Demokrasia katika nchi masikini ni umasikini

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,018
Reaction score
20,489
Kifalsafa zaidi Afrika haiwezi kuishi maisha yaliyoishi Ulaya na Amerika, Nchi zote zilizoendelea zilipita kwenye mikono ya kiimla na kidikteta japokuwa nyakati ziliruhusu kuwa hivyo,

Njia hizo haziwezi na hazitotokea kuisaidia Afrika, Afrika lazima ichague utaratibu wake wa kufikia malengo iyatakayo na siyo njia hii tuiendeayo ambayo ni njia waliyopita Ulaya na Amerika karne ya 18-19, Nyakati za leo zinakataa. Wapo wanaoitazama dunia kuwa inaongwa kidkteta hasa Uchina, Korea Kaskazini, Korea Kusini, Urusi nk... Lakini hawafahamu kuwa ule sio udikta ni utawala wa sheria na katiba uliojengwa katika misingi ya karne ya 18-19 ambpo dunia ilikuwa chini ya mkono wa chuma. Leo ule SIO UDIKTETA.

Udikteta upo wa aina moja tu, ni utawala usiofuata katiba na sheria, utawala wa mtu mmoja tu, utawala wa matamko (decree), na madikteta wapo wa aina mbili, ambao ni Dikteta msomi, na dikteta mpuumbavu... Hawa hutofautiana katika staili zao za kutawala, Dikteta msomi hutawala huku watu wake wakilia machozi moyoni na usoni wakicheka, huku dikteta mpuumbavu, hutawala huku watu wake wakilia machozi machoni huku moyoni wakikenua meno... Uchaguzi ni wako.

Udikteta wowote hata ule unaopambwa na wajasiliasiasa kuwa ni udikteta mamboleo kamwe haujawahi kuiendesha dunia ya leo, labla kwenye nchi ya Nodi. Hakuna udikteta mamboleo duniani, hilo ni ingizo jipya katika uhalifu wa kisiasa wa wanasiasa wanaotumia vibaya kiuongo chao kiitwacho tumbo.. Tumbo ukiliruhusu likutawale litakufanya hata uwe Prof utafanya mambo kama Prof Lipumba au hata uwe Dr utafanya mambo kama Dr Rutengwe.

Demokrasia ya ulaya katika nchi masikini ni umasikini.
 
......kama hakuna udikteta mamboleo kuna nini?????
 
Yerico unaongelea udikteta upi?
Toa boriti kwanza kwenye jicho lako
Chadema wameondoa kinyemela kipengele cha ukomo wa uongozi,yaani Mbowe ni mwenyekiti hadi siku ya kiama
Chadema huruhusiwi kwenda mahakamani,ukienda tu umejifukuzisha!!!hii haki ya msingi imepokwa Mbona hatumuoni Yerico na genge la wasanii wenzie kupiga kelele?
Bavicha msifanye watu wote ni wajinga kama wafuasi wenu
 
Chama cha siasa ni kama msikiti au kanisa, ukiona mafundisho haya hayakufai unahamia kwingine.... Nchi huwezi kuhama unapambana mpaka tone la mwisho
 
Huwezi kupambana bila ya itikadi,na itikadi inapatikana kwenye chama cha siasa
Chadema mmepoteza ajenda rasmi ya kuwasimamia watanzania,sasa mnatapatapa kama askari arushae risasi hovyo,kila siku mnakuja na matamko na mipango koko
 
Mkuu hivi unakifahamu unachokiongea? Itikadi unaifahamu kweli?
 
......kama hakuna udikteta mamboleo kuna nini?????

Mada ya Yericko inajieleza kikamilifu, isome kwa umakini. Hakuba udikteta mamboleo. Kuna utawala wa sheria na Katiba.

Wanasiasa uchwara, kwa kuwa hawataki kutii sheria na kuheshimu Katiba ya nchi, hata Katiba za vyama vyao, ndio hao wanataka jamii ielewe kuna udikteta. Mifano ya wao kutokuheshimu Katiba za vyama vyao, iko mingi tu. Mfano ni ule wa kumteua mgombea wa Urais nje ya Katiba za vyama vyao. Walifanya hivyo, kwa kuwa ni wanasiasa wachumia matumbo.
 
Kutokana na umaskini katika nchi maskini hususan za Africa, hata watu wake wengi (sio wote) mawazo yao ni maskini pia, hayana afya!! Ukifuata demokrasia ya wengi wape, hawa watakupoteza, hapo sio kwa makusudi, ni kwa kuwa na uelewa mdogo, nn kifanyike? Ni lazima tuchague aina ya udikteta, kudikteti mawazo yao yasio na afya, japo wameyatoa kwa nia njm!! Kwa lugha rahisi demokrasia kwa watu maskini wa akili ni janga!!
 
kwa maana udikteta upo,sasa mbona unaandika hakuna???
 
Mada ya Yericko inajieleza kikamilifu, isome kwa umakini. Hakuba udikteta mamboleo. Kuna utawala wa sheria na Katiba.

Wanasiasa uchwara, kwa kuwa hawataki kutii sheria na kuheshimu Katiba ya nchi, hata Katiba za vyama vyao, ndio hao wanataka jamii ielewe kuna udikteta. Mifano ya wao kutokuheshimu Katiba za vyama vyao, iko mingi tu. Mfano ni ule wa kumteua mgombea wa Urais nje ya Katiba za vyama vyao. Walifanya hivyo, kwa kuwa ni wanasiasa wachumia matumbo.
Unapotosha nilichoandika na unanilisha maneno mdomoni...

Soma kilichoandikwa hakihusu Tanzania kinahusu Afrika...
 
Hahaha umeongea kifalsafa sana mkuu
Kutokana na umaskini katika nchi maskini hususan za Africa, hata watu wake wengi (sio wote) mawazo yao ni maskini pia, hayana afya!! Ukifuata demokrasia ya wengi wape, hawa watakupoteza, hapo sio kwa makusudi, ni kwa kuwa na uelewa mdogo, nn kifanyike? Ni lazima tuchague aina ya udikteta, kudikteti mawazo yao yasio na afya, japo wameyatoa kwa nia njm!! Kwa lugha rahisi demokrasia kwa watu maskini wa akili ni janga!!
 
Kifalsafa zaidi Afrika haiwezi kuishi maisha yaliyoishi Ulaya na Amerika, Nchi zote zilizoendelea zilipita kwenye mikono ya kiimla na kidikteta japokuwa nyakati ziliruhusu kuwa hivyo,

Njia hizo haziwezi na hazitotokea kuisaidia Afrika, Afrika lazima ichague utaratibu wake wa kufikia malengo iyatakayo na siyo njia hii tuiendeayo ambayo ni njia waliyopita Ulaya na Amerika karne ya 18-19, Nyakati za leo zinakataa. Wapo wanaoitazama dunia kuwa inaongwa kidkteta hasa Uchina, Korea Kaskazini, Korea Kusini, Urusi nk... Lakini hawafahamu kuwa ule sio udikta ni utawala wa sheria na katiba uliojengwa katika misingi ya karne ya 18-19 ambpo dunia ilikuwa chini ya mkono wa chuma. Leo ule SIO UDIKTETA.

Udikteta upo wa aina moja tu, ni utawala usiofuata katiba na sheria, utawala wa mtu mmoja tu, utawala wa matamko (decree), na madikteta wapo wa aina mbili, ambao ni Dikteta msomi, na dikteta mpuumbavu... Hawa hutofautiana katika staili zao za kutawala, Dikteta msomi hutawala huku watu wake wakilia machozi moyoni na usoni wakicheka, huku dikteta mpuumbavu, hutawala huku watu wake wakilia machozi machoni huku moyoni wakikenua meno... Uchaguzi ni wako.

Udikteta wowote hata ule unaopambwa na wajasiliasiasa kuwa ni udikteta mamboleo kamwe haujawahi kuiendesha dunia ya leo, labla kwenye nchi ya Nodi. Hakuna udikteta mamboleo duniani, hilo ni ingizo jipya katika uhalifu wa kisiasa wa wanasiasa wanaotumia vibaya kiuongo chao kiitwacho tumbo.. Tumbo ukiliruhusu likutawale litakufanya hata uwe Prof utafanya mambo kama Prof Lipumba au hata uwe Dr utafanya mambo kama Dr Rutengwe.

Demokrasia ya ulaya katika nchi masikini ni umasikini.

Mkuu, umeanza kulitambua lini hili? Na umeliishi kwa namna gani tangu ulitambue hili? Heri yako maana si kila macho yatazamayo yana uthubutu wa kuona.
 
Back
Top Bottom