DC wa JK na CCM kayafanya haya hadharani

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
DC amtimua jukwaani diwani wa Chadema Send to a friend
Monday, 19 September 2011 20:10
0diggsdigg

Shija Felician, Kahama
MKUU wa Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, Meja mstaafu Bahati Matala, nusura avuruge kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru yaliyofanyika wilayani hapa, baada ya kumtimua jukwaani Diwani wa Kata ya Majengo (Chadema), Bobson Wambura, hali iliyopingwa na wafuasi wa chama hicho.

Sakata hilo lililotokea juzi saa 5:00 asubuhi kwenye uwanja wa halmashauri ya wilaya, Matala alipanda jukwaani na kuanza kuwatambulisha viongozi waliojumuika akiwamo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama, Andrew Masanje, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri, Eliza Bwana na Mwenyekiti wa halmashauri, Alfred Mhanganya.

Matala baada ya kumwona diwani huyo akiwa amekaa na viongozi hao jukwaani, kwa kutumia kipaza alitangaza akimtaka Wambura kuondoka mara moja.

“Bobson ondoka jukwaani mara moja,” alifoka Matala.Hatua hiyo iliwakasirisha watu wengi waliokuwa wamehudhuria na kuanza kuguna, hali ambayo ilitulizwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Masanje ambaye alichukua kipaza sauti haraka kutoka kwa Matala, huku akimtaka diwani huyo kurejea mara moja jukwaani na kusalimia wananchi.

“Bobson tafadhali rudi uwasalimie wananchi wako, sioni sababu ya kumfukuza diwani wa Chadema kwenye jukwaa hili, leo tunasherekea miaka 50 ya uhuru wakati mwaka 1961 tunajitawala, uhuru ulikuwa wa Watanzania wote siyo Chadema wala CCM, sherehe hizi ni za watu wote,” alisema Masanje huku akishangiliwa na wananchi.
Licha ya Masanje kupinga uamuzi wa mkuu huyo wa wilaya, alirudia tena upya utambulisho wa madiwani wote akiwataka wasimame na kuwapungia mkono wananchi.

“Waheshimiwa madiwani popote mlipo pamoja na Bobson simameni muwapungie mikono wananchi,” alisema Matala.Akizungumzia hatua hiyo, baada ya kumalizika kwa sherehe hizo, Wambura alisema alisikitishwa na kitendo cha mkuu wa wilaya kumfukuza jukwaani, ilhali maadhimisho hayo yalikuwa yanafanyika kwenye eneo lake na kwamba, atafikisha suala hilo kwa wananchi.

Katika hatua nyingine, utoaji zawadi kwenye kada mbalimbali zilizoshiriki maadhimisho hayo nusura uingie dosari baada ya mwanamke mmoja, kuangua kilio mbele ya mgeni rasmi kutokana na kuchakachuliwa kwa zawadi yake ya Sh100,000 aliyoahidiwa kwa kushinda mbio za baiskeli upande wa wanawake.

Kilio hicho kilianza baada ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Kapteni mstaafu James Yamungu, kutangaza Sh50,000 iliyomfanya mwanamke huyo kupinga na kuangua kilio.Baada ya kuona hali hiyo Yamungu alitaka kuongeza fedha yake kuokoa jahazi, lakini Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Orest Mushi, alianzisha mchango wa papo kwa hapo.


 

SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
33,197
37,376
Ma-DC wapuuzi kama hawa tukiwadhibiti BAKWATA inawatetea,tutaedelea kula nao sahani moja hatuchekei uhalifu sisi kama hao magamaba na mashehe ubwabwa wao.
 

Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Hii thread mbona inarudiwa? Tayari kuna thread kama hii na ambayo inaendelea kuchangiwa.
 

We Know Next

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
797
363
Basi nae achukuliwe hatua kwa kuvujna sheria kumvukuza Diwani ambaye ni chaguo la wananchi siku ya kusherekea miaka 50 ya Uhuru
 

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
408
Matumizi mabaya ya madaraka.
...Hivi huyo diwani akiamua kumkomoa huyo DC si anaweza kumshitaki kwa kumdhalilisha hadharani? Hivi alikuwa na sababu gani ya maana ya kumfukuza pale jukwaani. Kweli watawala wa wabongo hamnazo kabisa..
 

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
unlike wana ccm ambao huwa wanaona mabaya tu ya upinzani mimi nachukua hatua hii kumpongeza bwana andrew masanje mwenyekiti wa CCM huko shinyanga kwa kumkumbusha DC kuwa uhuru siyo wa CCM bali ni wa wananchi wote.
 

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,897
1,287
nilisema siku za nyuma, nitajieni mwanaccm makini , nitajieni mwadilifu , nitajieni mwenye nafuu....! hakuna , na hatakuwamo, waadilifu wote waliishatoka, wamebaki wachumia tumbo, walea ufisadi, wanafiki, madikteta na wehu.
 

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,541
928
sammosses:jambo lolote lile likifka mwisho watendao huona ni kawaida kwa kila wafanyao,lakini watendewa hutabiri kuwa huo ndo mwisho wa
utawala dhalimu na kikomo cha ombwe la uongozi,nasema wataendelea kuchemka kwa kauli zao mpaka hitma yao ifike.sisi
tunasema endeleeni kuchemka,ili mabadiliko yaongeze kasi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom