Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,185
- 18,513
Dereva wa Dart aliye endesha gari namba T803 DGV jana jioni linalofanya safari zake Kimara -Kivukoni na jana tarehe 30 May 2016 majira ya jioni alifanya safari ya Kimara- Morocco.
Huyu dereva kwanza anaijua kazi yake, alipo fika Morocco akatukaribisha , yeye anaita "watu wangu wa Kimara" maneno kibao kiasi abiria tukaanza kucheka hata kabla ya kuondoka Morocco.
Tunaanza kuondoka akaanza kutupa ushauri kwa lugha ya kishikaji sana eti anatupa ubuyu ili tusipate shida watu wake wa Kimara kwa kuwa anatupenda sana na hataki tupate shida yoyote.
Akwatwambia mengi kuhusu sheria za dart na matumizi ya barabara, madaraja na vituo pamoja na magari lakini kutokana na jinsi anavyo ongea vizuri kwa bwebwe na akiitumia vizuri kifaa cha sauti abiria wakaanza kufurahi na kupenda kumsikiliza.
Safari ya kutoka Morocco ilikua kama fupi kutokana na entertainments za dereva hadi watu wanapitiliza vituo na baadhi ya abiria kutaka kumpa fedha japo aliwajibu kwa kuwashukuru na kusema waendelee kutumia usafiri salama wa dart.
Kilichonivutia hata kusema apewe bonus kwanza anaipenda kazi yake, pili anaipenda kampuni iliyo mwajiri kwa kuwaekeleza abiria mambo muhimu ya kuzingatia na adhabu wanazo weza kupewa(ubuyu), lakini tatu ni lugha yake nzuri kwa abiria na anavyo mudu matumizi ya kifaa cha sauti, na mengine mengi wengine watasema kama yupo aliye shuhudia jana jioni.
Laiti kama madereva wote wa dart wangekua kama huyu jamaa, watu tungekua tunapanda dart hata kama hatuna safari na wale wenye stress basi zingekua zinaishia dart..
Nilitamani jana nimpongeze kwa meneno tuu bahati mbaya nikashukia njiani.