Denti wa chuo kikuu atekwa, na kuwawa

Haya matokeo ya utekeaji mbona ynapamba moto kwa kasi sana sasa hivi.

Kuna umuhimu mkubwa wa wa mambo ya ndani kujipanga kwani awmeshindwa kazi.
Haya mambo yamekuwa yakijirudia sana.

Sina niambaya na huyo binti marehemu, ila mabinti wengine wajifunze kupunguza tamaa ya fedha na kutembea na matajiri ambao wengi wao hutoa kafara kulinda utajiri wao, sio kila kingaacho ni dhahabu, sio kila pesa ni halali..kuweni macho.
 
rest n peace,bibie nac tuko njiani either kwa ukimwi,ajali,malaria,madawa ya kulevya or kutegwa sumu
 
[h=3]DENTI CHUO KIKUU ATEKWA, NA KUUWAWA[/h]
Marehemu Agnes B. King'unza enzi za uhai wake.
Mwili wa Marehemu Agnes ukiwa kanisani kwa heshima za mwisho.
Mama mzazi wa Agnes akilia kwa uchungu baada ya kuona mwili wa mwanae.
Baba mzazi wa marehemu Agnes, Bwana Bernard King'unza (mwenye koti jeusi kulia).
Baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakisoma na marehemu katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu Cha Usimamizi wa Fedha, (IFM) jijini Dar es Salaam, Agnes B. King'unza (pichani), amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuokotwa akiwa hajitambui katika ufukwe wa Bahari ya Hindi jirani na Coco Beach.
Habari za kipolisi zinasema Agnes alitekwa kisha akaokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali anatajwa kuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Coco Beach, ambako ndiko alikokutwa akiwa hajitambui.
"Polisi na hata watu wengine wanahisi kuwa msichana huyo alitekwa kisha kutupwa na watu wasiofahamika, baada ya kufanyiwa ukatili wa kutisha kwa kunyweshwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni sumu," kilisema chanzo chetu cha habari ndani ya jeshi la polisi.
Habari zinasema baadaye mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akichukua shahada ya mambo ya kodi, alipelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay kisha askari hao wakamkimbiza Hospitali ya Agha Khan kwa matibabu.
Hata hivyo, habari zinasema madaktari wa Agha Khan baada ya kuona hali ya mgonjwa ilikuwa mbaya, walimpa rufaa na kumpeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
"Agnes alifariki jioni ya Julai 16, mwaka huu katika Hospitali ya Muhimbili na habari za kifo chake zilisababisha Chuo cha IFM kuzizima kwa wanafunzi kumlilia mwenzao," kilisema chanzo hicho.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema kwamba wasamaria wema walisema waliona Bajaj ikifika eneo alilotupwa Agnes wakadhani wanatupa mzigo.
"Walipokwenda kuangalia wakakuta ni mtu akiwa hoi hajitambui. Baada ya kupelekwa hospitali siku ya pili alikuja mama mdogo wa marehemu Agnes aitwaye Veronica Galus na akaleta taarifa kuwa binti yao huyo amefariki dunia. Polisi tunaendelea na uchunguzi kuwatafuta wahusika," alisema Kenyela. Hata hivyo, kifo hicho kimeacha maswali mengi kuwa binti huyo alilishwa nini na nani?
Mzazi wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Bernad King'unza mkazi wa Kimara Dar, hakupatikana kwa maelezo kwamba alikuwa safarini Iringa kwenye mazishi ya mpendwa wao huyo yaliyofanyika nyumbani kwao Kalenga, Iringa Julai 19, mwaka huu.


COMMENT%2BTAG.PNG
 
mnaoujua sababu za kifo chake isaidieni polisi ili wahaflifu hao wakamatwe.
 
naona hii info itawasaidia pia haiendani na hii habari.
Kindly note there is a new technique used by robbers and carjackers to escape from arrest due to their criminal activities. They are collecting used scratch cards and once they abandon the car or where they dump the dead bodies they leave the already used scratch card at the scene. Once the police arrive they are using the scratch card serial numbers to track on which phone number it was loaded then they start tracking the phone number owner. Already Two people are in Keko who fell victim of the trick. Kindly once you load airtime make sure you destroy the card before you dispose it to avoid such incidences. Share this information with your friends. **
 
Sina niambaya na huyo binti marehemu, ila mabinti wengine wajifunze kupunguza tamaa ya fedha na kutembea na matajiri ambao wengi wao hutoa kafara kulinda utajiri wao, sio kila kingaacho ni dhahabu, sio kila pesa ni halali..kuweni macho.

Usihukumu bila kujua chanzo au wewe unajua alikuwa na hao matajiri?
Vaa kiatu cha huyo binti na wazazi wake.

Ushauri wako ni mzuri lakini ni bora watanzania tukajifunza kutafuta vyanzo vya matatizo na si kugeneralize na kudhani.
Hili ni tatizo la nchi usalama wa raia uko matatani.
Chukulia ni binti yako au dada yako!
 
Usihukumu bila kujua chanzo au wewe unajua alikuwa na hao matajiri?
Vaa kiatu cha huyo binti na wazazi wake.

Ushauri wako ni mzuri lakini ni bora watanzania tukajifunza kutafuta vyanzo vya matatizo na si kugeneralize na kudhani.
Hili ni tatizo la nchi usalama wa raia uko matatani.
Chukulia ni binti yako au dada yako!

Ndio maana nikatanguliza kusema sihukumu, au hukuona?? haya wewe mwenye busara kuliko wote humu JF tuambie chanzo cha tatizo la huyu binti ni nini? sio kwa kuhisi with facts...
 
Ndio maana nikatanguliza kusema sihukumu, au hukuona?? haya wewe mwenye busara kuliko wote humu JF tuambie chanzo cha tatizo la huyu binti ni nini? sio kwa kuhisi with facts...

Hilo umeliona wewe, but facts mimi si mpelelezi tungoje upelelezi ukamilike then tuanze kutoa mawazo yetu.
 
Back
Top Bottom