Deadline yangu mwakani, ndoa lazima nifunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Deadline yangu mwakani, ndoa lazima nifunge

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ms Judith, Jan 27, 2011.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  1.
  Kila niwapo salani, naomba mola nichunge,
  Nipatetinga ndoani, upendo wako nipunge,
  Niishi kama peponi, dunia isinizonge,
  Dedilaini mwakani, ndoa lazima nifunge

  2.
  Butege aliuliza, kwa vipi ningali misi,
  Hoja yake kakuza, wangu huu si halisi,
  Hata bila kuuliza, yeye kajipa makisi,
  Dedilaini mwakani, ndoa lazima nifunge.

  3.
  Kweli wengi nimeepa, wachumba pia washenga,
  Walokuwa na za epa, wote walipigwa chenga,
  Walonukia vikwapa, kwa wao huo mpunga,
  Dedilaini mwakani, ndoa lazima nifunge

  4.
  Walianza praimari, nikiwa bado kichanga,
  Enzi zile sekondari, wengi walijiunga,
  Chuo hakika hatari, kama vya hari vimbunga,
  Dedilaini mwakani, ndoa lazima nifunge

  5.
  Kutunza bikira kazi, katika hii dunia,
  Wengi waruka wazazi, kwa zao mbaya tabia,
  Ya siri sasa ya wazi, wapi bikira tunzia,
  Dedilaini mwakani, ndoa lazima nifunge

  6.
  Namshukuru Manani, himeni yangu salama,
  Hadi huko mwakani, haitotiwa alama,
  Wala siweki sokoni, yake wangu kujinoma,
  Dedilaini mwakani, ndoa lazima nifunge

  7.
  Maisha yetu mabinti, kweli yataka hesabu,
  Ili kupata pointi, liwe sahihi jawabu,
  Ukihaha nazo senti, tachacha kama ulabu,
  Dedilaini mwakani, ndoa lazima nifunge

  8.
  Miaka inapopaa, nawe wapaswa jipanga,
  Ni nani wa kukufaa, lazima kichwa kugonga,
  Japo awe msambaa, tabibu au mchunga,
  Dedilaini mwakani, ndoa lazima nifunge

  9.
  Mimi yangu tayari, ndoa ni hapo mwakani,
  mlio nayo mahari, sasa leteni ukweni,
  hima leteni habari, ya ndoa ilo makini,
  Dedilaini mwakani, ndoa lazima nifunge

  10.
  Nawaaga mabachala, nao wenye masitazi,
  wapweke na makapela, usingo hakika kazi,
  hata ukiwa na hela, hazikwishi jinamizi
  Dedilaini mwakani, ndoa lazima nifunge
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  :clap2:
   
 3. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mmh, sijakuelewa hapo. weka kamstari japo kamoja nawe ujaribu vina na mizani basi. hahah.

  mzima lakini, ulipotea sana na nilikumiss
   
 4. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Mimi mzima ndugu, hapo kwenye kuweka vina na mizani usiwe na wasi wasi,, ndo namalizia ubeti wa mwisho halafu nitamtuma mshenga aje kughani kwenu,,, ila natumaini na yeye hutamkwepa kama ulivyotanabaisha kwenye ubeti wa tatu.....

  Tulimisiana kwa kweli:tea:
   
 5. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Mungu Akubariki malengo yatimie nikapata Muda nirtaweka mashairi kukusaidia
   
 6. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  hodi hodi naingia, naomba nipokeeni
  miss nakusalimia, bibie u hali gani?
  waanza kufurahia, ndoa ya hapo mwakani
  mchumba hatujamjua,usitufiche jamani

  mbona umejiamini , kwenye lako shairi
  ni lazima mwakani, hakuna hili na hili
  muowaji ni nani ?, umeificha kauli
  hapa kuna siri gani?, taja ubavu wa pili

  yupo hapa jeiefu?, suala najiuliza
  ni upi wake wasifu?, shule ameshamaliza?
  macho yake ni kipofu? au ana makengeza?
  utatujuza halafu? , maelezo yako giza

  kama haujampata, mbona umejiamini?
  kwa makeke mejikita,lazima iwe mwakani
  kama unamtafuta , usiweke dedilaini
  yasije yakakukuta, ukakimbia jamvini

  naomba ufafanuzi, nipate kukuelewa
  nisije nikakuuzi , mke wa mtarajiwa
  pengine ni mwanafunzi, shairi sijaelewa
  kipenzi wangu laazizi , naomba fafanuliwa

  na kama ni siri yako, usihofu endelea
  harusi sio maziko , dua tunakuombea
  ufurahi na mwenzako, kama ushajipatia
  au kesho aje kwako, kama wajitafutia
   
 7. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Miss Judith kumbe nawe umooo eehhh haya kila la kheri dear
   
 8. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Kutunza penzi ni kazi katika hii dunia
   
 9. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,361
  Likes Received: 3,193
  Trophy Points: 280
  Kama hilo shairi umejiimbia wewe basi mimi na mke wangu tunakutakia ndoa njema. Lakini ubeti wa kwanza kwamba uishi hapa duniani kama peponi sidhani, kumbuka hapa duniani hata Yesu alijaribiwa.

  Kila la kheri twakutakia, mchango wetu elfu thelathini (isiwe ndoa ya kifahari please)
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,480
  Likes Received: 81,771
  Trophy Points: 280
  Kila la heri Judy. Kwa michango yako hapa jamvini miye nakuona ni mtu makini sana hivyo huyo atakayebahatika kukuoa atapata mke mwema na ndoa yenu itadumu kwa miaka mingi.


   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Kila la heri.
   
 12. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  All the best :clap2:
   
 13. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Hongera mama kwa uamuzi wa maana!
   
 14. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280
  Hivi hii si ingeenda kule kwenye forum ya burudani? Au ungetoa single. Halafu wewe ni Miss Judith na yule mwimbaji wa ubongo wa flavour (JeyD) ni Judith Wambura, ndio huyo huyo au tofauti?
   
 15. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  muweke Muumba Mbele, kwa unayojipangia
  Akupe baraka tele, mwenza kukupatia
  sali na omba milele, utakacho kitamea
  Nakutakia lakheri, Katika yako mipango

  Miss uwe misezi, dada uitwe mama
  upate watoto shazi, maisha yawe mema
  Upate mme mlezi, shida zenu kuzizima
  Nakutakia lakheri, Katika yako mipango

  funzadume mwana wa washawasha
   
 16. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Asante klorokwini, mistari yako makini,
  Karibu sana ukweni, sote tutakuthamini,
  Kama hujawa ndoani, nawe wafaa kundini,
  Beti ya tisa makini, bado ni mchakatoni,

  Beti ya tisa I wazi, mchumba bado kupata,
  japo kumpata kazi, kwalo siwezi kudata,
  Mwakani hilo ni wazi, lazima nitakamata
  Beti ya tisa makini, bado ni mchakatoni,

  Walojitokeza kenda, watatu walizimia,
  Vitendo wakavitenda, subira kuazimia,
  Mie nikubali tenda, mlango wafungulia
  Beti ya tisa makini, bado ni mchakatoni,

  Kauli sikuitoa, nani wa kumkubali,
  Masomo yalizingia, ratiba ikawa kali,
  Muda kusubiria, hadi ifaapo hali,
  Beti ya tisa makini, bado ni mchakatoni,

  Jiamini sina budi, japo bado kumpata,
  Sina walau ahadi, nachanga vyema karata,
  Taweka hata miadi, moja lazima tanata
  Beti ya tisa makini, bado ni mchakatoni,
   
 17. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  asante funzadume, kwa hizo zako Baraka,
  mwema mwana wa kiume, najua hilo hakila,
  wanena kama mtume, kwa yote uloandika,
  Mola anipapo mume, duazo tazikumbuka,

  Misi kuwa misezi, hilo jema hakika,
  dada geuka mzazi, hizo za mola Baraka,
  yakiwa mema malezi, shukuru kwazo fanaka,
  Mola anipapo mume, duazo tazikumbuka,
   
 18. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  haha....

  wako siwezimkwepa, hilo liko hadharani,
  nafasi hiyo takupa, kama ukija makini,
  mkono sitakutupa, takutia maanani,
  kama waweza kulipa, jongea sasa ukweni
   
 19. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Miss Judith, all the best my dear!!!,
  lakini italeta raha zaidi,
  ukimpata mume anaejua kughani vilevile!!!!!
   
 20. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #20
  Jan 28, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  karibu mbona wasita, na muda waulilia,
  hata pasipo vitita, vya muda utawezea,
  shairi nalo lapita, wengi wanalimendea,
  beti zipake mafuta, zing'are kusaidia
   
Loading...