Deo Kisandu akacha siasa

Deo Kisandu akacha siasa

Atakwambia mbona Nyerere alikuwa Mwalimu.....

Alikuwa Mwalimu mwenye akili ambaye hakusukumwa na tamaa za kutajirikia kwenye siasa. Hawa wanaingia leo, kesho wanataka wawe na nyumba na magari mawili-mawili. Siasa ni utumishi wa umma. Utumishi wa umma ni kukubali maisha ya kiasi.
 
TAMKO LA KUJIVUA UANACHAMA WA CHAMA CHA
NCCR – MAGEUZI 17 Juni 2014.

1 :0 UTANGULIZI
Ndugu wana habari na ndugu Watanzania, kwa kutambua mchango wangu mkubwa ambao nimkuwa nikiufanya katika ujenzi wa vyama vya siasa hasa Upinzani hapa nchini, ni dhahiri nimekuwa mjenzi wa vyama kuliko mafanikio ya wananchi. Nimegundua mengi sana na kujifunza mengi sana juu ya hivyo vyama vyetu vya Siasa, tunapotafuta demokrasia katika nchi yetu sio tu kuwa huru kwa kila jambo bali kuwa na UTU kwa watu tunaowatafutia Demokrasia ya kweli, hatuwezi kusema nchi haina demokrasia kama hatujatenda haki kwa wanachama au wananchi wetu.

SABABU ZA KUJIUDHURU UANACHAMA NA NYADIFA ZOTE ZA UONGOZI.

2 :0 AJALI YA GARI
Mwaka jana June 2013 kulikuwa na uchaguzi mdogo wa Udiwani Wilayani sengerema Kata ya Nyampulukano na mimi nikiwa msimamizi wa Uchaguzi huo mdogo wa marudio, jumamosi ya kuamkia uchaguzi tulipata ajali ya gari tukitoka kukagua vituo vya kupigia kura na mimi nilikuwa kiti cha mbele cha gari na nikapata maumivu makali sana, japo nilipewa huduma ya kwanza lakini baada ya hapo sikupata matibabu stahiki kitu ambacho mpaka sasa, nisingeweza kulaumu kama hawajui lakini wanajua fika viongozi wenzangu, na ukizingatia wakati ule nilikuwa Katibu wa Mahusiano na Uenezi Taifa kitengo cha Vijana.

Kutokana na hali kuwa si nzuri na kufikia kuona nalalamika ujue kabisa hali si nzuri ki afya, jambo la msingi kwa wenzangu hata kama wanahisi na makosa lakini jambo la Busara ni UTU kwanza wakumponya aliye mgonjwa ndipo busara zingine zinafanyika, kiukweli nasikitika sana na ninaumia sana kwa tukio hili maana ile ilikuwa ni kazi ya chama na siya mtu, ina maana hata Elfu kumi tu nayo ni ngumu ? kweli hapa tujiulize sasa, na ndio maana naumia sana kwa hilo, kwa hili mimi naona kama wamenitelekeza na kuniachia familia yangu mzigo.

Nashauri tu kuwa vijana wenzangu wa Kitanzania tunapo jiunga na vyama vya Siasa tuchunguze UTU kwanza kabla hatujafikia maamuzi na tusiwe washabiki wasiasa bila kujua hatima yetu kimaisha, nashauri kama vijana tuwe tunasapotiana kwenye matatizo maana leo limemkuta Kisandu kesho linakuja kwako. Nimejaribu hatakuomba msaada kwa baadhi ya viongozi rafiki msaada wa aina yoyote bila mafanikio.

USHAURI WANGU kwa chama changu NCCR – Mageuzi naomba kama hili limetokea kwangu basi lisijirudie kwa mwingine kwani hata Mungu hapendi kuona hali kama hizo.

Kutokana na hili la matibabu ndugu na familia yangu wamenishauri niachane na Siasa za vyama ili waweze kuona wananisaidia vipi, kimsingi naungana na ndugu zangu na kukubali ombi lao kuliko kuumia namna hii. Naomba msamaha kwa viongozi wenzangu pale tulipo kwazana na mimi na wasamehe pale walipo nikosea japo nabaki na maumivu ya kiafya.

3 :0 KATIBA MPYA
Kwa upande wa swala la KATIBA MPYA, huu mchakato si wa mtu mmoja au watu kadhaa bali ni mchakato wa Watanzania wote. Swala la Muundo wa Muungano si swala la CCM wala UKAWA bali ni letu sote, hapa ningeshauri tu kuepuka mvutano baina ya serikali mbili au Serikali tatu, wakakaa pamoja na kufikia maridhiano yenye Busara ili tupate Katiba mpya inayoendana na mazingira ya Kitanzania. Pia lazima wawakilishi wetu Bunge la Katiba watambue kuwa maoni ya Serikai mbili ni ya Wananchi na Maoni ya Serikali tatu nayo pia ni ya Wananchi hivyo Busara ndio itumike kurejesha Umoja wetu wenye katiba ya pamoja.

4 :0 KUHUSU BAJETI YA SERIKALI MWAKA HUU
Viongozi wetu watambue kuwa Bajeti hii ni ya Watanzania wote hivyo badala ya kukosoa tunapaswa kuboresha na tusikosoe bila kuiboresha maana kama tutakosoa tu mwisho wa siku tutakuwa hatuja tibu chochote bali serikali ikosolewe kwa kupewa solution.

5:0 UKAWA
Hakuna dhambi mbaya kama dhambi ya ubaguzi, Baba au Mama akibagua baadhi ya watoto tena wadamu ni dhambi kali sana ya ubaguzi inayohitaji kukemewa. Ndugu zangu wanao jiita UKAWA hawa jamaa si wazalendo kabisa wametawaliwa na dhambi ya ubaguzi wa vyama. Vyama vya Siasa vipo 23, vyama 22 vikawa ni vyama vya Upinzani, iweje leo wote ni wapinzani eti UKAWA iwe ya vyama vitatu vya upinzani fikiria kama ni uchaguzi Mkuu, vyama vitatu kugombea uchaguzi haisaidii maana hata robo haijafika. Ubaguzi uliofanywa na hawa jamaa hauvumiliki kabisa na si vitendo bali ni Umoja ndani ya Mtengano. Wakiweza kuungana vyote vyama 22 vikawa UKAWA basi nitakuwa tayari kuendelea na siasa na hata Serikali 3 nitaunga mkono lakini dhambi ya kubaguana ya vyama itaendelea basi ni heri Serikali 2 au 1 maana UKAWA ni ya vyama vitatu na si ya wananchi maana ya UKAWA ya wananchi ni ya vyama vyote 22 vya Upinzani dhambi ya ubaguzi iacheni ni Pepo mchafu.

6:0 FIKRA MBADALA
Vijana wenzangu tuache mihemko na jaziba katika ushabiki wa mambo ya kisiasa na tuhamie katika uzalendo wa kujenga nchi yeye Amani na Uzalendo bila kujali itikadi za vyama vyetu na tusijikite kuchagua vyama bali tuchague viongozi wanaotufaa bila kujali Ushabiki wa vyama.

7:0 MAPUMZIKO
Kwa sasa nimeamua kupumzika siasa na kuangalia mstakabli wa maisha ya kifamilia kwanza, pamoja na kupumzika huko nitapumzika na kwamba nitakuwa naelekea chama gani hilo si swala la leo mpaka pale nitakapooona inafaa na sijui ni lini.

Ndugu wanahabari nifikishieni taarifa hii kwa umma wa Watanzania na Mungu atupe uzima wa maisha marefu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.

MWL. DEOGRATIUS KISANDU
ALIYEKUWA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU TAIFA NCCR – MAGEUZI 17 / 06 / 2014

Huyu dogo hawezi kujitoa mhanga we rudi shule kafundishe.
 
Mwehu, huyu jamaa ,leo bado a nafikiri ana heshima hata hapa JUKWAANI kutuandikia ujinga huu......we are tired ......
 
"Suala la muundo wa muungano si la ccm wala ukawa, ni letu sote".

Kauli hiyo ni ya kijinga kabisa! Inawezekana tatizo kubwa ni wengi kutokuelewa maana halisi ya "rasimu ya katiba ya wananchi"

Katika utaratibu uliotumika, maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Warioba, ambayo ndo msingi wa upatikanaji wa katiba yetu mpya, yanatuwakilisha sisi "sote".

Kusema suala la muungano/katiba mpya ni "letu sote" na si la ccm wala ukawa, Inaonyesha kutokuuelewa huu mchakato wa katiba mpya!

Nafasi ya UKAWA si kuepeleka maoni yao kwenye bunge la katiba vs CCM,, bali kuisimamia rasimu ya katiba ambayo Inawakilisha maoni yetu sisi wananchi kuhusiana na katiba mpya!

Pole sana Kisandu! Mlijiingiza kwenye siasa kwa maslahi binafsi.Ukombozi wa nchi siyo starehe! Ulizia Fidel Castro et al, fuatilia maisha ya wapigania uhuru na watetezi wa wanyonge na wapigania haki uone kama walihudumiwa kila kitu!
 
Huyu Kisandu ni msaka tonge kupitia siasa. CCM hatuhitaji watu wa dizaini hii.

Mnamkataa jembe huoni anatetea serikali 2 ambayo ndo msimamo wa chama chetu cha magamba. Huoni alivyofanya upembuzi yakinifu dhidi ya udhaifu wa upinzani nchini, huoni alivotukana ukawa lakini bado unamkataa!!?
 
Bila shaka vijana wenzako waliochepuka na kuacha njia kuu watapokea ushauri wako kwa mikono miwili.
 
Anasubiri kwenda ACT I knew this was coming alipoanza porojo juzi.

Sasa mbona alikuwa anaangaika kama mtu anayeoga nje,
si unafiki wa wazi kabisa unaonekana, hicho chama cha ACT naona patachimbika maana sijuhi nani atakuwa kiongozi na nani atakuwa mwanachama wa Kawaida

Hapo ndio kwa anagalau unaweza kukubaliana na CHADEMA kuwa kulikuwa na wanafiki ndani ya chama, maana mtu hata hajatulia ndani ya NCCR tayari nao ni wabaya
 
Hizi dalili za kwenda ccm....nenda angalau ukapate tonge kama stela na shonza

Sent from my iPhone 5 using JamiiForums
 
Used condoms zinajisalimisha duh!!!!

cc Mtella Mwampamba, Juliana Shonza na Chriss Lukosi..nyie mtajisalimisha lina.??
Jose na Kisandu yamewashinda!!
 
Hii dhambi yako ya usaliti iliyokutafuna , ITAFIKA HADI KWA WANAO , USALITI NI LAANA ENDELEVU !
 
TAMKO LA KUJIVUA UANACHAMA WA CHAMA CHA
NCCR – MAGEUZI 17 Juni 2014.

1 :0 UTANGULIZI
Ndugu wana habari na ndugu Watanzania, kwa kutambua mchango wangu mkubwa ambao nimkuwa nikiufanya katika ujenzi wa vyama vya siasa hasa Upinzani hapa nchini, ni dhahiri nimekuwa mjenzi wa vyama kuliko mafanikio ya wananchi. Nimegundua mengi sana na kujifunza mengi sana juu ya hivyo vyama vyetu vya Siasa, tunapotafuta demokrasia katika nchi yetu sio tu kuwa huru kwa kila jambo bali kuwa na UTU kwa watu tunaowatafutia Demokrasia ya kweli, hatuwezi kusema nchi haina demokrasia kama hatujatenda haki kwa wanachama au wananchi wetu.

SABABU ZA KUJIUDHURU UANACHAMA NA NYADIFA ZOTE ZA UONGOZI.

2 :0 AJALI YA GARI
Mwaka jana June 2013 kulikuwa na uchaguzi mdogo wa Udiwani Wilayani sengerema Kata ya Nyampulukano na mimi nikiwa msimamizi wa Uchaguzi huo mdogo wa marudio, jumamosi ya kuamkia uchaguzi tulipata ajali ya gari tukitoka kukagua vituo vya kupigia kura na mimi nilikuwa kiti cha mbele cha gari na nikapata maumivu makali sana, japo nilipewa huduma ya kwanza lakini baada ya hapo sikupata matibabu stahiki kitu ambacho mpaka sasa, nisingeweza kulaumu kama hawajui lakini wanajua fika viongozi wenzangu, na ukizingatia wakati ule nilikuwa Katibu wa Mahusiano na Uenezi Taifa kitengo cha Vijana.

Kutokana na hali kuwa si nzuri na kufikia kuona nalalamika ujue kabisa hali si nzuri ki afya, jambo la msingi kwa wenzangu hata kama wanahisi na makosa lakini jambo la Busara ni UTU kwanza wakumponya aliye mgonjwa ndipo busara zingine zinafanyika, kiukweli nasikitika sana na ninaumia sana kwa tukio hili maana ile ilikuwa ni kazi ya chama na siya mtu, ina maana hata Elfu kumi tu nayo ni ngumu ? kweli hapa tujiulize sasa, na ndio maana naumia sana kwa hilo, kwa hili mimi naona kama wamenitelekeza na kuniachia familia yangu mzigo.

Nashauri tu kuwa vijana wenzangu wa Kitanzania tunapo jiunga na vyama vya Siasa tuchunguze UTU kwanza kabla hatujafikia maamuzi na tusiwe washabiki wasiasa bila kujua hatima yetu kimaisha, nashauri kama vijana tuwe tunasapotiana kwenye matatizo maana leo limemkuta Kisandu kesho linakuja kwako. Nimejaribu hatakuomba msaada kwa baadhi ya viongozi rafiki msaada wa aina yoyote bila mafanikio.

USHAURI WANGU kwa chama changu NCCR – Mageuzi naomba kama hili limetokea kwangu basi lisijirudie kwa mwingine kwani hata Mungu hapendi kuona hali kama hizo.

Kutokana na hili la matibabu ndugu na familia yangu wamenishauri niachane na Siasa za vyama ili waweze kuona wananisaidia vipi, kimsingi naungana na ndugu zangu na kukubali ombi lao kuliko kuumia namna hii. Naomba msamaha kwa viongozi wenzangu pale tulipo kwazana na mimi na wasamehe pale walipo nikosea japo nabaki na maumivu ya kiafya.

3 :0 KATIBA MPYA
Kwa upande wa swala la KATIBA MPYA, huu mchakato si wa mtu mmoja au watu kadhaa bali ni mchakato wa Watanzania wote. Swala la Muundo wa Muungano si swala la CCM wala UKAWA bali ni letu sote, hapa ningeshauri tu kuepuka mvutano baina ya serikali mbili au Serikali tatu, wakakaa pamoja na kufikia maridhiano yenye Busara ili tupate Katiba mpya inayoendana na mazingira ya Kitanzania. Pia lazima wawakilishi wetu Bunge la Katiba watambue kuwa maoni ya Serikai mbili ni ya Wananchi na Maoni ya Serikali tatu nayo pia ni ya Wananchi hivyo Busara ndio itumike kurejesha Umoja wetu wenye katiba ya pamoja.

4 :0 KUHUSU BAJETI YA SERIKALI MWAKA HUU
Viongozi wetu watambue kuwa Bajeti hii ni ya Watanzania wote hivyo badala ya kukosoa tunapaswa kuboresha na tusikosoe bila kuiboresha maana kama tutakosoa tu mwisho wa siku tutakuwa hatuja tibu chochote bali serikali ikosolewe kwa kupewa solution.

5:0 UKAWA
Hakuna dhambi mbaya kama dhambi ya ubaguzi, Baba au Mama akibagua baadhi ya watoto tena wadamu ni dhambi kali sana ya ubaguzi inayohitaji kukemewa. Ndugu zangu wanao jiita UKAWA hawa jamaa si wazalendo kabisa wametawaliwa na dhambi ya ubaguzi wa vyama. Vyama vya Siasa vipo 23, vyama 22 vikawa ni vyama vya Upinzani, iweje leo wote ni wapinzani eti UKAWA iwe ya vyama vitatu vya upinzani fikiria kama ni uchaguzi Mkuu, vyama vitatu kugombea uchaguzi haisaidii maana hata robo haijafika. Ubaguzi uliofanywa na hawa jamaa hauvumiliki kabisa na si vitendo bali ni Umoja ndani ya Mtengano. Wakiweza kuungana vyote vyama 22 vikawa UKAWA basi nitakuwa tayari kuendelea na siasa na hata Serikali 3 nitaunga mkono lakini dhambi ya kubaguana ya vyama itaendelea basi ni heri Serikali 2 au 1 maana UKAWA ni ya vyama vitatu na si ya wananchi maana ya UKAWA ya wananchi ni ya vyama vyote 22 vya Upinzani dhambi ya ubaguzi iacheni ni Pepo mchafu.

6:0 FIKRA MBADALA
Vijana wenzangu tuache mihemko na jaziba katika ushabiki wa mambo ya kisiasa na tuhamie katika uzalendo wa kujenga nchi yeye Amani na Uzalendo bila kujali itikadi za vyama vyetu na tusijikite kuchagua vyama bali tuchague viongozi wanaotufaa bila kujali Ushabiki wa vyama.

7:0 MAPUMZIKO
Kwa sasa nimeamua kupumzika siasa na kuangalia mstakabli wa maisha ya kifamilia kwanza, pamoja na kupumzika huko nitapumzika na kwamba nitakuwa naelekea chama gani hilo si swala la leo mpaka pale nitakapooona inafaa na sijui ni lini.

Ndugu wanahabari nifikishieni taarifa hii kwa umma wa Watanzania na Mungu atupe uzima wa maisha marefu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.

MWL. DEOGRATIUS KISANDU
ALIYEKUWA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU TAIFA NCCR – MAGEUZI 17 / 06 / 2014
Inatuhusu nini sisi wewe kujivua uanachama?
 
Njaa ndo inakusumbua wewe! kama umeshindwa kazi si unavua tu kamba, mbwembwe za nini? UKAWA is the collision of the willing. Kwa hiyo unataka na Mrema ambaye katakata yupo CCM avutwe kwa nguvu kwenda UKAWA bila kuona umuhimu wake. Wewe nenda huko ulikoahidiwa buku saba saba.
 
Back
Top Bottom