Ninachojua kiongozi yeyote Anatakiwa kuonesha njia. Aya ya mwisho katika tangazo lako inachekesha na kushangaza. Halmashauri imejenga nyumba za wakuu wa idara kwa gharama ya zaidi ya 240M. Tena ya kuishi wewe DED na furniture ukawekewa, wewe mbona HUISHI PALE? Nyumba zimechakaa Ziko katikati ya pori na umeanza kufanya usafi baada ya kusikia RC atafanya ziara ofisini kwako. Acha unafiki toka lini ulikuwa na dhamana ya kusafirisha watumishi? Mbona watumishi tunatumia hiace kwa gharama zetu?Au unataka RC ajue unafanya kazi? Nashangaa umeanza na mchakato wa kukopa pesa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi ilhali zilizopo hazitumiki. Kama sio kutafuta Namna bora ya kuiba pesa ni nini?. Ungesema katika tangazo lako kuwa ni marufuku gari lisimchukue Afisa Utumishi ungeeleweka. Maana yeye ndio kila Siku gari humfuata nyumbani na kumrudisha.
Fanya kazi za kuhudumia jamii zaidi, Jiulize umefanya vitu vingapi ukijilinganisha na wenzio? Acha kuhangaika na DAGAA Kama ulivyowaita Siku wamepanda magari yako machakavu ambayo nawe umerithi. Umenunua gari kwa miaka miwili uliyokaa madarakani?