Tanzania Mpya
JF-Expert Member
- Apr 11, 2012
- 252
- 145
Nilipanda basi la Mwendo Kasi kutoka Kariakoo kwenda Ubungo asubuhi hii kwenye saa 2 na robo hivi.
Nimemshangaa Dereva wa basi namba T144DGW anavyoendesha kwa speed kubwa na kutoacha nafasi ya kutosha kati yake na mwenzake aliye mbele yake! Anafanya michezo kama dereva wa daladala, anamfuata mwenzake kwa karibu mno na kusababisha kufunga breki za ghafla pale mwenzake wa mbele anapopunguza mwendo au kusimama.
Kuna wakati nilihisi kwamba atamgonga yule wa mbele! Hata aliposimama kituo changu cha Shekilango, jamaa anaingia kituoni kwa speed na nafasi aliyoicha kati yake na sakafu ya kituo ni sentimita chache tu tofauti na wenzake wanavyosimama.
Naomba Mamlaka ya husika imuonye Dereva huyo ajirekebishe la sivyo ataisababishia hasara Serikali muda si mrefu. Hawa madereva wakumbuke kwamba haya magari pamoja na miundombinu yake vimegharimu fedha zetu nyingi, kwa hiyo wawe waangalifu.
Nashauri pia wapimwe kama wamelewa kabla ya kukabidhiwa magari hayo.
Mungu ibariki Tanzania.