Dear WEWE........

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,090
Dear Wewe,

Yapata wiki ya tatu sasa nakuona ukiwa unatokea upande wa kaskazini wa pale ninapokuona kila siku asubuhi. Najua huenda hunijui lakini mie nakufahamu vyema kwani katika kipindi cha wiki tatu hizi nimefanya homework ya haja kiasi cha kujua mpaka nyumba uliyohamia. Labda nikukumbushe tu kama utanikumbuka, mi ni yule kijana niliyekusalimia siku ile ulipodondosha pochi yako baada ya kusukumwa na yule muuza matunda aliyekuwa na toroli pale kituoni, ingawa wakati najiandaa kuanzisha mazungumzo likatokea lile gari jeusi lenye namba za stk na ukapanda na kuondoka huku mi nikizuiliwa kuingia ingawa gari lilikuwa tupu.

Natumaini sasa umeweza kunikumbuka japo kidogo, najua utakuwa unajiuliza maneno meengi haya ninayoandika yana lengo gani, ntajaribu kupunguza maneno ili isiwe kama tuko kwenye mkutano wa siasa kule katani kwetu maana wale wanasiasa hupiga maneno mengi na dakika tano za mwisho ndipo husema lengo lao kubwa la kuwa kwenye mkutano ule. Basi mi nitaenda moja kwa moja kwenye dhumuni kuu ya waraka huu.

Baada ya kukuona siku ya kwanza na nakumbuka tulipanda wote daladala kuelekea mjini, moyo wangu ulihisi kupata ganzi. Sio kwakuwa we u mrembo sana, bali ni hali isiyoweza kuelezeka ya nguvu kali ya uvutano toka kwako ingawa nina shaka kama nguvu hii itakuja kuwa inatoka kwa pande zote mbili. Hata hivyo kwa kipindi chote hiki nimejaribu kufanya homework yangu ili kuweza kukufahamu nikisaidiwa na FBI ya kichwa changu, na LPD ya miguu yangu, CIA ya macho yangu na KGB ya masikio yangu. Pia nikapata msaada mkubwa wa Reuters na CNN ya karatasi na kalamu zangu ili kufanikisha mchakato mzima huu. Mchakato huu umefanikisha kujua mahali unapoishi, pale unapofanyia kazi, siku gani unazokwenda kazini na siku za mapumziko na hata kumjua yule rafiki yako ambaye nimekuja kugundua kuwa ni secretary wa pale kazini kwenu (yule mwenye maneno meeengi kama radio iliyowekwa betri mpya)

Jambo lililonopa moyo na mshawasha wa kuendelea na mpango wangu ni kutoona hata siku moja binadamu wa jinsia ya kiume akiingia ama kutoka pale nyumbani kwako. Hii ni kwa msaada wa CCTV kali za yule mama wa gengeni pale pembeni yenu, fundi viatu wa pale mwembeni pamoja yule dogo mjukuu wa mama mwenye nyumba wako ambao either nimelazimika kuwa mteja wa bidhaa zao au kulazimika kufadhili baadhi ya mahitaji yao ili kufanikisha kazi yao ya kuku-cctv na mimi kupata habari zote bila chenga.

Sasa hili ndilo langu ninalotaka kulileta kwako...........................................

Dont miss episode 2
 
Unapenda hadithi snowhite ?...ngoja nikuitie Kaizer akuhadithie....

niitie tu pacha
mi napenda maelezo bwana sijui ni hii HKL hii yani napenda kidume kijieleze sio haya mambo ya mtu unatuma sms nzuuri af kidume kijibu 'ok' yani huwa natamani mtu aone navofura kwa hasira!mi nimejieleeeza mwenye we cha kunijib mwenzio 'noted' ndo nini!hebu niitie Kaizer anipe maelezo naweza nikampa remedials leo
 
Last edited by a moderator:
amesemaje.......?

Sasa hili ndilo langu ninalotaka kulileta kwako......................... ..................
ahhahahhhahahhahahhaahh
 
niitie tu pacha
mi napenda maelezo bwana sijui ni hii HKL hii yani napenda kidume kijieleze sio haya mambo ya mtu unatuma sms nzuuri af kidume kijibu 'ok' yani huwa natamani mtu aone navofura kwa hasira!mi nimejieleeeza mwenye we cha kunijib mwenzio 'noted' ndo nini!hebu niitie Kaizer anipe maelezo naweza nikampa remedials leo

thanks
 
Ndio matatizo yenu wazee wa ngwine..sie wazee wa PCM..no story, formulae tu ..maisha yanasogea...
 
sijui labda nijifunze sasa lakini mi siwezi majibu mafupi i see!yani ni maelezo kwa kwenda mbele!hata hisia nazifungukiaga kwa maneno mengi i see!habari ya 'I :A S-heart-2: U' hapana kwa kweli shurti lazima nijimwage uwanda wa moyo!shem wako kashazoea manake na ye ni mzee wa PCM,ilikuwa kazi kweli kweli!
 
Hahahaaaaaaa! Si umface huyo dada umueleze live bila chenga????
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom