December | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

December

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jpinduzi, Dec 10, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Dec 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ikiwa zimebaki wiki chache kabla ya kuanza sikukuu mfululizo, hatuna budi kumshukuru Mungu kwa uwezo wake na mapenzi yake kutuacha hai mpaka siku hii ya leo tunapoelekea mwisho wa mwaka. Hakika tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa hilo!
  Katika mwezi Desemba wa kila mwaka, kuna mambo mengi ambayo hutokea hasa kwa wapendanao. Hakika ni mwezi mzuri sana kwa wale ambao ni waaminifu na wenye mapenzi ya kweli yasiyo na migogoro, lakini pia ni mwezi mbaya sana kwa wale ambao watahitilafiana na wapenzi wao.

  Katika mwezi Desemba mambo mengi hutokea, kuna ambao huachana na wapenzi, kuna ambao hupata wapenzi wapya, lakini suala la msingi ni kuwa makini na kuhakikisha humuudhi mpenzi wako.

  Katika hayo mengi ambayo hutokea mwezi huu, yakiwemo mabaya na mema ni vyema ukawa makini ili kuhakikisha kuwa yanayokufika mwezi huu ni mema zaidi kuliko mabaya! Hakika yote yanawezekana kama ukiwa makini. Lakini pia kuna ambao ni wapweke na waliochomwa mioyo yao na wapenzi wao, huwa ni mwezi mbaya zaidi kwao. Pamoja na hayo, hebu fuatilia vipengele vifuatavyo kwa makini ili ujue jinsi ya kusherehekea sikukuu zijazo vyema pasipo matatizo.
  WAPWEKE
  [​IMG]
  Huenda katika siku za karibuni uliachana na mpenzi wako na sasa upo katika hali ya upweke, usijali bado unaweza kusherehekea sikukuu zinazokuja bila kuwa na sononeko moyoni mwako. Elewa jambo moja rafiki/shemeji yangu mpenzi, katika kipindi cha sikukuu mambo mengi hutokea ambayo wakati mwingine huathiri kwa kiasi kikubwa maisha ya watu mbalimbali.

  Usilazimishe kutafuta mpenzi mpya haraka kwa nia ya kupata mtu wa kutoka naye ‘OUT' mwezi huu ulio na sikukuu kibao. Hakika ni hatari kwa sababu ni lazima utakuwa na mtu ambaye huna mapenzi ya dhati kwake, hata kama utakuwa umempenda ni wazi kuwa utakuwa umeamua kuwa naye kwa nia ya kuziba ufa ili usijione mpweke.

  Nakuhakikishia kuwa japokuwa unaweza ukatafuta mtu wa kuwa naye siku hiyo kwa nia ya kujiondolea upweke, lakini badala ya kuondokewa na upweke inaweza kuwa siku mbaya zaidi kwako na kukuachia historia mbaya katika maisha yako.

  Utakapotoka na mpenzi mpya ambaye umeamua kuwa naye kwa nia ya kuziba ufa, lolote linaweza kutokea! Pengine unatumia kilevi, baada ya kilevi kukolea unaweza ukajikuta ukifanya mapenzi na patina mpya bila kinga na hata kama ukitumia kinga usitumie kwa njia inayofaa.

  Usitake mwezi huu ukawa mwezi mbaya kuliko miezi yote katika maisha yako ya kimapenzi, achana na ulimbukeni, kubaliana na hali halisi kuwa sasa huna mpenzi, amini kuwa mwezi huu unaweza kuwa mzuri bila kuwa na mpenzi.

  Kimsingi unachopaswa kufanya ni kumuomba Mungu wako akupe amani katika moyo wako ili mwezi huu na hekakeha zake zote usije kuwa ni wa majonzi katika maisha yako.

  WENYE WAPENZI
  [​IMG]

  Hakika ni mwezi mzuri sana kwa ajili yenu, lakini pia unaweza kuwa mbaya sana kwenu. Ni mwezi ambao uamnifu wa mtu huonekana, uongo huonekana na mambo mengine mengi yaliyokuwa nyuma ya pazia huonekana kutokana na msongamano wa sikukuu. Ni siku mbaya sana kwa wale wasio waaminifu!
  Katika siku za sikukuu hasa za mwisho wa mwaka, lazima kunakuwa na ratiba za mtoko na mpenzi wako, sasa kama una mpenzi zaidi ya mmoja ndipo hapo mambo yatakapoanza kuharibika, kwa sababu utatoka na yupi hasa, sababu kila anayemdanganya kuwa yuko peke yake hukutegemea na kukuhitaji kutoka na wewe ‘out' mkasherehekee pamoja.

  Sasa basi kitakachotokea hapo baada ya kutoka na mwingine, huyo mwingine ambaye hujatoka naye lazima atapiga simu kila wakati na kukuandikia sms akitaka kujua kulikoni! Ni hapo sasa balaa litakapoanzia hasa kama mpenzi uliyenaye atafuma sms hizo.

  Uaminifu hauhitajiki mwezi huu pekee, uaminifu ni silaha madhubuti kwa ajili ya wapendanao na siku zote tunapaswa kuzingatia uaminifu kwa wapenzi wetu. Tambua kuwa dunia sio yako, fanya ufanyayo lakini elewa kuwa unafanya vibaya na mwisho wake hautakuwa mzuri.

  Jitahidi kutomuumiza mwenzako mwezi huu, ni mwezi wa furaha kwako na kwa mpenzi wako, sasa ukimwumiza mpenzi wako na kumwachia doa katika moyo wake, elewa kuwa sio tabia nzuri na utakuwa mwanzo mbaya wa maisha mapya katika mwaka mpya ujao. Usiruhusu mtu akamwaga machozi kwa ajili yako siku hiyo! Kwa sababu machozi hayo lazima utayalipia, kwa bahati mbaya sana malipo yake sio madogo, yatakugharimu sana maisha yako na yanaweza kuathiri maisha yako yote!
   
 2. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  wish you jpinduzi a marvelous festive season,mi na mwandani wangu tumeamua kujificha zetu Hawaii,tunaondoka kesho na emirates,karibu!
   
 3. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #3
  Dec 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  NASHUKURU MKUU!Safari njema!kila lakheri!
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Heri ya krismas na Mwaka mpya.

  Ila mimi sijui nna mtindio maandishi marefu hata yawe matamuje yananishinda.
  Bora uandike kwa namba.

  Asante source sredi ya Lizzy
   
 5. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #5
  Dec 10, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Umepiga kote kote Mkuu...
  kwa wapweke na walo na wapenzi.
  Safi saana.

  Asante kwa ujumbe mzuri....
  Naomba soma Sig yangu.:biggrin:
   
 6. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #6
  Dec 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nashukuru!Nimesoma sig yako,wishing you too.
   
 7. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #7
  Dec 10, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Pamoja Saana.

  ADI.
   
 8. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #8
  Dec 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
   
 9. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #9
  Dec 10, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Asante sana,yaani umenigusa kabisa mimi mpweke. Maskini wa Mungu sijui ntaitoa wapi amani ya moyo wangu. My heart has been broken into pieces and they've been scattered away.
   
 10. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #10
  Dec 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Amini tu ipo siku utapata wa kwako.
   
 11. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #11
  Dec 10, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Usijali my daughter, mwenyezi Mungu hamtupi mja wake! Vipi kuhusu kampani ya kidada dada, inanoga hiyo kwenye msimu wa sikukuu!!
   
 12. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #12
  Dec 10, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  uuuuhh!!! Yaani hiyo signature ndo inanimaliza kabisa, I wish to see some people aisee!!
   
 13. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #13
  Dec 10, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  am hoping maybe i would one day,but as for now ntajiepusha kabisa na maneno ya mapenzi
   
 14. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #14
  Dec 10, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  hao friends ndio wananikampan saa izi,i surely don know wat i would ave done without them.but stil kuna mtu nnammiss.
   
 15. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #15
  Dec 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  sijaelewa hiyo red hapo juu!
   
 16. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #16
  Dec 10, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Yeah......ni kweli, kwa sababu marafiki wamejaza sehemu yao tu as friends, so ile nafasi nyingine inahitaji mhusika wake. Lakini don't be so sad kiviiiile, mambo mengine huwa yanapita tu but there is that 'natural happiness' my dear, hope utairuhusu itake place! Nakutakia mema mpendwa wangu....
   
 17. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #17
  Dec 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kumbuka kwamba Mume/Mke mwema hutoka kwa Bwana na utaweza kupata pale utakapo omba (kwa IMANI) maana tumeambiwa tukiomba lolote tutapewa ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Na pia katika kitabu cha Wakolasai 3:15 tumeambiwa kwamba AMANI YA KRISTO IAMUE MIOYONI MWETU… Hivyo basi, endelea Kumuomba Mungu bila kukata tamaa.
   
Loading...