Deo Kisandu akacha siasa

Deo Kisandu akacha siasa

Hapa ndugu umechemka sana.Sababu halisi si kutelekezwa inavyoonekana maana umechanganya story nyingi hadi UKAWA ndani.Jinsi ulivyojieleza hufai kwa chama chochote labda ukalime tu sasa.

Mkuu Msingida waombe radhi wakulima. Mbona shughuli ya kilimo mnaiona kama ya watu mbumbumbu sana?. Huyu Kisandu hafai kwa lolote na hata degree yake sijui aliipataje! Hivi mtu heading anaandika"sababu za kujivua uanachama" then ndani yake anaingiza aya ya kutoa maoni yake kuhusu bajeti ya serikali,huyo anatimamu kweli? Eti ndg zake wamemkatalia siasa halafu tena anajichanganya kwamba atajiunga na chama muda ukifika! Ni boya sana huyu na mimi naona Sekuco/Sekomu wangemvua tu degree yake(najua sheria hairuhusu ila busara itumike) maana anakiaibisha chuo hicho.
 
Last edited by a moderator:
Unavuna ulichokipanda, dhambi ya usaliti itawatafuna popote muendapo, mala unasingizia Chadema sijui inafanyaje, sasa umeanza kuisingizia NCCR, hiyo ni dhambi ya usaliti inayokutafuna, acha kutapatapa, mulaumu Kibalaka wa ccm Zitto kabwe aliyewapoteza ambaye naye kashapoteana.
 
sipati picha hao watoto watakaofundishwa na kisanduku.mungu aepushie mbali

kumbe ni mwalimu huyu punguwani? sasa badala ya kwenda kufundisha alidhani siasa ndio njia ya mkato ya utajili?

nadhani ushauri wangu kwake na kwa mtela mwampamba wakaombe ajila za ualimu kwenye siasa si sehemu ya kusaka tonge.
 
Alipo anza tu kuitukana NCCR nikajua kitakachofuatia ni hiki na ninajua kitakacho fuatia baadae ni kipi!!!

CCM mpokeeni mtu wenu
 
Ningempa mdogo wangu wa darasa la saba kazi ya kuandika insha akaandika kitu hakijapangiliwa wala hakina mantiki kama hiki, nadhani nitashauri anyimwe chakula home kwa siku 2...
 
Sikutaka ku~log In, Ila kwakua nimeona kinyesi humu acha nishiriki kukisafisha .
Kisandu miaka mitatu hivi nyuma ulipojitoa CDM na kujiunga NCCR ndio ilikua mara yangu ya kwanza kukusikia, Ila moyoni kwakua,ulitangazwa hadi magazetini nikajua wewe ni Mwanasiasa mahiri mithiri ya kina Kafulila.

Ambacho nimekiona kwamo ni kitu kidogo tu , Umekua msaliti wa Nafsi yako , Na hilo ndilo kosa kubwa litakalotesa moyo na nafsi yako kwa miaka mingi Ijayo.
Ulifanya siasa kama njia ya kusaka,mafanikio ya haraka. Hapa hukuwa na subira wala simile kila mtu akijitokeza kugusa kila unachoamini kuwa ni njia yako ya kupiga bingo.

Siasa unayojaribu kushiriki ni siasa hafifu mnoo . siasa ya kulia na kudeka kila mara, siasa yako si sehemu yabufumbuzi wa matatizo.

NccR hawana cha kupoteza kwa kuondoka kwako ila gunia la kinyesi,lilosogezwa mbali. Nafikiri wala hawana chakujuta bali kujilaumu kwakutumiaka kama kokoro la kuokota kila mwanasiasa aliefukuzwa atokako kisha kumoa madaraka na kumuamini kama walivyofanya kwa huyu Kisandu.

Basi, Uende , uende , Uende siasa si Kitu cha kipuuzi kama kiwango chako cga,kufikiri kilivyo
 
KATIBA MPYA: Maoni ya S2 ni maoni ya wananchi na maoni ya S3 ni maoni ya wananchi! I pray that hiyo ajali haikutengua pia mendulla oblongota yako. Kwenye katiba mpya you have sucked a lot!
 
TAMKO LA KUJIVUA UANACHAMA WA CHAMA CHA NCCR – MAGEUZI 17 Juni 2014. 1 :0 UTANGULIZI Ndugu wana habari na ndugu Watanzania, kwa kutambua mchango wangu mkubwa ambao nimkuwa nikiufanya katika ujenzi wa vyama vya siasa hasa Upinzani hapa nchini, ni dhahiri nimekuwa mjenzi wa vyama kuliko mafanikio ya wananchi. Nimegundua mengi sana na kujifunza mengi sana juu ya hivyo vyama vyetu vya Siasa, tunapotafuta demokrasia katika nchi yetu sio tu kuwa huru kwa kila jambo bali kuwa na UTU kwa watu tunaowatafutia Demokrasia ya kweli, hatuwezi kusema nchi haina demokrasia kama hatujatenda haki kwa wanachama au wananchi wetu. SABABU ZA KUJIUDHURU UANACHAMA NA NYADIFA ZOTE ZA UONGOZI. 2 :0 AJALI YA GARI Mwaka jana June 2013 kulikuwa na uchaguzi mdogo wa Udiwani Wilayani sengerema Kata ya Nyampulukano na mimi nikiwa msimamizi wa Uchaguzi huo mdogo wa marudio, jumamosi ya kuamkia uchaguzi tulipata ajali ya gari tukitoka kukagua vituo vya kupigia kura na mimi nilikuwa kiti cha mbele cha gari na nikapata maumivu makali sana, japo nilipewa huduma ya kwanza lakini baada ya hapo sikupata matibabu stahiki kitu ambacho mpaka sasa, nisingeweza kulaumu kama hawajui lakini wanajua fika viongozi wenzangu, na ukizingatia wakati ule nilikuwa Katibu wa Mahusiano na Uenezi Taifa kitengo cha Vijana. Kutokana na hali kuwa si nzuri na kufikia kuona nalalamika ujue kabisa hali si nzuri ki afya, jambo la msingi kwa wenzangu hata kama wanahisi na makosa lakini jambo la Busara ni UTU kwanza wakumponya aliye mgonjwa ndipo busara zingine zinafanyika, kiukweli nasikitika sana na ninaumia sana kwa tukio hili maana ile ilikuwa ni kazi ya chama na siya mtu, ina maana hata Elfu kumi tu nayo ni ngumu ? kweli hapa tujiulize sasa, na ndio maana naumia sana kwa hilo, kwa hili mimi naona kama wamenitelekeza na kuniachia familia yangu mzigo. Nashauri tu kuwa vijana wenzangu wa Kitanzania tunapo jiunga na vyama vya Siasa tuchunguze UTU kwanza kabla hatujafikia maamuzi na tusiwe washabiki wasiasa bila kujua hatima yetu kimaisha, nashauri kama vijana tuwe tunasapotiana kwenye matatizo maana leo limemkuta Kisandu kesho linakuja kwako. Nimejaribu hatakuomba msaada kwa baadhi ya viongozi rafiki msaada wa aina yoyote bila mafanikio. USHAURI WANGU kwa chama changu NCCR – Mageuzi naomba kama hili limetokea kwangu basi lisijirudie kwa mwingine kwani hata Mungu hapendi kuona hali kama hizo. Kutokana na hili la matibabu ndugu na familia yangu wamenishauri niachane na Siasa za vyama ili waweze kuona wananisaidia vipi, kimsingi naungana na ndugu zangu na kukubali ombi lao kuliko kuumia namna hii. Naomba msamaha kwa viongozi wenzangu pale tulipo kwazana na mimi na wasamehe pale walipo nikosea japo nabaki na maumivu ya kiafya. 3 :0 KATIBA MPYA Kwa upande wa swala la KATIBA MPYA, huu mchakato si wa mtu mmoja au watu kadhaa bali ni mchakato wa Watanzania wote. Swala la Muundo wa Muungano si swala la CCM wala UKAWA bali ni letu sote, hapa ningeshauri tu kuepuka mvutano baina ya serikali mbili au Serikali tatu, wakakaa pamoja na kufikia maridhiano yenye Busara ili tupate Katiba mpya inayoendana na mazingira ya Kitanzania. Pia lazima wawakilishi wetu Bunge la Katiba watambue kuwa maoni ya Serikai mbili ni ya Wananchi na Maoni ya Serikali tatu nayo pia ni ya Wananchi hivyo Busara ndio itumike kurejesha Umoja wetu wenye katiba ya pamoja. 4 :0 KUHUSU BAJETI YA SERIKALI MWAKA HUU Viongozi wetu watambue kuwa Bajeti hii ni ya Watanzania wote hivyo badala ya kukosoa tunapaswa kuboresha na tusikosoe bila kuiboresha maana kama tutakosoa tu mwisho wa siku tutakuwa hatuja tibu chochote bali serikali ikosolewe kwa kupewa solution. 5:0 UKAWA Hakuna dhambi mbaya kama dhambi ya ubaguzi, Baba au Mama akibagua baadhi ya watoto tena wadamu ni dhambi kali sana ya ubaguzi inayohitaji kukemewa. Ndugu zangu wanao jiita UKAWA hawa jamaa si wazalendo kabisa wametawaliwa na dhambi ya ubaguzi wa vyama. Vyama vya Siasa vipo 23, vyama 22 vikawa ni vyama vya Upinzani, iweje leo wote ni wapinzani eti UKAWA iwe ya vyama vitatu vya upinzani fikiria kama ni uchaguzi Mkuu, vyama vitatu kugombea uchaguzi haisaidii maana hata robo haijafika. Ubaguzi uliofanywa na hawa jamaa hauvumiliki kabisa na si vitendo bali ni Umoja ndani ya Mtengano. Wakiweza kuungana vyote vyama 22 vikawa UKAWA basi nitakuwa tayari kuendelea na siasa na hata Serikali 3 nitaunga mkono lakini dhambi ya kubaguana ya vyama itaendelea basi ni heri Serikali 2 au 1 maana UKAWA ni ya vyama vitatu na si ya wananchi maana ya UKAWA ya wananchi ni ya vyama vyote 22 vya Upinzani dhambi ya ubaguzi iacheni ni Pepo mchafu. 6:0 FIKRA MBADALA Vijana wenzangu tuache mihemko na jaziba katika ushabiki wa mambo ya kisiasa na tuhamie katika uzalendo wa kujenga nchi yeye Amani na Uzalendo bila kujali itikadi za vyama vyetu na tusijikite kuchagua vyama bali tuchague viongozi wanaotufaa bila kujali Ushabiki wa vyama. 7:0 MAPUMZIKO Kwa sasa nimeamua kupumzika siasa na kuangalia mstakabli wa maisha ya kifamilia kwanza, pamoja na kupumzika huko nitapumzika na kwamba nitakuwa naelekea chama gani hilo si swala la leo mpaka pale nitakapooona inafaa na sijui ni lini. Ndugu wanahabari nifikishieni taarifa hii kwa umma wa Watanzania na Mungu atupe uzima wa maisha marefu. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA. MWL. DEOGRATIUS KISANDU ALIYEKUWA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU TAIFA NCCR – MAGEUZI 17 / 06 / 2014
CCM mimi nawasifu sana kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa vijana wajinga wajinga kama KISANDU. Huna tofauti na ile mipira yetu ile. la kukushauri kijana kisandu kwa vile njaa ndio inayokusumbua wewe nenda kwa ccm wezi wenzako mkashirikiane vizuri kuwaibia watanzania maana huna jipya. Hivyo vyama 22 unavyovitetea vinafanana na wewe,viko pale kuua vyama vya upinzani vyenye nguvu. kama unaona ni vyma vya upinzani nenda kajiunge navyo Wewe kwa sasa ni useless
 
Kisandu is worthless, infact worthless like a toilet paper.
 
Huyu Deogratias Kisandu ndio nani? Mbona alalamika kutibiwa na NCCR, analilia buku kumi?
 
Huyu Deogratias Kisandu ndio nani? Mbona alalamika kutibiwa na NCCR, analilia buku kumi?

Huyu ni kijana mtiifu wa chama kilichomtuma awe mamluki kwenye vyama vya upinzani. Alitangulia kutoka miguu badala ya kichwa. Hamjui babaye halisi wa kumzaa. Unataka kujua zaidi ya hapo?
 
Dah!Kaka yangu,ndugu yangu,swahiba wangu Mhe.Mwl.Deogratius Pio Kisandu...

Hatimae yamekufika,ila kwa style hii ya uandishi wa press yako sijaipenda na wewe ni Mwl.wa sekondari tena mwenye degree ya Special Education mahili wa kiswahili,kama wewe umeshindwa kupangilia press yako,watoto wetu unawafundishaje au ndo stress za ajali?!

Kosa ulilokosewa NCCR ni dogo sana na kama wewe ulikuwa mpiganaji wa kweli hiyo sio sababu ya kukuondoa kwenye chama ambacho misngi yake unaiamini na kuitumikia.

Suala la wewe kuweka mambo ya bajeti na UKAWA kwenye press yako pia linazidi kutatanisha tu kwani mantiki ya press yako ni ipi hasa?Ukisema UKAWA na CCM wakae meza moja unataka wapitishe yapi?Kwani maoni ya wananchi ni kuwa na muundo wa serikali 3 na CCM hawana muda,ni yupi ajirudi na arejee kwenye matakwa ya wananchi?

Karibu Mwamala sekondari kwa mara nyingine tena ama unabaki Mkolani Sekondari tu?!! Pole kaka yangu.
 
TAMKO LA KUJIVUA UANACHAMA WA CHAMA CHA
NCCR – MAGEUZI 17 Juni 2014.


4 :0 KUHUSU BAJETI YA SERIKALI MWAKA HUU
Viongozi wetu watambue kuwa Bajeti hii ni ya Watanzania wote hivyo badala ya kukosoa tunapaswa kuboresha na tusikosoe bila kuiboresha maana kama tutakosoa tu mwisho wa siku tutakuwa hatuja tibu chochote bali serikali ikosolewe kwa kupewa solution.

5:0 UKAWA
Hakuna dhambi mbaya kama dhambi ya ubaguzi, Baba au Mama akibagua baadhi ya watoto tena wadamu ni dhambi kali sana ya ubaguzi inayohitaji kukemewa. Ndugu zangu wanao jiita UKAWA hawa jamaa si wazalendo kabisa wametawaliwa na dhambi ya ubaguzi wa vyama. Vyama vya Siasa vipo 23, vyama 22 vikawa ni vyama vya Upinzani, iweje leo wote ni wapinzani eti UKAWA iwe ya vyama vitatu vya upinzani fikiria kama ni uchaguzi Mkuu, vyama vitatu kugombea uchaguzi haisaidii maana hata robo haijafika. Ubaguzi uliofanywa na hawa jamaa hauvumiliki kabisa na si vitendo bali ni Umoja ndani ya Mtengano. Wakiweza kuungana vyote vyama 22 vikawa UKAWA basi nitakuwa tayari kuendelea na siasa na hata Serikali 3 nitaunga mkono lakini dhambi ya kubaguana ya vyama itaendelea basi ni heri Serikali 2 au 1 maana UKAWA ni ya vyama vitatu na si ya wananchi maana ya UKAWA ya wananchi ni ya vyama vyote 22 vya Upinzani dhambi ya ubaguzi iacheni ni Pepo mchafu.

6:0 FIKRA MBADALA
Vijana wenzangu tuache mihemko na jaziba katika ushabiki wa mambo ya kisiasa na tuhamie katika uzalendo wa kujenga nchi yeye Amani na Uzalendo bila kujali itikadi za vyama vyetu na tusijikite kuchagua vyama bali tuchague viongozi wanaotufaa bila kujali Ushabiki wa vyama.

7:0 MAPUMZIKO
Kwa sasa nimeamua kupumzika siasa na kuangalia mstakabli wa maisha ya kifamilia kwanza, pamoja na kupumzika huko nitapumzika na kwamba nitakuwa naelekea chama gani hilo si swala la leo mpaka pale nitakapooona inafaa na sijui ni lini.

Ndugu wanahabari nifikishieni taarifa hii kwa umma wa Watanzania na Mungu atupe uzima wa maisha marefu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.

MWL. DEOGRATIUS KISANDU
ALIYEKUWA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU TAIFA NCCR – MAGEUZI 17 / 06 / 2014

Bwana Deo,

Pole sana na ajali iliyokupata. Sasa nimeamini kuwa kweli ulipata ajali. Na sii ajali ndogo kama unavyofikiri. Inaonekana imeathiri mpaka mpaka ubongo na huenda ubongo ulitikisika ukaathiri hata uwezo wa kufikiri. Nikiangalia taarifa yako imejaa mambo ambayo kwa mtu mwenye uwezo wa kufikiri, kuna hoja ambazo asingezitoa.

Kwenye suala la bajeti na wewe umelalamika na kukosoa tu. Huajatoa suluhisho. Au ndo tuite nyani haoni kundule?

Suala la Ukawa umeviuliza hivyo vyama vingine kwa nini havijajiunga vikakwambia kuwa vilizuiwa? Kama memory centre yako haijaathiriwa na ajali unakumbuka alichokisema Isack Cheyo na Peter Mziray ndani ya Bunge la katiba baada ya wana Ukawa kutoka? Una uhakika kuwa Ukawa ni vyama vitatu tu? DP, NLD si vyama vya upinzani?

Familia inayo kila haki kukuzuia kuendelea na siasa maana unawaaibisha kwa unachoandika. Subiri familia ikutibu kwanza, ukishapata kumbukumbu vizuri najua hawatakuzuia kuendelea na siasa.
 
Bwana Deo,

Pole sana na ajali iliyokupata. Sasa nimeamini kuwa kweli ulipata ajali. Na sii ajali ndogo kama unavyofikiri. Inaonekana imeathiri mpaka mpaka ubongo na huenda ubongo ulitikisika ukaathiri hata uwezo wa kufikiri. Nikiangalia taarifa yako imejaa mambo ambayo kwa mtu mwenye uwezo wa kufikiri, kuna hoja ambazo asingezitoa.

Kwenye suala la bajeti na wewe umelalamika na kukosoa tu. Huajatoa suluhisho. Au ndo tuite nyani haoni kundule?

Suala la Ukawa umeviuliza hivyo vyama vingine kwa nini havijajiunga vikakwambia kuwa vilizuiwa? Kama memory centre yako haijaathiriwa na ajali unakumbuka alichokisema Isack Cheyo na Peter Mziray ndani ya Bunge la katiba baada ya wana Ukawa kutoka? Una uhakika kuwa Ukawa ni vyama vitatu tu? DP, NLD si vyama vya upinzani?

Familia inayo kila haki kukuzuia kuendelea na siasa maana unawaaibisha kwa unachoandika. Subiri familia ikutibu kwanza, ukishapata kumbukumbu vizuri najua hawatakuzuia kuendelea na siasa.

Familia itatibu nini maana ubongo wake haupo sawa.Huyo anywe vidonge tu vya kupunguza hayo matatizo yake ya ubongo namaanisha uchizi.
 
Familia itatibu nini maana ubongo wake haupo sawa.Huyo anywe vidonge tu vya kupunguza hayo matatizo yake ya ubongo namaanisha uchizi.

Alikumbwa na ile kitu wataalam mnaiita "brein konkashen" ila yake imemuacha na pumzi ndo maana tunaona anaropokaropoka hapa.
 
Akiibuka tena utamsikia kwenye majukwaa ya CCM. I knew this was coming!!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app

Jamaa toka akiwa cdm anapenda kujitangaza sana..

Kuna wakati alidai anawania urais kupitia cdm.
 
Bwana Deo,

Pole sana na ajali iliyokupata. Sasa nimeamini kuwa kweli ulipata ajali. Na sii ajali ndogo kama unavyofikiri. Inaonekana imeathiri mpaka mpaka ubongo na huenda ubongo ulitikisika ukaathiri hata uwezo wa kufikiri. Nikiangalia taarifa yako imejaa mambo ambayo kwa mtu mwenye uwezo wa kufikiri, kuna hoja ambazo asingezitoa.

Kwenye suala la bajeti na wewe umelalamika na kukosoa tu. Huajatoa suluhisho. Au ndo tuite nyani haoni kundule?

Suala la Ukawa umeviuliza hivyo vyama vingine kwa nini havijajiunga vikakwambia kuwa vilizuiwa? Kama memory centre yako haijaathiriwa na ajali unakumbuka alichokisema Isack Cheyo na Peter Mziray ndani ya Bunge la katiba baada ya wana Ukawa kutoka? Una uhakika kuwa Ukawa ni vyama vitatu tu? DP, NLD si vyama vya upinzani?

Familia inayo kila haki kukuzuia kuendelea na siasa maana unawaaibisha kwa unachoandika. Subiri familia ikutibu kwanza, ukishapata kumbukumbu vizuri najua hawatakuzuia kuendelea na siasa.
wewe ni mstaarabu.
 
Back
Top Bottom