DC Makonda: Mchungaji tapeli wa ardhi achunguzwe

chula migingo

Member
Mar 4, 2015
18
6
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, ameagiza kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua mtu anayedaiwa kutapeli ardhi kwa kutumia cheo cha mwenyekiti Serikali ya mtaa.

Mtu huyo anadaiwa pia kuwa mchungaji wa kanisa la kipentekoste, Nyakasangwe Kata ya Wazo, ametajwa kuwa ni Peter Mibilale.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Makonda alisema kuwa ofisi yake imeanza kushughulikia tatizo sugu la migogoro ya ardhi katika Manispaa ya Kinondoni na kuziagiza mamlaka husika kuchunguza tuhuma za mtu huyo ili sheria ichukue mkondo wake.

"Imenibidi nicheke kwa sababu naangalia ni jinsi gani ya kutatua migogoro ya ardhi katika eneo hili, bado tena kiongozi wa kiroho na ambaye nimeambiwa ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa, badala ya kushirikiana na wananchi, anaongeza kasi ya migogoro…achunguzwe na achukuliwe hatua," alisema.
==================

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, ameagiza kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua mtu anayedaiwa kutapeli ardhi kwa kutumia cheo cha mwenyekiti wa kijiji.

Mtu huyo anadaiwa pia kuwa mchungaji wa kanisa la kipentekoste, Nyakasangwe Kata ya Wazo, ametajwa kuwa ni Peter Mibilale.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Makonda alisema kuwa ofisi yake imeanza kushughulikia tatizo sugu la migogoro ya ardhi katika Manispaa ya Kinondoni na kuziagiza mamlaka husika kuchunguza tuhuma za mtu huyo ili sheria ichukue mkondo wake.

"Imenibidi nicheke kwa sababu naangalia ni jinsi gani ya kutatua migogoro ya ardhi katika eneo hili, bado tena kiongozi wa kiroho na ambaye nimeambiwa ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa, badala ya kushirikiana na wananchi, anaongeza kasi ya migogoro…achunguzwe na achukuliwe hatua," alisema.

Ofisa Ardhi wa Manispaa ya Kinondoni, Jeriman Masinga, alisema ni kinyume cha sheria mtu yeyote kuuza ardhi ambayo si mali yake na ni kosa la jinai.

"Mwenyekiti wa kijiji hana mamlaka kwa sheria hii kuuza ardhi…ardhi ni mali ya serikali na mamlaka zinazohusika kisheria ni halmashauri kwa kuzingatia mipango miji na upimaji wa ardhi," alisisitiza.

Alisema watu waliofanyiwa hujuma hiyo wana haki kisheria kumshitaki mwenyekiti wao kwa kuwa kisheria amejiweka kitanzini mwenyewe.

Mmoja wa watu wanaolalamika ardhi zao kuchukuliwa na mwenyekiti huyo na kuuzwa kwa watu wengine, Claud Chikonyi, alisema awali katika nyakati tofauti mwenyekiti huyo alimshawishi kufanya usafi na usimamizi katika eneo lake ili kutovamiwa na matapeli.

Badala yake, alishangaa Februari 21, mwaka huu alipewa barua na serikali ya mtaa ikimtaarifu kujibu shitaka la kuvuka mipaka na kuingia eneo jingine lililotengwa na wananchi kwa shughuli za kijamii na kusitishwa kutolifuatilia tena eneo lake.

Chikonyi alidai kuwa eneo hilo alilipata tangu mwaka 2001 lakini mwenyekiti huyo na genge lingine la watu aliodai kuwa ni mtandao wa matapeli wanaojiita mabaunsa wamekuwa wakiwaandama wananchi na kuwachukulia maeneo yao halali.

Hata hivyo, alisema kwa kutumia wadhifa wake, mwenyekiti huyo alichukua eneo hilo kwa nguvu na kumuuzia mwananchi mwingine kwa Shilingi milioni nne.

Alipotafutwa kuzungumzia tuhuma hizo kwa njia ya simu jana, mwenyekiti huyo alikata simu na baada ya mwandishi kujaribu kwa mara nyingine simu hiyo haikupatikana.

Chanzo:Nipashe
 
Niliwahi kuhoji katika kazi ya uenyekiti wa mtaa kuna nini? ni kazi isiyokuwa na mshahara wala marupurupu lakini watu wanapigana vikumbo kugombea wanapeana sumu wanapigana wanalala usiku kucha wakipindua kura na wengine wanakesha wakilinda kura. Ukweli hakuna kingine ni udalali wa viwanja na maeneo ya wazi.

Kwa utaratibu uliopo sasa maeneo yasiyopimwa uuzaji wake husimamiwa na wenyeviti wa mtaa na maeneo yaliyopimwa mauziano hushuhudiwa na mwenyekiti wa mtaa kabla taratibu za kuhamisha umiliki hazijaanza, hivyo hawa wenyeviti wa ntaa ni kiungo muhimu katika migogoro ya ardhi.
 
Back
Top Bottom