Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,842
- 31,075
Hata hivyo kilichofanywa na Ukawa bungeni jana ni jambo la kawaida sana kwenye mabunge mengi duniani.
Hiyo ndiyo njia pekee ya kufikisha ujumbe kwa watawala ambao huwa wanajifanya 'viziwi' kutotaka kusikiliza hoja za msingi zinazotolewa na kambi za upinzani kwa maslahi ya Umma wa wananchi waliowapa ridhaa ya kuingia bungeni.
Hata hivyo mbona walichofanya Ukawa jana bungeni ni 'cha mtoto' ukilinganisha na kashikashi zinazotokea kwenye baadhi ya mabunge mengine duniani?
Yapo baadhi ya mabunge mengine huwa inafikia waheshimiwa wabunge wanazichapa kavu kavu kutokana na 'kiburi' cha watawala na hata wakati mwingine kurushiana hadi viti vilivyoko mabungeni.
Ujumbe pekee tunaoweza kumpa huyo Spika Ndugai na msaidizi wake Dr Tulia Ackson, kama hawatataka bunge letu lisifikie huko kulikofikiwa kwenye mabunge mengine duniani, watalazimika kujivua 'ukada' na wawe fair kwa wabunge wote bila kujali itikadi zao za kisiasa.
Lakini kama wataamua kupuuzia ushauri huu na wakaamua kuendelea kutumia 'mbeleko'yao ya Uspika kuibeba serikali basi watarajie ngumi zikichapwa humo bungeni siku si nyingi sana kutoka hivi sasa.