Demokrasia ya ccm ni ya mashaka. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Demokrasia ya ccm ni ya mashaka.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by enzihuru, Aug 24, 2012.

 1. e

  enzihuru Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku za karibu mheshimiwa Nape alisema CCM hawana utaratibu wa mtu kuomba kugombea nafasi ya mwenykiti ngazi ya taifa bali kamati kuu humpendekeza.Kamati hii huteuliwa na mwenyekiti wa chama taifa,kama ilivyofanywa hivi karibuni wakati wa porojo za kujivua gamba.Kwangu. Hii ni hadithi ya kuku kutaga yai ili yai litoe kuku; kulipana fadhila tuu.Matokeo yake chama kinakuwa cha koo za Mnauye, Kawawa,Mwinyi,Malecela,Kikwete na walewale wengine wachache ambao majina yao tunaweza hata kuyaota kwa vile yalivyozoeleka.
  Ni wakati sasa kuondoa mfumo huu wa demokrasia ya hofu kwa kuruhusu kila mtu anayeona kuwa anaweza, agombee na wanachama wapewe kazi ya kuamua nani anafaa.Tusiteuane kulinda maslahi ya watu fulani tu bali tupanue demokrasia yetu kwa manufaa ya chama, hasa wakati huu ambapo wapinzani kama Chadema, wanakuja na mikakati imara ya ushindi kila leo, wakiwa wameshikamana vilivyo.Ndio maana hata propaganda za udini na ukabila dhidi ya chadema hazifui dafu kwani ndani ya CCm kuna element hizo ambazo waliofanikiwa kuziepuka ni Sokoine na Nyerere tu.
  Mwenye mdomo, aseme na mwenye ufahamu na atafakari haya.
   
 2. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  ya magamba tuwachie magamba yenyewe!
   
Loading...