Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 18,304
- 46,118
Hapa kilichodhahiri ni kuwa haijalishi kama Kapuya alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na huyu mwanamke au la, kilichodhahiri ni KUWA MWANAMKE HUYU NI TAPELI. Hilo linadhihirika kwa kuwa na majina mengi, kwa nini atumie majina tofauti kwa watu tofauti. Pili kitendo cha kumtapeli Salma mpaka kufikia kuwekwa ndani nao ni ushahidi tosha kuwa huyu mwanamke ni tapeli na ni mwizi. Na tatu, kwa nini adanganye umri wake? Amefanya hivyo makusudi ili kufanikisha malengo yake.
Fikra zangu zinanituma kuwa Kapuya aliwekewa mtego na huyu tapeli na kunaswa. Fundisho kwa Kapuya ni kuwa anastahili kuwa mwanagalifu katika nyenendo zake au kujitafakari maana mara nyingi binadamu hutegwa na kunaswa kwenye udhaifu wake. Lakini pia jamii ni lazima ikemee na kuchukua hatua kali dhidi ya mabinti tapeli kama huyu. Tusiendekeze na kushabikia utapeli wa kutumia usichana.