DC Sabaya amshukia vikali Mwenyekiti wa halmashauri ya HAI 'ukinizingua nakuzingua '

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro,Lengai Ole Sabaya amemwagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Yohana Sintoo kuhakikisha analipa deni la zaidi ya sh,milioni 600 linalotokana na madai ya wazabuni ,sekta binafsi na mifuko ya hifadhi ya jamii ndani ya siku Saba kabla hajachukua hatua.

Agizo hilo ambalo linaanza leo, amelitoa mapema leo katika halmashauri hiyo wakati akiongea na watumishi wa halmashauri hiyo,wazabuni ,taasisi za fedha ,sekta binafsi na wananchi mbalimbali ambao wanaidai halmashauri hiyo.

"Mkurugenzi kama hajawalipa watu fedha zao kwa muda wa siku Saba nilizoagiza maana yake umezingua na Mimi nitakujibu kwa kukuzingua"alisema Sabaya

Mkuu huyo wa wilaya amesema zipo jitihada za Maksudi zinazofanywa na baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo kuipaka matope serikali kwa kushindwa kulipa madai halali ya wazabuni na hivyo kuwafanya wananchi waichukie serikali yao.

Ameagiza ndani ya siku Saba mkurugenzi huyo kuhakikisha analipa Madeni mbalimbali yanayotokana na wazabuni , Saccos na mfuko wa hifadhi ya jamii PSSSF ambapo mkurugenzi huyo anadaiwa kutowasilisha michango ya wanachama inayofikia kiasi cha zaidi ya sh, milioni 95 na kusababisha Deni hilo kufikia kiasi Cha sh,bilioni 3.

"Nakuagiza mkurugenzi ndani ya siku saba madeni yote mnayodaiwa yawe yameshalipwa na ukizingua na mimi nitakuzingua"alisema Ole Sabaya

Aidha Ole Sabaya alitoa maagizo kwa watoza ushuru wa halmashauri kuacha tabia ya kuwatoza walipa kodi ushuru wa mwezi mzima bila kuwakatia risiti na kuacha tabia ya kupanga vizimba kwenye masoko kwa kuwa hiyo sio kazi yao.

Wakizungumza katika kikao hicho Baadhi ya wazabuni ambao wanaoidai halmashauri hiyo fedha mbalimbali walieleza kwa uchungu jinsi halmashauri hiyo ilivyolenga kuwadhulumu fedha zao huku wakimtuhumu mweka hazina wa halmashauri hiyo (DT) ,Verda Msangi kwa kuonyesha dharau na kuwatolea maneno machafu wakati wakifuatilia fedha zao.

Felix Jonathan ambaye ni kaimu meneja wa Psssf mkoani Kilimanjaro alisema kwamba mfuko wao unaidai halmashauri ya Hai kiasi cha sh,3 bilioni za michango ya wanachama mbalimbali wa halmashauri hiyo ambapo deni halisi ni milioni 95 lililoongezeka kutokana na tozo na malimbikizo ya muda mrefu.

Naye Simbo Mbasha ambaye anadai kukodisha trekta kwa halmashauri ya Hai tangu mwaka 2019 kwa kiasi cha sh,18 milioni alilalamika mbele ya Ole Sabaya kutolipwa fedha hizo mpaka Sasa.

Kaimu meneja wa Saccos ya walimu wilayani Hai ,Sara Swai alisema chama chao kinaidai halmashauri hiyo jumla ya shilingi milioni 34 tangu mwaka 2017 mpaka sasa ambapo wamekuwa wakizungushwa mpaka Sasa.

Elly Obonyoson ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Data Logic Solution ambaye alisambaza vifaa vya elimu na ofisi vyenye thamani ya sh,milioni 6.9 tangu mwaka 2016 anaidai halmashauri hiyo fedha hizo ambapo mpaka sasa hajalipwa chochote.

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Herick Marisham katika kikao hicho aliahidi kutekeleza agizo hilo ndani ya muda uliotolewa.

1.jpg

Ends.............
 
Si tuliambiwa mwamba kajiudhuru , kumbe anapiga kazi ,Ila mshikaji ashawahi nichapa Kofi tukiwa O-level pale Ikizu secondary na mm nikamdhulumu kitabu, ye alikuwa form four mi nilikuwa nyoya
Alisoma ikizu mwaka gan?, alikuwa kiranja ?
 
Hana jipya huyu! Huko nyuma alikuwa hayajui haya! ajiandae kufungasha virago wenye fedha zao alizowapora wakamgegede huko mtaani. Mwenzie Makonda jiji la Dar analiogopa kama ukoma kwa mabaya aliyofanya
 
Back
Top Bottom