Wabongo mnazingua kwa Ujuaji usio na msingi.
Kuna namna nyingi za kuonesha una " akili " au " Upeo" tofauti na hii ya kukosoa kila kitu.
1. Simba na Yanga ni timu kama timu Zingine.
2. Kanuni za Ligi kuu zinafahamika.
Bingwa wa FA na Bingwa wa Ligi watacheza Mechi ya Ngao ya hisani kuashiria kuanza kwa ligi ( saiv kanuni imerekebishwa zimekuwa team nne badala ya 2).
3. Haijalishi ni team gani zimechukua kombe na kushika nafasi za juu Ngao ya jamii lazima ifanyike.
4. Uwezo wa uwanja wa mkwakwani ni Mdogo, ukiweka kiingilio Kidogo unaweza sababisha Vurugu. Weka kiingilio kikubwa kupunguza watu.