DC wa Tanga nusura amsweke rumande padre

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
990
Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki parokia ya Chumbageni, Padre James Kabosa ameponea chupuchupu kuswekwa ndani na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego kwa madai ya utovu wa nidhamu. Tukio hilo limethibitishwa na Mkuu wa wilaya mwenyewe, Padre Kabosa na msemaji wa Askofu, Padre Peter Kagaba walipozungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti.





Imedaiwa kuwa padre huyo aliepuka kuswekwa ndani kwa kuondoka ofisini hapo baada ya kutofautiana na mkuu huyo wa wilaya na hivyo kumuita mkuu wa polisi wa wilaya afike na kumsweka ndani ndipo wazee wa kanisa waliokuwa wameambatana naye kumsihi Padre aondoke. Imedaiwa kuwa baada ya tukio hilo Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Tanga, Mhashamu Baba Askofu Anthon Banzi, alifika ofisini kwa mkuu huyo wa wilaya akitaka kujua chanzo cha Padre Kabosa kufukuzwa na kutishiwa kuswekwa ndani.

Habari zimebainisha kuwa baada ya mkuu wa wilaya kuona Askofu ofisini akiwa na waumini alimuelewesha kiini cha kumtimua Padre na kumuomba msamaha. Waumini waliokuwa wamemsindikiza Askofu wao walishikwa na butwaa baada ya kumuona mkuu wa wilaya huyo akipiga magoti mbele ya Askofu Banzi na kuomba abarikiwe na askofu kwa madai mumewe pia ni mkatoliki abarikiwe ili Mungu amsaidie katika kazi zake za kuiongoza jamii.

Akiongea na NIPASHE kuhusu tukio hilo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mtakatifu Mikael, Kiule Msofe, alisema tukio la kufukuzwa kwa Padre lilitokea Machi 27, mwaka huu majira ya saa 8 mchana na tukio la Askofu kufika kwa mkuu huyo wa wilaya lilitokea Aprili 3 na kuwa matukio yote mawili alikuwapo na kuyashuhudia.

Kuhusu chanzo cha tukio hilo, Kiule alisema ni kutokana na mgogoro wa ardhi wa eneo la wazi lililogawanywa na diwani wa kata ya Nguvumali, Selemani Mhina (sele boss) CCM, lililopo mbele ya kanisa la Kigango cha Majani Mapana kinyume cha sheria za ardhi.
Alisema kanisa katoliki lilishaomba eneo hilo zaidi ya mara mbili kwa Jiji la Tanga na kujibiwa kuwa ni eneo la wazi na lakini lilitolewa kwa wafanyabiashara kwa madai kuwa ni agizo la mkuu wa wilaya ili kujenga mashine za kusaga nafaka. Kwa upande wa padre Kabosa alikiri kupatwa na kadhia hiyo lakini alidai kuwa tayari suala hilo linashughulikiwa na viongozi wakuu wa kanisa hilo kwa hatua zaidi za kurejesha amani na mshikamano ulioonekana kukosekana.

Naye Mkuu wa wilaya, Dendego alipotakiwa kuelezea shutuma hizo alikiri ujio wa padre Kabosa ofisini kwake na kutofautiana kimazungumzo lakini alidai kuwa alimuamuru kuondoka ofisini hapo kwa kuwa hakumtambua kama ni kiongozi wa dini.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya alikanusha tuhuma za kueneza udini na kwamba hilo halikufanyika kwa ajili ya udini bali ni moja ya matokeo ya kiutendaji. Alimtupia lawama na kumtaja diwani Mhina kuwa ndiye anayechochea mgogoro huo kwa kueneza udini kuwa yeye anawapendelea waislamu jambo ambalo ni hatari.



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI


 
Jamani huyu mama kachanganyikiwa. Ndo maana watu wenye uelewa wanaomba mapumziko na wanasafiri wanaenda mbali. Apumzike matatizo yamemzidi.
 
Kwann uandike uongo mbn nipashe hawakuandika hizo habari za mkuu wa wilaya kupiga magoti kumuomba askofu ambariki,ww umezitoa wapi?
 
Kwann uandike uongo mbn nipashe hawakuandika hizo habari za mkuu wa wilaya kupiga magoti kumuomba askofu ambariki,ww umezitoa wapi?

Sihitaji kuandika uongo, una ruhusa ya kucheki hapa:

:: IPPMEDIA

Swali ninalotaka kuuliza hivi Tanzania kila mtu akishakuwa 'district au regional something' basi anaamuru tu mtu asiyekubaliana naye awekwe rumande? Mipaka ya hawa viongozi wa jk ni ipi, na je wananchi wa kawaida wanaifahamu? Inaelekea kwa mwendo huu mpaka 2015 wataingizwa wengi sana rumande!
 
Cv ya Dendegu please.... Maana kila ucho tunapata news mpya za matukio
 
Capture.JPG
Kwa wale wanaosema habari hii ni ya uongo...haya basi.
 
Hivi nani ana haki ya kumuweka ndani mtu Tanzania? Ni viongozi au ni kazi ya polisi. Inatisha, maana kumbe ukitofautiana mawazo na kiongozi unaweza kuwekwa ndani!!
 
Huyu mama ana Mume kweli!? Maana matukio ya kibaamedi kila kukicha. Alinivunja mbavu alipopiga magoti kuomba upako...hahaaaa.
 
Ukishamuita mtuu mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya inakuwa inamaanisha kuwa yeye ni mkuu kuliko wananchi wote hapo mkoani au wilayani.
Sasa ni mwaka 2013 lakini tanzania tuna vyeo vyenye sura ya ukoloni na haya ndiyo matokeo yake.
Hivi vyeo vyenye minajiri ya ukoloni tunapaswa kuvifuta kwa kupitia mabadiliko ya katiba.
Kiongozi wa umma aliyechaguliwa na umma hawezi kufanya maamuzi ya kikatili kama ya uyu Dc mteule wa JK.
Kwa muda sasa tunasikia hawa wateule wa raisi wanatumia ofisi zao kuzalilisha watanzania, mwingine ametukana mwanasheria wa halmashauri kuwa ana degree ya chupi, mwingine anasweka ndani viongozi wa halmashauri, yani kwa kifupi vyeo vyote vya kuteuliwa kuanzia majaji, wakuu wa wilaya, wakuu wa mkoa n.k tuwapigie kura ndio wakabidhiwe ofisi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
nimependa hapo alipopiga magoti kwa baba Askofu. kumbe anaheshima ila jeuri tu.!!
 
Kwann uandike uongo mbn nipashe hawakuandika hizo habari za mkuu wa wilaya kupiga magoti kumuomba askofu ambariki,ww umezitoa wapi?

kinachokukera wewe ni Askofu kupigiwa magoti, mbona kawaida tu.!!
 
Hivi waandishi wa habari hawajui kuwa paragraph ya kwanza na pili ya habari ni lazima ielezee what,where,how when and possibly why? Yaani unasoma habari unakuja kukuta chanzo (what) paragraph ya pili kutoka mwisho,uandishi wa wapi huu?Mimi sio mwandishi wa habari lakini za kuripoti habari au tkio zipo the same katika tasnia karibu zote,kwa nn waandishi wa habari wa TZ mnatuchosha kusoma habari nzima ili kujua nn kilitokea????!!!!
 
kwa hiyo mkitofautiana mawazo tu na mkuu wa wilaya au kiongozi wa serikali solution ni kukusweka ndani? Ama kweli ccm oyeee
 
Hivi nani ana haki ya kumuweka ndani mtu Tanzania? Ni viongozi au ni kazi ya polisi. Inatisha, maana kumbe ukitofautiana mawazo na kiongozi unaweza kuwekwa ndani!!

Ndo katiba yetu hii, inampa mkuu wa mkoa/wilaya mamlaka makubwa, si unajua hawa jamaa ndo wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama. Kuna haja ya kuondoa huu uozo kwenye katiba mpya.
 
Taasisi ya kidini iwe ya kikristo ,kiislam au dini nyingine zinahudumia umma,kinachonishangaza hapa ni iweje kanisa lililoomba eneo hilo mapema linyimwe kwa maelezo kwamba ni eneo la wazi na baadaye wapewe wafanya biashara tena wa kusaga unga? wangekuwa wanajenga uwanja wa mpira ningeelewa maana nao una sura ya uwanja wa wazi maana unaweza kutumiwa kwa matukio ya umma.
Mimi naona dhana ya udini kufutika hapa nchini ni lazima ipitie mlango uleule ilikoingilia ambako ni mioyoni mwa viongozi wa serikali ndo itakubali kutoka.Kama dhana hii haikuisha mioyoni mwao siyo rahisi kuimaliza huku nje.
Jambo hili linafanana na ubepari ulioko mioyoni mwa viongozi waliowengi lakini nje unazungumzwa ujamaa,matokeo yake kila anayepewa nafasi anafanya yale anayoyaona moyoni mwake,na hii imezaa neno ufisadi lisiloisha kila kukicha.
Namshauri huyo mkuu wa wilaya kama kweli siyo mdini,awape hilo eneo maana walikuwa wa kwanza kuliomba la sivyo liendelee kubaki wazi kama ilivyotamkwa mwanzo,Vinginevyo sisi watazamaji hatuna jina jingine la kumpa huyo Dc isipokuwa MDINI
 
Back
Top Bottom