Denti wa chuo kikuu atekwa, na kuwawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Denti wa chuo kikuu atekwa, na kuwawa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gumzo, Jul 24, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu Cha Usimamizi wa Fedha, (IFM) jijini Dar es Salaam, Agnes B. King’unza (pichani), amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuokotwa akiwa hajitambui katika ufukwe wa Bahari ya Hindi jirani na Coco Beach.
  Habari za kipolisi zinasema Agnes alitekwa kisha akaokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali anatajwa kuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Coco Beach, ambako ndiko alikokutwa akiwa hajitambui.
  “Polisi na hata watu wengine wanahisi kuwa msichana huyo alitekwa kisha kutupwa na watu wasiofahamika, baada ya kufanyiwa ukatili wa kutisha kwa kunyweshwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni sumu,” kilisema chanzo chetu cha habari ndani ya jeshi la polisi.
  Habari zinasema baadaye mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akichukua shahada ya mambo ya kodi, alipelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay kisha askari hao wakamkimbiza Hospitali ya Agha Khan kwa matibabu.
  Hata hivyo, habari zinasema madaktari wa Agha Khan baada ya kuona hali ya mgonjwa ilikuwa mbaya, walimpa rufaa na kumpeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
  “Agnes alifariki jioni ya Julai 16, mwaka huu katika Hospitali ya Muhimbili na habari za kifo chake zilisababisha Chuo cha IFM kuzizima kwa wanafunzi kumlilia mwenzao,” kilisema chanzo hicho.
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema kwamba wasamaria wema walisema waliona Bajaj ikifika eneo alilotupwa Agnes wakadhani wanatupa mzigo.

  KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA
  GUMZO LA JIJI

   
 2. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Hivi IFM ni Chuo Kikuu?
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,468
  Trophy Points: 280
  uzembe wa kwanza
  mtu hajitambui wanampeleka polisi?
  halafu aga khan alikuwa na pesa au insuarance card?
  pengine walikataa kwa kuwa hawakuona uwezekano wa kulipwa
  tatu muhimbili inajulikana kwa uzembe
   
 4. j

  jeneneke JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 760
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Wahariri bwana wanafunzi wa IFM wamefunga walilia wapi?
   
 5. nziriye

  nziriye JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 960
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  hata mie nashangaa???,what i knw kuwa ifm ni chuo cha usimamizi wa fedha a.k.a institute of finance management.
   
 6. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Sasa hivi kila chuo kimekuwa chuo kikuu!
  Binti kama alitekwa kwa hila za watu roho yake ipumzike kwa amani
  Lakini kama ilikuwa ni tabia za wadada kuwachuna wakaka iwefundisho kwa wale wadada wanaopenda vya bure.
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,265
  Trophy Points: 280
  Wanafunzi wote wanakuwa wanalipa insurance money (nadhani laki moja hivi), so matibabu isingekuwa tatizo. Na aghakhan hawakatai emergencies, watafanya huduma ya kwanza na kupeleka mgonjwa safely to another hospital
   
 8. R

  Rubesha Kipesha Member

  #8
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kisa cha kusikitisha! Dunia imani imekwisha umebakia unyama!
  Mungu atunusuru.
   
 9. Nyanya mbichi

  Nyanya mbichi JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 3,218
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  baadhi ya vyuo vimepandishwa hadhi na kuwa vyuo vikuu vishiriki
  e.g I.F.M
  C.B.E
  D.I.T
  ustawi wa jamii e.t.c
   
 10. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #10
  Jul 24, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ni vyuo vikuu vishiriki vya chuo gani hapa Tanzania? unaelewa nini maana ya chuo kikuu kishiriki?
   
 11. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,061
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  habari hii niliiona michuzi wiki jana..inasikitisha kweli, binadamu tumezidi ukatili..Inahitaji uangalifu kweli!!
   
 12. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #12
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45

  Mkuu, hii taarifa uliyoleta inabidi uifafanue tuelewe.
  Awali ya yote nina mashaka kama unaelewa maana ya Chuo Kikuu Kishiriki!
  Ungetusaidia sana kama ungedokeza Vyuo tajwa hapo juu vimekuwa chini ya Vyuo Vikuu gani.
  Kwa kifupi,kwa kawaida,ili Chuo kiweze kuwa chuo Kkuu Kishiriki ni sharti chuo husika kiwe chini ya Chuo Kikuu fulani ambacho ni kamili.
  Kadiri ninavyojua,IFM ni moja ya Taasisi za Elimu ya Juu hapa nchini.
   
 13. L

  Lugeye JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 1,081
  Likes Received: 1,379
  Trophy Points: 280
  wanafunzi jaman hasa wa kike muwe na woga mnapotolewa out na mtu usiyemfahamu vizuri
   
 14. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,954
  Likes Received: 2,096
  Trophy Points: 280
  Labda wale wa supplementary exams au short courses!
   
 15. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,954
  Likes Received: 2,096
  Trophy Points: 280
  Sio woga tu bali kutumia mechanisms za male brain na kuacha tamaaaaaa!!
   
 16. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Haya matokeo ya utekeaji mbona ynapamba moto kwa kasi sana sasa hivi.

  Kuna umuhimu mkubwa wa wa mambo ya ndani kujipanga kwani awmeshindwa kazi.
  Haya mambo yamekuwa yakijirudia sana.
   
 17. G

  Ginner JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 1,139
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 180
  marehemu agnes hakutekwa.......
   
 18. C

  CAY JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Vimepandishwa kuwa vyuo vikuu vishiriki vya chuo gani?
   
 19. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Picha iko wapi sasa?Kama hakutekwa tupe za chi ni ya kapeti.
   
 20. Ndukidi

  Ndukidi JF-Expert Member

  #20
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 821
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Ginner
  Mbona unakanusha kuwa hakutekwa, je nini kilitokea? hebu funguka mkuu....
   
Loading...