Dear Men, kwanini ni vigumu kusema samahani?

Poleni sana akina dada na mama zetu.Hiyo ni changamoto kubwa sana mnayopata kutoka kwetu wanaume.
Nimeyashuhudia hayo sana mpaka huwa naumia sana.Tena sio samahani tuu hata kusema asante tuu kwa mpenzi wako kwa jambo lolote ni shida.mf.MKEO/mpenzi...amekupikia amekuandalia chakula unashindwaje kusema asante sana na kumtia moyo zaidi.
Mimi ni mwanaume lakini huwa ninaomba msamaha kwa siku mara nyingi sana hata kama ni kakosa kadogo sana mf,missed call..kuchelewa kidogo hata kama nilimpa taarifa lakini nitakapo rudi lazima nimuombe msamaha mke wangu na kumpa pole kwa kuwa mpweke ingawa ndoa yangu sasa ina miaka 10...
Tujitahidi wanaume kuomba msamaha haraka pale tunapojua umemkwaza mwenzio hata kwa jambo unaloliona wewe ni dogo lakini kwa mwenzio linaweza kuwa limemuumiza sana.

Semeni asante kwa kila jambo unalotendewa na mkeo mpenzi mtajikuta mnapunguza migogoro mingi midogomidogo ambayo ndio chanzo cha kukosekana kwa amani na maelewano kwenye ndoa.
Si kwamba mke wangu ni bora sana ila nimejua kuwa mume ukuwa na akili unaweza kumfanya mke hata mbaya akawa mzuri cha msingi ni kila jambo unalofanya ni lazima utumie hekima sana hata kama unaona unayo haki au umekosewa.
 
Kuomba radhi ni hulka ya mtu.. Si kweli wanaume hatuombi msamaha tunapokosea. Wote tu tuko hivyo usitarajie uko matawi then kila siku wa kujishusha yeye tu
 
Sipendi kusema samahani hata kama nimekosea kwa sababu sisi wanaume wa tarime hatujafundihswa hiyo sorry.... Sisi tukosee tusikosee huwa tunajieka katika nafasi ya kwamba tuko sahihi.
 
dah kaka mahusiano yangu yako complicated sana huyu binti yupo wired na mother na ni rafk wa familia kwa ujumla. maamuzi magumu huwa yanashindikana
Kama familia ndio watakao ishi na huyo binti basi sawa lakini mm naona ww ndio muhusika mkuu.
 
Mwanaume wako ndio mgumu kusema samahani
 
Kuomba msamaha kwa mwanaume ni weakness!!!ushaona baba anajamba alafu mnacheka watoto???mwiko!!!
 
Hebu tuache na ubabe wetu sisi..
 
Cous kosa ni hali isiyoonekana, laiti ingeonekana, hata mm ningekuwa wa kwnz kuomba msamaha
 
Yaani wadada mna maswali yaajabu sana yale ya msingi mnayaacha, kwanini usijiulize nikwanini mwanamke akichepuka hua hakiri (kukubali) hata umshikie kisu atakataa bora umuue na ukimpga au ukimfukuza anaanza kulalamika eti "kwanini wanaume hawawezi kusamehe kama wanawake"? Sasa shida inajia kwamba huwezi kumsamehe mtu ambaye hajakiri kosa. Na jibu la swali lako nikwamba wanawake ukifanya kosa ukimuomba msamaha anataka akusakame kutwa lakini mwanaume ukimuomba msamaha anakusamehe na anakua kimyaa
 
Yani Sijui wapoje wanaume yani mie jamaa wangu ukimkosea ukamuomba msamaha next time ukimkosea anakumbushia kosa la nyuma yani anaboa mpaka nawazaga kumwaga Ila yy kuomba msamaha yupo fast
 
Hili tatizo dada angu ni kwa watu wote. mi nina mchumba angu hata anikosee vipi huwa haombi msamahaa. ukimuuliza kwann anakuambia yeye humuomba msamaha mungu tu. Huwa naishia kusikitika tu[emoji20] [emoji20]
Hakufai kbs Mimi sijaolewa sina mpnz wala mchumba lkn Huyo mwanamke hakufai... Si kwamba nakuonea wivu la hasha!! Ila hakufaiii utakuja kunipa mrejesho we muoe
 
Yani bora umelisema mwenzangu utafikiri ulikuwa moyoni mwanguuu

Wanaume ni wazito sana kuomba samahaniii tena Sana'a
Style yao ya kuomba ni hivi
Yaishe basi
Kausha bhanaa
Mbn unagubu we mwanamkea si yameisha
Yapotezee bhanaa

Ni wanaume wa chache sana wanaoweza kujishusha nskusemaa samahaniii

Atakwambia huo ni uboyo kumuomba mwanamke samahanii
 
Hakufai kbs Mimi sijaolewa sina mpnz wala mchumba lkn Huyo mwanamke hakufai... Si kwamba nakuonea wivu la hasha!! Ila hakufaiii utakuja kunipa mrejesho we muoe
Tatzo yupo wired na mother. Ndugu wote anacheza nao vzr wanampenda sana. tatzo ndo lipo kwenye hicho kipengele na makelele sometimes
 
Kuomba msamaha ni jambo la heri hata kama ulimuudhi mwenza hushusha pumzi na wala si ujinga bali hujenga upendo, lakini ubabe ndiyo hupelekea visasi na kulipizana visasi tambua asiye omba msamaha daima hilo kosa hulirudia tena na tena
 
Kitendo cha kuomba radhi ni cha hekima na busara, ni cha kutambua jinsi gani umekosea na uko tayari kubadilika...Kuomba msamaha hudumisha mahusiano na kufanya muishi vyema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…