Demokrasia ya Tanzania na mauaji ya raia

Dopas

JF-Expert Member
Aug 14, 2010
1,151
392
WanaJF
Uchaguzi wa Igunga unaendelea kuleta machungu.
Uchaguzi umeisha ingawa hatuna hakika kama ulikuwa huru na haki, kwani hadi sasa hakuna aliyelalamikia kwa hoja pale ambapo kura hazikutosha. Zaidi tunasikia tambo za kupita kiasi za ccm ambao kura zilitosha, kulingana na tume ya uchaguzi. Tambo ambazo zinatufanya tufikiri mara mbili, huenda sio za halali? Huenda kuna hila zilifanyika? Kwanini kuzunguka Tz nzima kusherekea ushindi wa Igunga, jimbo moja tu ya Tanzania? Tuyaache haya, muda utatuambia mengi.
Lakini kilichonisukuma kuandika machache ni machungu yaliyoletwa na uchaguzi huo.
Kwanza tunafahamu jinsi kampeni za Igunga zilivyoendeshwa kwa matisho makubwa. Hasa kutoka CCM na vyombo vya dola. Lakini pamoja na yote hayo nadhani hakuna aliyetegemea baada ya uchaguzi huu kungekuwa na watanzania waliopoteza maisha yao.
Cha ajabu hadi jana tumesikia taarifa kuwa maiti watatu wamepatikana waliosadikiwa walikuwa wafuasi wa CDM. Haidhuru wangekuwa wafuasi wa chama gani, walikuwa raia wema wa Tanzania.
Swali langu ni wauaji hawa wametoka nchi gani? Kweli ni watanzania? Inafikia hatua mtanzania anamuua mwenzake kwa ajili ya uchaguzi wa mbunge au hata rais?
Tulishuhudia mauaji ya Arusha iliyofanywa na polisi, japo ilituuma lakini hatukushangaa sana kwani polisi wa Tanzania wamezoea kuua, tumesikia mara nyingi North Mara wakiua watanzania kwaajili ya maslahi ya makaburu, tumesikia mara kwa mara wakiwaua raia wema, wasio hata na silaha, kwa visingizio mbalimbali. Hatushangai, labda kwa sababu hawana mahali pa kufanyia mazoezi ya mauaji. Walau hili la Igunga labda sio wao, labda ni vijana waliowekwa kambi huko singida kwa mwezi moja. Lakini ni watanzania kweli hao? Je tunakoelekea ni sawa, hatujapotea kweli mwelekeo? Ndiyo namna kuwapata viongozi kwa njia ya demokrasia?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom