mukizahp2
JF-Expert Member
- Jul 28, 2012
- 705
- 378
Dear Mwalimu Nyerere,
Tangu ututoke hapa nchini hali Imebadilika sana:
Kwanza siku hizi Ziwa Nyasa liko nchini Malawi, mlima Kilimanjaro uko Kenya na wachaga wote ni watu wa Kenya, Tanzanite inazalishwa South Africa.
Mbaya Zaidi Shirika la kutoa huduma kwa Jamii bure enzi hizo TANESCO nasikia limekuwa la Waziri mstaafu Mwenye Mvi nyingi, siku hizi Rais Wetu Hakai Ikulu kusikiliza matatizo yetu Bali anakaa Airport ili awahi Ulaya kuomba misaada na mgodi wa Kiwira coal mine ni Rais Mstaafu na Karamagi.
Vilevile yale madini uliyosema tusiyachimbe kwa sasa mpaka tupate watu wenye akili, wameanza kuchimba wanabadilishana na Vyandarua vyenye ngao ya kudumu, na Ninasikia tetesi hata Kaburi lako halipo Tanzania Liko Butiama Kenya.
Shirika la ndege halina ndege sababu zimeharibika kwa kubeba twiga na meno ya tembo badala ya watu na mizigo.
Mwalimu kile chama chako ulichokianzisha kimesahau kila kitu ulichowaambia, kuna mabilionea kwenye chama kuliko East Africa nzima. Polisi enzi zako walikuwa wanalinda raia, mwalimu siku hizi wana kazi moja tu kuua raia wasio na hatia na wanaua hadi waandishi wa habari!
Mwalimu, usalama wa taifa enzi zako walikuwa wanaangalia usalama wa taifa ila siku hizi wapo kwenye misitu mabwepande! Mwalimu lile jeshi lako la JWTZ siku hizi lina watu wenye fedha nyingi sana sababu ya miradi feki.
Nina mambo mengi sana ila mwisho ile nchi uliyoiacha sio hiyo tena, siku hizi kuna wakuu wa wilaya, wakuu wa makampuni ya umma, watoto wa rais, marais wastaafu, mawaziri wakuu waliostaafishwa, wakuu wa usalama wa taifa na JWTZ ambao ni mabilionea!
Mwisho kabisa, mwalimu benki zetu zimekuwa ndogo kwahiyo hao niliowataja hapo juu wameamua kupeleka hela zao Uswiss"
Ni mimi
Mtanganyika