Dereva huyu wa gari la mwendokasi aonywe!

Mi nafikiri tatizo sio mwendokasi, tatizo ni udereva usio zinagtia kanuni za udereva. Kuendesha bila kuacha mita sita baina yako na aliye mbele ni kosa kubwa sana kwasababu wa mbele akifunga breki ni rahisi kumgonga.

Kuhusu suala la speed sitaki kuzungumza maana kwa ufahamu wangu ni kuwa magari haya ya mwndokasi hayakimbii hata kidogo! Ukweli ni kuwa yameitwa ya mwendokasi kwasababu hayakai kwenye foleni na si kwasababu yanakimbia. Waliopanda magari haya ni mashahidi kuwa magari haya hayafikishi hata spidi 80, muda mwingi yanatembea na spidi 40 hadi 60 au 70 hivi. Mtu anavosema linakimbia lilikuwa spidi ngapi??? Ni bora kusema ukweli kuwa jamaa anaendesha bila kuzingatia taratibu za udereva. Suala la spidi ni ngumu kuthibitisha maana kuna siku nilikuwa nasafiri na dada mmoja akaanza kupiga kelele eti gari inakimbia sana na ilikuwa kwenye spidi 60 hivi! Nilishangaa sana nikaona huu ni upuuzi, kwa spidi ya chini ya 60KPH mwanza ni safari ya wiki nzima hiyo! Kinachoweza kuthibitisha spidi ni speedomiter sio muono, muono mara nyingi ni relative, mwingine ataona inakimbia na mwingine haikimbii. Kuna haja ya watu kutembea na handheld speedometers.
 
Ndani ya hayo mabasi kwenye kioo cha mbele kuna tahadhari iliyoko pale kwa ajili ya kumuonya dereva kuwa ni marufuku kuendesha kwa mwendo wa haraka na ikitokea akifanya hivyo ni kufukuzwa kazi mara moja!!
 
Nilipanda basi la Mwendo Kasi kutoka Kariakoo kwenda Ubungo asubuhi hii kwenye saa 2 na robo hivi. Nimemshangaa Dereva wa basi namba T144DGW anavyoendesha kwa speed kubwa na kutoacha nafasi ya kutosha kati yake na mwenzake aliye mbele yake! Anafanya michezo kama dereva wa daladala, anamfuata mwenzake kwa karibu mno na kusababisha kufunga breki za ghafla pale mwenzake wa mbele anapopunguza mwendo au kusimama. Kuna wakatinilihisi kwamba atamgonga yule wa mbele! Hata aliposimama kituo changu cha Shekilango, jamaa anaingia kituoni kwa speed na nafasi aliyoicha kati yake na sakafu ya kituo ni sentimita chache tu tofauti na wenzake wanavyosimama.

Naomba Mamlaka ya husika imuonye Dereva huyo ajirekebishe la sivyo ataisababishia hasara Serikali muda si mrefu. Hawa madereva wakumbuke kwamba haya magari pamoja na miundombinu yake vimegharimu fedha zetu nyingi, kwa hiyo wawe waangalifu. Nashauri pia wapimwe kama wamelewa kabla ya kukabidhiwa magari hayo.

Mungu ibariki Tanzania.
Nilisikia walikuwa madereva wa daladala
 
Mi nafikiri tatizo sio mwendokasi, tatizo ni udereva usio zinagtia kanuni za udereva. Kuendesha bila kuacha mita sita baina yako na aliye mbele ni kosa kubwa sana kwasababu wa mbele akifunga breki ni rahisi kumgonga.

Kuhusu suala la speed sitaki kuzungumza maana kwa ufahamu wangu ni kuwa magari haya ya mwndokasi hayakimbii hata kidogo! Ukweli ni kuwa yameitwa ya mwendokasi kwasababu hayakai kwenye foleni na si kwasababu yanakimbia. Waliopanda magari haya ni mashahidi kuwa magari haya hayafikishi hata spidi 80, muda mwingi yanatembea na spidi 40 hadi 60 au 70 hivi. Mtu anavosema linakimbia lilikuwa spidi ngapi??? Ni bora kusema ukweli kuwa jamaa anaendesha bila kuzingatia taratibu za udereva. Suala la spidi ni ngumu kuthibitisha maana kuna siku nilikuwa nasafiri na dada mmoja akaanza kupiga kelele eti gari inakimbia sana na ilikuwa kwenye spidi 60 hivi! Nilishangaa sana nikaona huu ni upuuzi, kwa spidi ya chini ya 60KPH mwanza ni safari ya wiki nzima hiyo! Kinachoweza kuthibitisha spidi ni speedomiter sio muono, muono mara nyingi ni relative, mwingine ataona inakimbia na mwingine haikimbii. Kuna haja ya watu kutembea na handheld speedometers.

Safi sana Mkuu! Asante kwa kuelimisha.
 
Nilipanda basi la Mwendo Kasi kutoka Kariakoo kwenda Ubungo asubuhi hii kwenye saa 2 na robo hivi.

Nimemshangaa Dereva wa basi namba T144DGW anavyoendesha kwa speed kubwa na kutoacha nafasi ya kutosha kati yake na mwenzake aliye mbele yake! Anafanya michezo kama dereva wa daladala, anamfuata mwenzake kwa karibu mno na kusababisha kufunga breki za ghafla pale mwenzake wa mbele anapopunguza mwendo au kusimama.

Kuna wakati nilihisi kwamba atamgonga yule wa mbele! Hata aliposimama kituo changu cha Shekilango, jamaa anaingia kituoni kwa speed na nafasi aliyoicha kati yake na sakafu ya kituo ni sentimita chache tu tofauti na wenzake wanavyosimama.

Naomba Mamlaka ya husika imuonye Dereva huyo ajirekebishe la sivyo ataisababishia hasara Serikali muda si mrefu. Hawa madereva wakumbuke kwamba haya magari pamoja na miundombinu yake vimegharimu fedha zetu nyingi, kwa hiyo wawe waangalifu.

Nashauri pia wapimwe kama wamelewa kabla ya kukabidhiwa magari hayo.

Mungu ibariki Tanzania.
Kuna dereva mmoja hivi wanamuita dereva WA mwendokasi. Ana speed zake ukipanda lazima uone tofauti.
 
Kama ulipanda mabas ya mwendo kasi unalalamika anaendesha kwa kasi si ni hatari hii
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Hahahaha
Wa Dar hawaachi kulalamika,sasa wewe ulikuwa ndani ya Gari,je ulimuambia Driver au ulikaa unatoa Macho.
Yaani umeshuka kwenye gari mbio unakimbilia humu,wakati wa kumuambia ni Driver,na pia kuna numbers za Traffic zipo ungewapigia ili washughulikie.
Halafu hakuna speed kubwa kwa umbali wa vituo na pia ufahamaike uwezo wa gari hizo kuruhusiwa speed kwenye maeneo hayo,na pia gari zipo monitored na system na ndio maana Driver aliikunjua.
Ukitaka kujua Speed Panda Ngorika
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Back
Top Bottom