Deni hili ni pigo kubwa kwa wananchi

VISIONEER

Senior Member
Apr 29, 2011
141
20
TANZANIA TUNA PIGO KUBWA LA DENI LINALOTUKABILI AMBALO LINAONGEZEKA KWA KASI KUBWA SANA.
DENI HILI LA TRILIONI 10.5 NI PIGO KUBWA KWA SERIKALI NA WANANCHI KWASABABU WANANCHI NDIO WALIPA KODI.

KIKUBWA KINACHOHUZUNISHA NI KUONGEZEKA KWA MADENI KWA SPEED KALI KWA ASILIMIA 38, 2009/2010. NA MBAYA ZAIDI KWA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA TU DENI LA TAIFA LIMEONGEZEKA TZSHS TRILIONI 2.5.
SASA NINACHOJIULIZA KWA MIAKA 4 IJAYO ITAKUWAJE KWA MWENDO HUU.
RAIS ATAKAYEFUATA KAZI ANAYO.

SOURCE:MWANANCHI.
Kwanini nchi imezidiwa na madeni kiasi hiki?

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh

NI jambo la fedheha na aibu isiyo kifani kwa Watanzania kwamba nchi yetu imeendelea kulemewa na madeni kiasi kwamba sasa hata vizazi vyetu vijavyo pia vitapaswa kulipa madeni hayo. Ni maisha ya kero na aibu kwamba familia nzima, yaani baba, mama, watoto na wajukuu kila mmoja anajikuta akiishi na mzigo wa madeni makubwa ambayo anatakiwa awalipe wadai wake.

Lakini maisha hayo ya udhalilishwaji yanazidishwa na kutiwa uchungu na ukweli kwamba madeni hayo ya familia hiyo yalikopwa na baba aliyedai anafanya hivyo kwa niaba ya familia, ingawa familia hiyo haikuhusishwa wala kutaarifiwa kwa namna yoyote katika suala hilo. Baya zaidi ni pale baba alipokopa fedha hizo na kuzitumia kufuatana na matakwa yake binafsi.

Ni katika muktadha huo, mzigo wa deni la taifa ambao umefikia zaidi ya Sh 10.5 trilioni na unaoendelea kuwaelemea Watanzania unapaswa kuangaliwa. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema katika ripoti yake ya mwaka wa fedha wa 2009/2010 kuwa deni la taifa katika kipindi hicho liliongezeka kwa asilimia 38 kutoka Sh7.6 bilioni hadi Sh10.5 trilioni.

Hizi ni habari za kushtusha sana kwani kuongezeka kwa deni hilo ni pigo kubwa kwa wananchi kwa kuwa ndio walipaji wakubwa wa kodi mbalimbali licha ya wengi wao kuwa fukara. Ripoti hiyo ya CAG inazidi kuibua maswali kuliko majibu inaposema kuwa, katika kipindi cha mwaka mmoja tu, deni la taifa limeongezeka kwa Sh2.8 trilioni.

Hali hiyo haitoi matumaini kwa ustawi wa taifa letu, kwa maana ya Serikali kujenga uchumi imara kwa kuhakikisha kuwa nchi yetu haitumii kuliko kile inachopata. Ndio maana tunataharuki ripoti hiyo ya CAG inaposema pia kuwa, katika kipindi hicho, Serikali iliongeza deni la nje kwa zaidi ya Sh2.5 trilioni, sawa na asilimia 44, huku deni la ndani likiongezeka kwa zaidi ya Sh521.2 bilioni, sawa na asilimia 23.

Tafsiri ya moja kwa moja ya hali hiyo ni kwamba, pamoja na Serikali kusheheni wataalamu wa uchumi wanaoishauri, ilikopa kiasi kikubwa cha fedha kutoka katika taasisi mbalimbali za nje kuliko kiasi cha fedha kilichokopwa kutoka katika taasisi zetu hapa nchini. Kama CAG alivyosema katika ripoti hiyo, hii ina maana kuwa Serikali italazimika kuwalipa wadai wake walioko nje na hii kiuchumi ina maana kuwa kiasi kikubwa cha mtaji katika fedha za kigeni kitalipwa nje ya nchi.

Tunaungana na CAG kuishauri Serikali kwamba kwa kuwa uchumi wa nchi yetu umekua kwa asilimia 6.5 tu katika kipindi hicho, ni hatari kwa Serikali kuendelea kukopa pasipo kutilia maanani ukuaji wa hali ya uchumi wetu hasa kwa kutilia maanani kwamba CAG aligundua deni lisilotarajiwa ambapo wizara tisa na mikoa mitatu ilikopa Sh26 bilioni pasipo kuchukuliwa hatua. Madeni yasiyotarajiwa kama hayo ni mzigo kwa Serikali hasa pale yanapoiva na kutakiwa kulipwa.

Lakini jambo la kushangaza ni kuwa, wakati deni la taifa likizidi kukua kwa kiwango tulichotaja hapo juu, ripoti ya CAG inabaininisha kuwapo kwa mikopo isiyorejeshwa ya Sh424 bilioni katika kipindi hicho, ikiwa ni ongezeko la Sh7.6 bilioni, sawa na asilimia mbili kulinganisha na kipindi kilichotangulia cha mwaka 2008/9. Hii ni ishara mbaya kwa uchumi wetu, hasa ripoti ya CAG inaposisitiza kuwa madeni yamekaa bila kulipwa kwa kipindi cha miaka mitatu.

Sisi tunasema kuwa Serikali iuchukulie ushauri wa CAG kwa umuhimu mkubwa. Tunapendekeza kuwa mtindo wa kukopa pasipo kuzingatia vipaumbele vya taifa letu kiuchumi ukome na ubuniwe mchakato ambao utailazimisha Serikali kupitia kabla ya kutafuta mikopo kwa wafadhili na taasisi za fedha. Serikali isome alama za nyakati na kutambua kuwa wakati wa kukopa fedha na kuitumia itakavyo umepita.
 
Tunadanganyagwa misaada kumbe mikopo, sasa sijui watalipaje, hofu kwa wafanyakazi walipa kodi


kwa mtaji huu umaskini hautaisha tanzania, kweli rais unayefuata kazi unayo kuclear madeni kwanza maana mi navyojua madeni huleta umasikini.
 
Huu ni ufisadi mwingine, wataanza kulipa madeni ambayo pengine hata pesa au bidhaa hazikuletwa nchini... watch this space!
 
Back
Top Bottom