Dereva taxi achinjwa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
DEREVA teksi aliyefahamika kwa jina la Nicolaus Mwaikambo(25) mkazi wa Kinyanambo mjini Mafinga ameuawa na watu wasio julikana usiku wa kuamkia jana kwa kupigwa kwa kitu kinachodaiwa kuwa ni risasi katika shingo yake na kuweka jeraha kubwa lililotoboa shingo yake na kisha kuondoka na gari alilokuwa akiendesha.

Marehemu ambaye alikuwa akiendesha gari aina ya Corolla yenye namba za usajili T353 AZC alikodiwa majira ya kati ya saa 2:00 na saa 3:30 usiku katika eneo ambalo anaegesha gari lake njia panda ya kuelekea Mufindi karibu na kituo cha mafuta cha Total.

Baadhi ya watu wa karibu na marehemu walidai kuwa,watu watatu walifika katika kituo hicho cha kuegesha teksi na kuhitaji gari ya kukodi ambapo walimchukua marehemu wka lengo la kuwapeleka eneo la Ndolezi nje kidogo ya mji wa Mafinga.

Akizungumzia tukio hilo msimamizi wa teksi hizo aliyefahamika kwa jina la Robert Matanila alisema kuwa, aliachana na marehemu majira ya saa 2:00 usiku na kwamba hata hivyo alielezwa na marehemu kuwa anakwenda kuegesha gari lakini alipata taarifa asubuhi kuwa dereva huyo amekutwa amekufa akiwa na majeraha makubwa mwilini mwake.

Alisema kuwa mwili wa marehemu ulikuwa umeburuzika kama dalili za mapigano baina ya wauaji hao na marehemu ambapo mara baada ya kumuua mwili wake waliutumbukiza katika mto karibu na barabara iendayo Ndolezi.

Majira ya saa 4:00 asubuhi askari polisi wakiwa katika gari aina ya Land Rover Defender walifika karibu na stendi kuu ya mabasi ya mjini Mafinga ambako marehemu alikuwa akiegesha gari lake ambapo madereva hao waliutambua mwili wa marehemu.

Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Bw.Evarist Mangara alisema kuwa bado hajapata taarifa za tukio hilo na kwamba anawasiliana na askari mkuu wa kituo cha polisi Mafinga ili aweze kutolea ufafanuzi tukio hilo.

Aidha baadhi ya maderebva teksi wa eneo hilo wameelezea wasiwasi wa maisha yao na kusema kuwa jeshi la polisi kupitia dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi iwe na mkakati maalumu wa kupambana na uhalifu na mauaji ya madereva teksi ambao yamekuwa yakitishia maisha yao.

‘’Jeshi la polisi litusaidie katika hili…tunafanya kazi kwa hofu ya kuuawa,’’alisema Bw.Nico Luwago dereva teksi wa mjini Mafinga.

Kwa upande wake dereva teksi aliyejitambulisha kwa jina la Boniface Chura anayegesha gari lake karibu na stendi ya mabasi mjini Mafinga alisema kuwa madereva wanatakiwa kuwa na tahadhari na abiria ambao hukodi gari kwa umbali mrefu na kwamba kabla ya safari dereva anatakiwa kutoa taarifa madereva wenzie na ikiwezekana watoe taarifa katika kitruo cha polisi juu ya abiria ambaye wanamtilia mashaka.

Tukio hili la mauaji ya madereva teksi mkoani Irnga ni la tatu kuanzia mwaka jana ambapo katika wilaya ya Mufindi ni tukio la pili.
 
Back
Top Bottom