DC Magoti, 'achefukwa' wanaohujumu misitu na kumchongea kwa Rais

DC Magoti, 'achefukwa' wanaohujumu misitu na kumchongea kwa Rais

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti, ametangaza vita na 'vigogo' ambao wameifanya Hifadhi za Misitu ya Kazimzumbwi iliyopo katika Hifahi ya Pugu pamoja na Kisarawe kwa ajili ya masilahi yao bianafsi.

Amesema baadhi ya viongozi wamegeuza hifadhi ya Misitu Asilia ya Pugu Kazimzumbwi na nyingine zilizizopo katika wilaya hiyo kama shamba la 'bibi' huku wakitumia nafasi zao kuwatishia Askari na Maofisa wa Huduma ya Misitu Tanzania (TFS), kutekeleza majukumu ya kuwadhibiti, kwa kutengeneza njama za kuwafukuzisha kazi.

Kadhalika, amesema baada ya yeye (DC) na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kwa kushirikiana na maofisa wa TFS, kuwadhibiti hata yeye wanamtishia na kumchongea kwa madai kwamba anamwaribia Rais Samia Suluhu Hassan.

Magoti ametoa kauli hiyo leo kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha ustahimilivu wa bioanuawai ya misitu ya mazingira asilia dhidi ya matishio ya mabadiliko ya Tabianchi iliyofanyika katika hifadhi ya Pugu Kazimzumbwi.

Magoti amesema baadhi ya viongozi wasio waaminifu, wananunua pikipi na kuwapatia madereva kwa ajili ya kufanyia biashara ya kubebea mkaa na pale wasimamizi wa sheria wanaposimamia sheria kukomesha hilo, huwatishia kwa lengo la kuwakatisha tamaa wasitekeleze majukumu yao hayo.

Magoti, amesema si Askari au Maofisa wa TFS pekee, hata yeye kama kiongozi aliyeaminiwa katika eneo hilo, naye amekuwa akitishiwa na baadhi ya vigogo ambao wanataka kutumia hifadhi hizo kwa aili ya manufaa yao.
 
Huyu nae kazidi sasa

Anatafuta mno attention za kipumbafu. Atishiwe nini hebu aache ujinga
 
Ila Kwa Hili namuunga mkono jamaa. Lazima tutunze mazingira yetu. Hiyo misitu ya asili lazima ilindwe siasa isitumike.

Nyau de adriz
 
Nani huyo tena anampiga mkwara Dc wa kimataifa kutoka Kisarawee, hajui Dc ana migambo wengi sana
 
Back
Top Bottom