule jamaa mgeni pale kijijini ni dereva wa trekta, kaja kijijini kulima mashamba kwa wanaoweza kukodisha trekta, halafu ana redio kaseti ambayo kampa mpenzi, kwa hiyo mimi nimefutwa sina kitu. Iliniuma sana, maana ni kweli nisingeweza kushindana na mtu ambaye kila siku anaingiza hela akikodishwa kulima shamba na kwa vile ni msimu wa kilimo trekta linatakiwa kila siku.

Mimi hata baiskeli sina. Nikakata tamaa, machozi yakinidondoka. Wakati nawaza haya nikakumbuka kuwa hii ni mara ya pili jambo kama hili linanitokea. Nikakumbuka wakati niko darasa la tatu kulikuwa na msichana mmoja darasani nilikuwa nampenda kweli, kila asubuhi nikifika tu shule, nilikuwa nampelekea kiazi cha kuchoma au siku nyingine andazi.
Nikikaa darasani ilikuwa lazima nimwangalie mara kwa mara, katika akili yangu ya kitoto nilijua huyo ndiye nitakayemuoa nikiwa mkubwa. Najua naye alikuwa akinipenda maana naye akipewa kashata au pipi kwao alikuwa akiniletea, mambo yalikuwa matamu, hata shule nilikuwa nawahi ili tu nimuone anapoingia kwenye geti la shule.

Siku moja tukiwa darasani akaingia mwanafunzi mpya. Kitu ambacho kilikuwa wazi kwanza alikuwa kavaa nguo safi na mpya, pia alivaa viatu vyeusi vya ngozi vinang’aa kwa upya, kitu ambacho kwa shule yetu ya kijiji ilikuwa nadra sana, pili alikuwa kavaa miwani, hakuna hata mwalimu mmoja aliyekuwa na miwani, niliwahi kumuona mzee mmoja toka mjini siku moja ndiye alikuwa amevaa miwani.

Basi wote tukabaki tunamshangaa huyu mwanafunzi mpya baadaye tukaja kuambiwa alikuwa anasoma mjini sasa kaja kuishi kwa bibi yake, kwa kuwa baba yake kapata kazi Dar es Salaam. Kiukweli huyu jamaa aliuteka moyo wa shule nzima. Lakini kubwa zaidi si akauteka na moyo wa mpenzi wangu, nikawa mimi sina maana tena, kashata analetewa yule mtoto mpya mwenye miwani, kimsingi nikaachwa kwa sababu ya miwani.

Sasa ukubwani nimenyang’anywa mpenzi na dereva wa trekta, kweli duniani hakuna jipya.
Na wewe mchukue rafiki yake..
 
Jamaa anamlima sawasawa
 
Eti "hata shule nilikuwa nawahi ili tu nimuone anapoingia kwenye geti la shule".

Uongo wako umeuonesha ktk maneno yaliyokolezwa wino hapo juu bila wewe mwenyewe kujitambua. Tangu lini hapa Tanzania shule za vijijini zikawa na Geti? Kweli njia ya muongo ni fupi!
 
Urefu na mpangilio wa aya ni mzuri.Dhamira ya mwandishi iko wazi.Zaidi ongeza misamiati ya lugha adhim ya Kiswahili mvuto uongezeke.Tumia tanakali za sauti ikibidi,methali na hata misemo.

BTW:Karibu MMU...Natumai jukwaa lako pendwa hujaondoka mazima.
Hii I'd sijaiona muda mrefu humu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom