Deo Filikunjombe: Tanzania sio mali ya CCM

Ingekuwa vyama ni Club za mpira wa soka......CHADEMA wangewapa CCM mchezaji wao ZZK na nyongeza ya mchezaji mwingine (SHIBUDA).....ili kumsajili DEO FILIKUNJOMBE.
 
Filiph alinifurahisha kwa presentation yake na nilishangazwa na kusikitishwa sana na mtizamo wa watu wachache wa ccm wenye lengo la kupendekeza kupitia katiba ijayo ili kuzingatia mambo ya umri kama alivyosikika makamba akipendekeza,sikudhania kabisa kama angeweza kuwa na mawazo feck kihivyo kwani kamwe umri hautakuwa hoja ya msingi kwenye kuleta au kutokuleta maendeleo kwa taifa lolote duniani,sifa ya kuwa kiongozi kamwe haiwezi kuangaliwa kwa mambo ya umri na hapa nimepoteza imani na makamba kabisaaaaaa, kwa sababu wanatuelekeza na kwenye kabila na udini ukanda nk.
 
anajitahidi kuishi katika ukweli na ukweli unamfamya mtu angare kama mwanga, hivyo naye anangara kama mwanga
 
CCM wanaamini bila CCM Tanzania haipo lakini CCM wanaitegemea zaidi Tanzania kuliko Tanzania inavyo itegemea CCM
 
Hivi punde katika Kongamano ya miaka 51 baada ya uhuru, mwasiasa machachari na mbuge wa Ludewa Mh. Deo Filikunjombe ametoboa ukweli kuwa kuna kasumba na dhana potofu miongoni mwa watanzania wakidhani kuwa nchi hii (Tanzania) ni mali ya CCM. Hii nchi si mali ya CCM bali ya watanzania. Nimeipenda sana hiyo. Nape unayedhani kuwa hii nchi ni mali ya CCM umepotea, pata hiyo shule.
Zamani watu waliamini dunia ni kama meza na ukingoni ndo unakuta maji, aliyekuja kupinga alichinjwa na utawala wa warumi. Huyu jamaa atakutana na wakati mgumu sana lakini mawazo yake yanaweza likomboa taifa la tanganyika kama mandela alivyoikomboa south afrika. Deo_tupo nyuma yako
 
"Pamoja na rasilimali nyingi tulizonazo, Inasikitisha mno kuona kuwa tumefika mahali sasa ambapo wanafunzi wanaofaulu darasa la saba kwenda kidato cha kwanza wamekuwa hawajui kusoma na kuandika. Nyote mtakuwa mashahidi hapa kwamba mwaka jana zaidi ya wanafunzi 9,000 walifaulu kwenda kidato cha kwanza wakiwa hawajui kusoma na kuandika.

Sasa kama hawa waliofaulu hawajui kusoma na kuandika, je waliofeli watakuwaje?" - alisema Filikunjombe.
 
Hivi punde katika Kongamano ya miaka 51 baada ya uhuru, mwasiasa machachari na mbuge wa Ludewa Mh. Deo Filikunjombe ametoboa ukweli kuwa kuna kasumba na dhana potofu miongoni mwa watanzania wakidhani kuwa nchi hii (Tanzania) ni mali ya CCM. Hii nchi si mali ya CCM bali ya watanzania. Nimeipenda sana hiyo. Nape unayedhani kuwa hii nchi ni mali ya CCM umepotea, pata hiyo shule.

huyu ni mzalendo tunahitaji wabunge wazalendo awe wa ccm bali uzalendo kwa nchi yetu
 
Huyu bwana mdogo namkubali sana. He is a member of parliament of his kind from ccm. What spoils his integrity is the fact that he is a member of chama cha majambazi.
 
"Inasikitisha kuona kuwa wakati hatuna fedha kwaajili ya kuwaongezea mishahara walimu (sm msingi, sekondari, walimu wa vyuo vikuu) na madaktari, serikali imekuwa ikitumia zaidi ya tshs. bil 70 kwa mwaka kama mishahara kwa wafanyakazi hewa.

Taarifa ya serikali kwa Bunge Agosti 7, mwaka 2012 inaonyesha kuwa uhakiki ulifanywa na serikali mwezi Januari mwaka huu kwenye halmashauri 133 na kwenye taasisi na wakala za serikali 154 ulibaini majina 9,949 ya watumishi wasiostahili kuwemo mkwenye orodha ya mishahara ambao wamekuwa wakilipwa mabilioni hayo kwa kila mwezi," - alisema Filikunjombe.
 
"Pamoja na rasilimali tele tulizo nazo, Inasikitisha mno kuona kuwa leo hii Tanzania ipo katika kapu moja la nchi maskini sana duniani, tukiwa pamoja na Somalia, Cambodia, na Afghanistan," - Filikunjombe
 
Kiukweli Filikunjombe ni engine ya jet. CCM mkatae mkubali Filikunjombe ni jembe ulaya. NI MUWAZI, MKWELI, MTIIFU NA MTU WA WATU, Hivyo mkimtema Ludewa tutamrudisha tena bungeni kwa shangwe kupitia chama kingine HONGERA SANA FILIKUNJOMBE
 
"Pamoja na rasilimali nyingi tulizonazo, Inasikitisha sana kuona leo hii mgonjwa akienda Hospitali ya Muhimbili, inabidi aende na shuka lake mkononi la kulalia. Kwa ujumla, hali katika hospitali zetu ni mbaya sana.

Inasikitisha sana, kuona kwamba kwa magonjwa madogo madogo kabisa, viongozi wetu sasa hivi wanaenda India na ulaya kwa matibabu.

Badala ya kuimarisha huduma ya matibabu kwa wote tumezidi kutengeneza matabaka. Tabaka chovu la kutibiwa hapa hapa bongo na tabaka ‘teule’ la kutibiwa nje. Muhimbili hospitali sasa hivi imegeuka kuwa uwanja wa ndege - kwenda India," - alisema Filikunjombe.
 
Hakika kuna watu wachache sana wanafahamu uwajibikaji katika uongozi wao and one of them ni Deo nimepitia kwa umakini mkubwa sana maneno yako na nimerudia zaidi ya mara tano hakika ningependa kuona mwenyekiti wa ccm na wengine walio na ufahamu potofu kama Nape na wengine kusoma tena na tena kwenye hizi line tatu


  1. Umaskini wetu unatokana na viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kuongoza nchi hii kuwa wabinafsi.
  2. Watawala waondokane na dhana potovu kuwa Tanzania ni mali ya CCM, bali wasaidie kuelewa kuwa Tanzania ni mali ya watanzania kwa sasa CCM ndiyo inayoongoza.
  3. Kuna watendaji wa serikali wamevaa miwani ya mbao hawasikii, hawaelewi na wanawaangusha watanzania.
Deo brother hakina mzazi wako ana paswa kupewa sifa za pekee kwa kukupeleka shule, kwani alikuwa amepeleka mtu sahihi kwenye taifa hili ambalo watawala wa chama chako wanahisi kuwa ni mali za familia zao na sisi wenye mali ni kama watumwa wao.
 
filikunjombi baba njoo cdm achana na machichidodo na uchichidodo:sleepy:
Huyu anavyo jiamini akija huko kwenu hamalizi miezi mitatu,lazima atafukuzwa kwenye chama. Si ndio style yenu mpya,ukimpinga Slaa basi lazima ufukuzwe CDM.
 
JM kilaza namba moja. Mzee Butiku busara tele. Makamanda Esther Wasira, Deo Filikunjombe, Majjid Mjengwa wamechana ile mbaya waki-reflect kizazi bora kijacho kwa uongozi wa taifa letu na sio wale mapacha wapumbavu waliokazania rais ajaye lazima awe post-1961. Tunahitaji kusikia tutavukaje hapa tulipo kama taifa na sio umri wa rais ajaye uweje!

Yani huyu Januari Makamba nimemtoa akilini, ameongea utumbo mtupu, non sense. Amtafute Zzk amweleze. How can you put 1961 to be deciding factor ya rais ajae?
 
Tanzania ni mali ya wakulima,wafanyakazi na wafanyabiashara.Je kwenye vyama vyetu ni kundi lipi limezidi?
- Nini faida na hasara zake iwapo
  1. Wakulima wakazidi kwenye chama?
  2. Wafanyakazi wakazidi kwenye chama?
  3. Wafanyabiashara wakazidi kwenye chama?
Tanzania inaonekana kama ni mali ya CCM kutokana na makundi matatu hapo juu kuonekana kushamili ilihali vyama vingine kuonekana kama kuelemea zaidi kundi moja zaidi hasa lile la sekta binafsi na asasi zisizo za kiserikali (wanaharakati).Ndio maana kwa kuelekea uchaguzi mkuu 2015 kumekuwa na operation nyingi miongoni mwa vyama vikuu vya siasa ama kutumia asasi hizo ama operation zao ili kuweza kupata ushawishi wa kundi kubwa la wakulima huku wakifahamu kuwa kundi la wafanyakazi ni kundi ambalo ni ushawishi wako ni mdogo ama usioleweka.
Zipo dhana nyingi si hii tu,mfano watumishi wa umma kutojihusisha na siasa,lakini ni lazima wawajibike kwa wanasiasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom