Mrs Bishanga
JF-Expert Member
- Jun 30, 2013
- 1,002
- 2,293
Ikiwa bado siku chache kumaliza mwaka 2019 nimetafakari sana mambo ambayo mama anayafanya katika maisha ya mtoto wake.
mbali na kuwa nimekuwa mtu mzima ambaye najitegemea kwa kiasi kikubwa bado mama yangu amekuwa na mchango mkubwa katika maisha yangu. Nikiwa nimezongwa na mawazo ya maisha kimbilio ni Kwa mama yangu....nikisikia sauti yake tu ninapona na kujiona mpya kuweza kuikabili changamoto iliyo mbele yangu.
Hivi Hawa wamama wameumbwa na roho za aina gani? Wao yawe mazuri au mabaya huyabeba bila lawama.
Wana upendo wa kujitoa .....Yani hapendi kuniona ninasononeka? Yani hata awe na Akiba yake akiniona Nina mawazo ya kutatua ishu flani ya hela Basi Mara moja tukimaliza tu maongezi nitaona muamala wa tigopesa unasoma....kucheki mama ashaziba shimo...
Hata nikosee vipi huwa hahukumu Kama walivyo wababa. Huyu mama huwa namkosea weeeee lakini siku zote amebaki kuwa mtulivu na wa kusamehe bure bila hata kuombwa msamaha.
Mama ameweza kutoa Vingi ili kuniona ninatimiza ndoto zangu na ninakuwa mtu wa furaha bila kujali malipo.
Ee Mungu nijalie siku moja na Mimi niweze kumfurahisha mama yangu hadi asahau taabu zote alizopitia Kwa ajili yangu.
Ee mama nakuombea maisha marefu katika dunia hii.
Mpende mama yako bila kujali Hali yake.....mama Ndio mtu pekee duniani hapa ambaye hata dunia yote ikuzomee bado atabaki amesimama na wewe mpaka dakika ya mwisho.
Kama unamuombea mama yako heri Basi usipite bila kutia neno.View attachment 1304903