Deni la Taifa lafikia Tzs trilioni 61.8

Deni la Taifa lafikia Tzs trilioni 61.8

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,892
Kwa mujibu wa taarifa toka ITV, Deni la taifa laongezeka hadi kufikia shilingi trilioni sitini na moja nukta nane. Mwaka 2015 deni la taifa lilifikia Shilingi Trilioni 40

========

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imebaini kuwa deni la taifa limekua kukua kutoka shilingi trilioni hamsini na tatu nukta tatu mwaka 2017 hadi shilingi trilioni sitini na moja nukta nane mwaka 2018 kutokana na mahitaji ya uwekezaji kwenye miradi ya maendeleo na kijamii nchini kwa ajili ya kukuza uchumi.

Akizungumza bungeni jana wakati akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo katika kipindi cha nusu ya mwaka 2018/19, mwenyekiti wake, George Simbachawene alisema, “Kwa sasa Serikali imelazimika kujielekeza kukopa mikopo yenye masharti ya kibisahara (non concessional loans) kuliko yenye masharti nafuu (concessional) kama ilivyokuwa awali.

“Kamati inaona mikopo hiyo ina riba kubwa na hivyo kuwepo kwa mzigo mkubwa wa ugharamiaji wa mikopo kupitia mapato ya ndani.”

Simbachawene alisema hadi Novemba mwaka jana, Deni la Taifa lilikuwa Sh61.8 trilioni ambazo zimetokana na ukuaji wa deni hilo kwa taratibu kutokana na uwekezaji kwenye miradi ya maendeleo na kijamii nchini kwa ajili ya kukuza uchumi.

Alisema deni la Serikali linaendelea kukua likijumlisha fedha zilizokopwa kutoka vyanzo vya ndani na nje na sekta binafsi kwa ajili ya kugharamia miradi.

“Kamati inatambua kuwa Serikali hukopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kupata fedha za kigeni na kukopesha taasisi za ndani za umma kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimkakati,” alisema.

Mbunge huyo wa Kibakwe alisema kutokana na sababu nzuri za ukopaji ikiwamo uhimilivu wa deni, bado kamati yao inashauri Serikali iangalie uwiano uliopo kati ya mwenendo wa upatikanaji wa mapato ya ndani pamoja na ulipaji wa deni la Serikali na athari zake katika bajeti a uchumi.

Kamati hiyo ilishauri kuwa, umefika wakati Serikali ipange bajeti yake ya maendeleo kwa kutegemea mapato yake ya ndani na mikopo ya ndani ambayo upatikanaji wake ni wa uhakika.
Aliitaka Serikali kuhakikisha kuwa ukopaji wake katika vyanzo vya ndani hauathiri upatikanaji wa mikopo kwa sekta binafsi huku akiipongeza kwa kuendelea kufanyia kazi mapendekezo mbalimbali yanayotolewa na kamati hiyo.

Simbachawene alisema hadi Desemba mwaka jana, Serikali ilikuwa imekusanya Sh12.8 trilioni sawa na asilimia 80.4 ya lengo la kukusanya Sh15.974 trilioni na asilimia 32.5 ya lengo la mwaka ambapo zinatakiwa kukusanywa Sh32.475trilioni.

Alisema kodi ya ushuru wa forodha inaongoza kwa kukusanya Sh3.143 trilioni ikifuatiwa na walipa kodi wakubwa waliokusanya Sh2.980 trilioni wakifuatiwa na kodi za ndani Sh 1.594trilioni.

Alitaja sababu ya kutofikiwa kwa lengo la nusu mwaka kuwa ni kutokana na kutopokewa kwa misaada kwa wakati ambapo hadi kufikia Desemba mwaka jana, kiasi kilichokuwa kimepokewa na Serikali kutoka nchi wahisani ilikuwa ni Sh878.8 bilioni kati ya Sh 2.676 trilioni zilizoahidiwa.

Alisema kati ya Sh12.839 trilioni zilizokusanywa, Sh4.77trilioni sawa na asilimia 37.1 zilitumika kugharamia Deni la Taifa pamoja na riba ya madeni yaliyoiva ambapo Sh3.311 trilioni zilitumika kulipa mishahara na Sh4.749 trilioni ndizo zilizotumika kwa shughuli za maendeleo.

Alisema kwa mwendo huo, huenda Serikali ikashindwa kufikia malengo yake ya makusanyo kwani inaonyesha inaweza kufikia asilimia 80 hadi 95 na kupendekeza iongeze wigo wa ukusanyaji mapato ya ndani na kutafuta vyanzo vipya vya mapato.
 
Niliwahi sema huyu bwana atatuachia structures lakini tutabaki masikini wa kutupwa.

Kwa mujibu wa Zitto,ripoti ya Benki ya Dunia teyari imeonyesha ongezeko la watu masikini wapatao milioni 2 tangu huyu bwana achukue madaraka.

Tafsiri ya haya madeni ni serikali kutumia makusanyo ya ndani kuhudumia deni la Taifa na matokeo yake ni serikali kupunguza uwezo wa kuajiri,kununua madawa,kugharamia elimu,kutoa mikopo ya elimu ya juu,kupambana na umasikini,miradi ya maendeleo kuathirika kwa kukosa fedha za kutosha,serilali kushindwa kuongeza mishahara ya watumishi,kulipa madeni ya ndani,n.k.

Kwa kifupi, haya madeni ni janga kubwa sana kwa Taifa na yanachangia umasikini wa mtu mmoja mmoja kwa njia mbalimbali.

Na bahati mbaya sana,baadhi ya miradi tunayokopea fedha kuitekeleza inaweza kuja kugeuka kuwa ni white elephant projects na hivyo ikawa ni hasara juu ya hasara.
 
Mbona ni dogo sana ukilinganisha na miradi mikubwa inayoendelea kwa sasa hapa nchini. Angalau tufikie 100 Trillioni basi.
ko una kili ki namna flani kwamba pesa ya kuendesha hii miradi tumekopa na sio kama jiwe anavyo jitapa eti pesa za ndani.

kwamba unampinga mwenyekiti kwamba sio dona katri bali anakopa kinyemela (kama zzk alivyo wahi sema)

sisimu bwana mnafurahisha sana, mkuu akisema ni pesa za ndani mnakenua ikionekana deni limepanda jibu ndo kama ilo lako.

bro una akili ndogo hadi nimeogopa kama kuna watu dizaini iyo.
 
Mbona ni dogo sana ukilinganisha na miradi mikubwa inayoendelea kwa sasa hapa nchini. Angalau tufikie 100 Trillioni basi.

Tukisema rais wetu ni muongo wa kipaji mnapanic ile mbaya. Deni linatoka wapi wakati kila siku hadithi ni kwamba tunatumia fedha zetu za ndani? Tukisema huwa kiwango cha makusanyo ni cha kupika huwa mnalialia nini? Magu ataliachia taifa hili deni ambalo halilipiki kwa ajili ya political milage.
 
ko una kili ki namna flani kwamba pesa ya kuendesha hii miradi tumekopa na sio kama jiwe anavyo jitapa eti pesa za ndani.

kwamba unampinga mwenyekiti kwamba sio dona katri bali anakopa kinyemela (kama zzk alivyo wahi sema)

sisimu bwana mnafurahisha sana, mkuu akisema ni pesa za ndani mnakenua ikionekana deni limepanda jibu ndo kama ilo lako.

bro una akili ndogo hadi nimeogopa kama kuna watu dizaini iyo.

Nani atalilipa hilo deni, kwa fedha ya ndani au ya nje? Kama ni fedha ya ndani ni ya kina nani kama si yetu wenyewe wa Tanzania.
 
Tukisema rais wetu ni muongo wa kipaji mnapanic ile mbaya. Deni linatoka wapi wakati kila siku hadithi ni kwamba tunatumia fedha zetu za ndani? Tukisema huwa kiwango cha makusanyo ni cha kupika huwa mnalialia nini? Magu ataliachia taifa hili deni ambalo halilipiki kwa ajili ya political milage.

Ili Rais atakaye kuja baada ya yeye ajue anakazi ya kufanya. Hatutaki nchi hii iwe tena na Rais mwenye mentality ya kwenda kupiga picha na macelebreties wa ulaya ama kubembea ama kwanda kushangaa uwanja wa Real Madrid yaani mkuu wa nchi limbukeni. Atakaye taka Urais ajue ana kazi seriously za kulifanyia taifa ikiwemo kulipa deni la maana hasa.

Ulimbukeni wa kazi na bata ndio waliorithishwa na walio danganywa wakadanganyika, ati ni presidential materials, mawee!!
 
Ili Rais atakaye kuja basda ya yeye ajue anakazi ya kufanya. Hatutaki nchi hii iwe tena na Rais mwenye mentality ya kwenda kupiga picha na macelebreties wa ulaya ama kubembea ama kwanda kushangaa uwanja wa Real Madrid yaani mkuu wa nchi limbukeni. Atakaye taka Urais ajue ana kazi seriously za kulifanyia taifa ikiwemo kulipa deni la maana hasa.

So anakopa harusi anamuachia matanga ajaye? Hili la kukopa ni nani anashindwa? Zile kelele za kwamba ni pesa za ndani huwa anazitoa wapi?
 
Niliwahi sema huyu bwana atatuachia structures lakini tutabaki masikini wa kutupwa.

Kwa mujibu wa Zitto,ripoti ya Benki ya Dunia teyari imeonyesha ongezeko la watu masikini wapatao milioni 2 tangu huyu bwana achukue madaraka.

Tafsiri ya haya madeni ni serikali kutumia makusanyo ya ndani kuhudumia deni la Taifa na matokeo yake ni serikali kupunguza uwezo wa kuajiri,kununua madawa,kugharamia elimu,kutoa mikopo ya elimu ya juu,kupambana na umasikini,miradi ya maendeleo kuathirika kwa kukosa fedha za kutosha,serilali kushindwa kuongeza mishahara ya watumishi,kulipa madeni ya ndani,n.k.

Kwa kifupi, haya madeni ni janga kubwa sana kwa Taifa na yanachangia umasikini wa mtu mmoja mmoja kwa njia mbalimbali.

Na bahati mbaya sana,baadhi ya miradi tunayokopea fedha kuitekeleza ni white elephant projects kwahiyo ni hasara juu ya hasara.
Kwani hizo pesa ametumia magufuli na familia yake. ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Itafaa kama patakuja baadae kiongozi atakayetaifisha mali zote za watawala waliotuingiza kwenye madeni kwa sababu tu ya wao kutaka madaraka huku wakilipwa mamilioni ya fedha. Wakati huo huo wengi wakitamani kunufaika na kupata heshma kubwa kwa kustaafu kwa heshma kubwa huku wakiwaachia deni kubwa wananchi maskini huku wao wakiishi maisha ya peponi hata baada ya kustaafu.

Ifikie mahali mali za wakubwa waliolisbabishia taifa letu madeni zimulikwe mana miradi mingi inalenga kujinufaisha ama kisiasa au kupitia tenda wanazojipa kindugu na kirafiki. Hivyo hakuna anayejali mana deni la nchi halimpunguzii mnufaika chochote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom