DED wa Itigi: Ninapakaziwa kesi ya mauaji

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,426
Singida. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, Pius Luhende anayedaiwa kuhusika na mauaji ya Isaka Petro (28) amezungumza na Mwananchi akisema “nimepakaziwa tu.”

Luhende alitoa kauli hiyo baada ya mwandishi wetu kumtembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida alikolazwa tangu Jumanne wiki hii baada ya kupewa rufaa kutoka Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.

Kwa mujibu wa mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Ng’hungu Kuzenza, Luhende anasumbuliwa na pumu (asthma) na mapigo ya moyo.

Mkurugenzi huyo ni miongoni mwa watu saba wanaoshikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo yaliyotokea Jumamosi iliyopita katika Kanisa la Wasabato Kijiji cha Kazikazi mkoani humo.

Inaelezwa kuwa mauaji hayo yalitokea baada ya Luhende kuwafuata watuhumiwa wa kosa la kuharibu mali ya mlalamikaji Rose Andrew aliyedai kuharibiwa mali yake iliyopo ndani ya shamba la Tanganyika Packers linalomilikiwa na halmashauri hiyo.

Taarifa ya Polisi inasema kuwa Luhende alipoingia ndani ya kanisa hilo ilitokea vurugu na akaamua kutoka nje kabla ya askari wanyamapori waliokuwa na silaha kufyatua risasi kadhaa na moja ikampiga Isaka na kufariki dunia papo hapo.

Hata hivyo, waumini waliokuwepo katika kanisa hilo wakati mauaji hayo yakitokea walizungumza na Mwananchi na kupingana na polisi wakisema kuwa mkurugenzi huyo ndiye alimfyatulia risasi Isaka.

Luhende ambaye alikuwa akilindwa na askari kanzu wanne wodini alisema bado kifua kinambana mara kwa mara hasa nyakati za usiku.

“Hata hivyo, namshukuru Mungu kwa kunipigania naendelea vizuri kuliko nilipokuwa hospitali ya Manyoni,” alisema Luhende ambaye alikuwa amejilaza kitandani huku mikononi akiwa hajafungwa pingu.

Katika maelezo yake, mkurugenzi huyo alisema amepakaziwa bila kufafanua zaidi kuhusu kauli yake hiyo.

Awali, Dk Kuzenza alisema mkurugenzi huyo alipofikishwa hospitalini hapo alikuwa na hali mbaya akibanwa kifua na tatizo la mapigo ya moyo.

“Tulipompokea alikuwa na hali mbaya kutokana na kubanwa mara kwa mara na kifua. Kwa upande wa mapigo ya moyo tatizo hilo lilianza kupungua. Kwa sasa tatizo la presha tumelidhibiti kiasi cha kutosha,” alisema. Alisema hata tatizo la asthma limeanza kupungua na kwamba atakuwa chini ya uangalizi hadi keshokutwa, “tukijiridhisha kuwa hali yake imeimarika, tutamruhusu kuondoka.”

Wakati huohuo, kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Isaya Mbughi amesema bado wanaendelea kukamilisha hatua za kisheria kabla watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani.

Alisema taratibu hizo zikishakamilika, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili. “Luhende endapo atakuwa ameruhusiwa kutoka hospitalini tutamuunganisha,” alisema kamanda huyo.

Juzi, kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike alisema “hatujawapeleka mahakamani, bado kuna taratibu nyingine hazijakamilika, kwa sasa tunaandaa taarifa ya kumpelekea mwendesha mashtaka wa Serikali ambaye ataandaa taratibu za kuwafikisha mahakamani.”

Mgogoro wa ushuru wa mashamba katika mbuga ya Kitongoji cha Boma la kati unatajwa kuwa ndiyo chanzo cha tukio kwani halmashauri inasema mashamba hayo ambayo awali yalikuwa yakimilikiwa na Tanganyika Packers ni sehemu yao.

Chanzo: Mwananchi
 
Kwanini waliingia Kanisani Na Silaha?

Huenda ni Kweli Yeye binafsi hajahusika lakin akiwa Kama Kiongozi aliona Ni busara Kweli kuvamia Mkusanyiko Tena ndani ya Nyumba ya Ibada ukiwa Na Askari wenye Silaha Za Moto?

Kama pale kanisani kungekuwa Na Waumini wenye silaha Za Moto Pia si ingekuwa Zahmatu minal balaa?

Nabii Suleiman Alayhissalam aliomba Sana Hikma kwa Kuwa Hikma ndio Msingi wa Uongozi bora sio Elimu kwa Kuwa Wasaidizi wako wanatosha kukushauri kitaalam nawe ukaamua kwa hekma

Mkurugenzi alikosa Hikma
 
Hata kama akufyatua yeye risasi kama anavyodai bado anayo kesi ya kujibu tena kesi ya mauaji ya kukusudia kwani yeye ndiye alitoa maelekezo na hata mazingira yote ya tukio yanamuhusisha yeye kama mtuhumiwa namba moja..tunazokumbukumbu za kesi mbali mbali za namna hii mfano ni kesi ya hivi karibuni ya bilionea Msuya wa Arusha..waliofungwa sio tu waliommiminia risasi bilionea msuya bali hata waliopanga mauaji pia
 
Kwanini waliingia Kanisani Na Silaha?

Huenda ni Kweli Yeye binafsi hajahusika lakin akiwa Kama Kiongozi aliona Ni busara Kweli kuvamia Mkusanyiko Tena ndani ya Nyumba ya Ibada ukiwa Na Askari wenye Silaha Za Moto?

Kama pale kanisani kungekuwa Na Waumini wenye silaha Za Moto Pia si ingekuwa Zahmatu minal balaa?
Nabii Suleiman Alayhissalam aliomba Sana Hikma kwa Kuwa Hikma ndio Msingi wa Uongozi bora sio Elimu kwa Kuwa Wasaidizi wako wanatosha kukushauri kitaalam nawe ukaamua kwa hekma

Mkurugenzi alikosa Hikma
Mungu awasaidie viongozi wetu kuwa na hekima na busara wasitegemee digrii,udaktari na uprofesa in makaratasi tu.
 
Kwanini waliingia Kanisani Na Silaha?

Huenda ni Kweli Yeye binafsi hajahusika lakin akiwa Kama Kiongozi aliona Ni busara Kweli kuvamia Mkusanyiko Tena ndani ya Nyumba ya Ibada ukiwa Na Askari wenye Silaha Za Moto?

Kama pale kanisani kungekuwa Na Waumini wenye silaha Za Moto Pia si ingekuwa Zahmatu minal balaa?
Nabii Suleiman Alayhissalam aliomba Sana Hikma kwa Kuwa Hikma ndio Msingi wa Uongozi bora sio Elimu kwa Kuwa Wasaidizi wako wanatosha kukushauri kitaalam nawe ukaamua kwa hekma

Mkurugenzi alikosa Hikma
mkuu ukifuatilia kwa makini maelezo ya huyu DED ,tabia zake, maelezo ya polisi na mganga mfawidhi na waumini utabaini DED ndo kaua! swali ni je alikuwa na pumu kabla? kazi amesimamishwa au bado
 
Nashangaa huyu mtuhumiwa wa mauaji hajapigwa pingu hapo kitandani? Au ndo wanataka kumtorosha kiaina wasingizie mtuhumiwa kawaponyoka!!! Pigeni pingu huyo!!! Alivimbiwa madaraka huyo!!!
 
mkuu ukifuatilia kwa makini maelezo ya huyu DED ,tabia zake, maelezo ya polisi na mganga mfawidhi na waumini utabaini DED ndo kaua! swali ni je alikuwa na pumu kabla? kazi amesimamishwa au bado

Kumtia Hatiani Mtu Kwenye kesi ya Jinai ya Mauaji sio jambo jepesi Kama kumtia Mtu hatiani kwa kusimama Na gari Kwenye Zebra

Risasi ikiyotumika Kwenye mauaji imepatikana?
DED ana miliki Silaha Na jee hiyo Silaha ina uhusiano Na Risasi iliyotumika?

Huyo Afisa Wanyamapori alikuwa Na Silaha ambayo inaweza kushabihiana Na Risasi iliyotumika?

Hukumu Za Mauaji hazitegemei Msimamo wa wengi Au matakwa ya wengi bali facts tupu
Simjui DED wala simjui huyo Afisa Wanyamapori lakin Ni dhambi kubwa kumsingizia Au kumuonea Mtu kwa Jinai Za aina hiyo

Tunapo urgue tusiingizie Mapenzi Au Chuki zetu Za Kisiasa Kwenye kuhukumu kesi hii
 
kiuchunguzi bdo tuko sana si wachunguze maganda ya risasi ni kutoka katika aina gani ya bunduki

sema polisi wetu wanaongozwa na siasa sio weledi
 
Kumtia Hatiani Mtu Kwenye kesi ya Jinai ya Mauaji sio jambo jepesi Kama kumtia Mtu hatiani kwa kusimama Na gari Kwenye Zebra

Risasi ikiyotumika Kwenye mauaji imepatikana?
DED ana miliki Silaha Na jee hiyo Silaha ina uhusiano Na Risasi iliyotumika?

Huyo Afisa Wanyamapori alikuwa Na Silaha ambayo inaweza kushabihiana Na Risasi iliyotumika?

Hukumu Za Mauaji hazitegemei Msimamo wa wengi Au matakwa ya wengi bali facts tupu
Simjui DED wala simjui huyo Afisa Wanyamapori lakin Ni dhambi kubwa kumsingizia Au kumuonea Mtu kwa Jinai Za aina hiyo

Tunapo urgue tusiingizie Mapenzi Au Chuki zetu Za Kisiasa Kwenye kuhukumu kesi hii
upo sahihi kabsa mkuu
ninavyojua Ma DED wengi hasa hawa wa magufuli wanamiliki silaha! namjua mmoja anaenda nayo hadi ofisini
 
Kwa hili DED ni vyema afikishwe Mahakamani. Kwanza yeye ndiyo alikuwa kiongozi wa msafara na amri zote zilikuwa zinatoka kwake. Yeye alitokaje ndani ya Kanisa na kufunga mlango?. Alikuwa na nia gani?. Mimi binafsi wa kuachiwea hapa ni Mwanasheria, Katibu Tarafa.
 
Kumtia Hatiani Mtu Kwenye kesi ya Jinai ya Mauaji sio jambo jepesi Kama kumtia Mtu hatiani kwa kusimama Na gari Kwenye Zebra

Risasi ikiyotumika Kwenye mauaji imepatikana?
DED ana miliki Silaha Na jee hiyo Silaha ina uhusiano Na Risasi iliyotumika?

Huyo Afisa Wanyamapori alikuwa Na Silaha ambayo inaweza kushabihiana Na Risasi iliyotumika?

Hukumu Za Mauaji hazitegemei Msimamo wa wengi Au matakwa ya wengi bali facts tupu
Simjui DED wala simjui huyo Afisa Wanyamapori lakin Ni dhambi kubwa kumsingizia Au kumuonea Mtu kwa Jinai Za aina hiyo

Tunapo urgue tusiingizie Mapenzi Au Chuki zetu Za Kisiasa Kwenye kuhukumu kesi hii
Kweli si vizuri kumhukumu Mtu.
Ila hii kesi itamkalia vibaya DED, na sababu ya kwanza yeye ni shahidi na mhusika muhimu. Sababu ya pili ni mazingira ya tukio, ilikuwaje aende kumkamata Mtu nyumba katika nyumba ya ibada? Kulikuwa na dharula ya kimsingi? Tatu inawezekana kweli askari afyatue risasi bila kupata amri ya bosi wake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes Yeye Atakuwa ama Shahidi upande wa Jamhuri Au Mtuhumiwa wa Mauaji!

Ila nimeshangazwa msiba kufanywa haraka sina Hakika Kama Postmoterm ilifanyika

Hiki tukio linanikumbusha tukio la Swahiba wangu Almarhuum Ukiwaona Ramadhan Mwinshehe Ditopile wa Mzuzuri ambae Kesi ile ilimnyima raha Pamoja Na kufarijiwa Sana Na Utawala Pamoja Na Ndugu wa Yule Dereva mpaka akazidiwa Na Msongo wa Mawazo Na Pressure Na hatimae akafariki Hotelini Morogoro

Kesi Za Mauaji zinasononesha Sana moyo Kuliko Za Ufisadi
Allah atuepushe Na vizazi vyetu mkosi huu wa kutoa nafsi ya Kiumbe pasi Na haki
 
Hii awamu inachekesha. Kanisani watu wana Biblia na Vitabu vya nyimbo, Serikali inaingia na silaha za moto. Mungu anajua kututetea sisi waumini ili kudhihirishia ulimwengu licha ya viongozi wa dini kusifia jiwe kuwa ndiye kiongozi aliyekuwa anategemewa.
Je Askari wa wanyapori kuingia Kanisani na silaha kulikuwepo na Tembo, au Nyati ndani ya kanisa? Au siku hizi wananchi wanaonekana kama wanyama? Kwanini hawakusubiri Ibada iishe? na kwanini si askali wa kawaida waingie wale wa wanyama?
 
Back
Top Bottom