*DC CHRISTINA MNDEME KUKOMESHA MIMBA ZA UTOTONI DODOMA*
Wilaya ya Dodoma mjini chini ya Mkuu wa wilaya mh Christina Mndeme imezindua kampeni ya magauni manne katika kupambaba na changamoto za mimba za utotoni/wanafunzi,uamuzi huo umetokana na kukithiri kwa mimba kwa wanafunzi kiasi cha kukatisha masomo yao na hatimaye ndoto zao kukatishwa pia,vilevile kupelekea maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama ukimwi nk.
Mh Christina Mndeme ametumia siku ya tarehe 10/3/2017 kuongea na wanafunzi 5,000 wa kike wa shule za sekondari Dodoma mjini pamoja na walimu wao na wanajamii wengine,amewasihi wanafunzi kuepukana na tamaa na kuthamini masomo kwani ndio nguzo ya ndoto zao, ametoa rai kwa wazazi kutoa ushirikiano mkubwa pindi pale tunapotaka kuwabaini wahusika waliowapa watoto wao mimba kwani kwa kutokufanya hivyo wamekuwa wakirudisha nyuma mapambano haya.
Takwimu si nzuri kwa wilaya ya DODOMA mjini tayari kuna taarifa za mimba 74 zilizothibitika kwa sekondari kipindi cha January 2016 mpaka Machi 2017, tuungane katika ulezi wa watoto wetu ili watimize ndoto zao.
_Source_ Mwananchi 12/03/2017