Waungwana,
Utawasikia hawa wahuni na vilaza na wimbo wao maarufu "Tanzania inakopesheka" na hivyo kuendelea kukopa toka ndani ya mabenki ya biashara nchini ambayo riba yake ni kubwa mno. Miaka miwili iliyopita deni la Taifa lilikuwa ni 20 Trillioni lakini hawa vilaza na wahuni waliojivisha ngozi ya uongozi wakaendelea na wimbo wao maarufu ambao haujali maslahi ya Tanzania na Watanzania wimbo wa "Tanzania inakopesheka" na hivyo kuendelea kuchukua mikopo mikubwa toka mabenki ya biashara. Hatima yake katika miaka miwili deni la Taifa limeongezeka karibu mara mbili toka trillion 20 mpaka Trilioni 39 na yule mkwer pale Ikulu yuko kimyaaaaa wala hati neon. Kama alivyosema kishajichokea anangoja miezi yake ikatike akatafune mabilioni yake aliyopewa na marafiki zake akina Ruge na wenzie.
Cha kustaajabisha waungwana pamoja na deni kuongezeka kwa kasi ya kutisha hakuna hatua zozote zinazochukuliwa ili kupambana na kasi ya ukuaji wa deni la Taifa. Bado kila mwaka Serikali inaruhusu misamaha ya kodi ya shilingi trilioni 1.5, bado kila mwaka matumizi yaliyojaa matanuzi makubwa ununuzi wa mashangingi chungu nzima, safari za nje za mkwere ambazo hazina tija kwa Taifa akiwa na kundi kubwa la maofisa wake badi zinaendelea karibu kila mwezi bila kujali kwamba hali ya nchi kifedha ni mbaya sana. Na wakati huo huo pamoja na hali ya kifedha nchini kuwa mbaya Wabunge, Mawaziri, Waziri Mkuu na Rais ambao wana mishahara mikubwa sana bado mishahara yao haitozwi kodi. Serikali ilikuja na utaratibu wa wenye nyadhifa za juu wauziwe magari ya Serikali ili kuipunguzia Serikali mzigo mkubwa wa kuyagharamia magari hayo kwa petroli, matengenezo na mishahara ya madreva, lakini baada ya kuuziana magari hayo wakaendelea na ununuzi wa magari ya kifahari yenye consumption kubwa sana ya petroli bila kujali mzigo kwa walipa kodi na yale waliyonunua kuyaweka majumbani mwao.
Pamoja na nchi yetu kujaliwa utajiri mkubwa sana wa rasilimali chungu nzima ikiwemo dhahabu, uranium, almasi, Tanzanet, gesi na nyingi nyinginezo hawa wahuni na vilaza wamesaini mikataba ambayo haina maslahi kwa nchi yetu na watu wake. Kama mtakumbuka Muhongo alivyogoma kata kata kuipeleka mikataba mbali mbali ya madini nchini ikajadiliwe na Wabunge lakini hakufanya hivyo. Huyu Waziri mpya wa Madini na Nishati naye sijaona dalili zozote kama ana mpango wa kuipeleka mikataba hii Bungeni ili Watanzania tuwezi kufahamu kulikoni pamoja na utajiri mkubwa wa rasilimali nchini na kuwakaribisha wageni wavune rasilimali hizo lakini karibu mwaka wa 20 sasa bado Watanzania hatujaona maslahi yoyote yaliyoletwa na utjiri wetu mkubwa. Mashule, Mahospitali yetu bado yana hali ya kusikitisha. Shule hazina madawati wala walimu, barabara zetu ziko chini ya viwango, ATC iko hohehahe, usafiri wetu wa majini bado ni wa hatari na wa kusikitisha sana, mahospitali hayana madawa wala vifaa muhimu hawa wenye nchi wakiugua hao kiguu na njia kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa pesa za walipa kodi na huku mahospitali yakizidi kuwa katika hali mbaya. Upatikanaji wa maji na umeme bado ni wa kusuasua miaka nenda miaka rudi lakini hakuna anayejali hata kidogo.
Wanachojali hawa wahuni na vilaza ni wao kubaki madarakani kwa nguvu zao zote hata kama kwa kutumia mtutu wa bunduki na huku nchi ikizidi kuangamia. Waliimba wimbo wao maarufu "Tanzania tunakopesheka" wakati deni la Taifa liko trilioni 10, wakaendelea na wimbo huo miaka miwili iliyopita wakati deni lilikuwa limeongezeka mara mbili na kufikia Trilioni 20 hatima yake ni kwamba sasa deni liko karibu kufikia trilioni 40 bado tu wanaendelea na nyimbo yao "Tanzania tunakopesheka" sijui tunalipa principal kiasi gani kwa mwezi/mwaka na riba tunalipa kiasi gani hawa wahuni na vilaza wanalificha hili makusudi ili waweze kuendelea kuimba wimbo wao "Tanzania tunakopesheka"
Haya Waungwana tuendelee nasi kuimba huu wimbo wa hawa wahuni na vilaza "Tanzania tunapokesheka" na labda miaka miwili mingine hili deni la Taifa litakuwa limefikia trilioni 80 labda hapo tutastuka na kubadili wimbo na kuanza kuimba "Tanzania hatukopesheki" wimbo ambao tulitakiwa tuuimbe miaka 20 iliyopita.
Muwe na weekend njema.