DC Ludewa: Waliosusia kikao changu wakamatwe

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,709
Reaction score
59,229
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw. Andrea Tsere ametoa agizo la kukamatwa kwa wananchi wa kitongoji cha Ngalawale wilayani humo kwa kususia kikao cha mkuu huyo wa wilaya.

Akizungumza katika eneo la tukio mkuu huyo wa wilaya ameeleza kusikitishwa kwake na kitendo cha wananchi kususia vikao vya maendeleo vinavyoitishwa na serikali ambapo ikitokea tatizo au mradi ukiwa unafanyika katika eneo lao wanakuwa wa kwanza kulalamika kwamba hawashirikishwi.

“Naagiza wananchi wa kitongoji hiki wakamatwe majumbani hadi walipe faini, haiwezekani tuitishe kikao cha kujadili maendeleo yanayowahusu na wao washindwe kujitokeza hii siyo dalili nzuri katika kuwashirikisha mambo yanayowahusu” Amesema Tsere.

Aidha tangu ateuliwe kushika wadhifa huo wa ukuu wa wilaya , Bw. Tsere amekuwa akifanya ziara katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi jambo ambalo amesisitiza ushirikiano kutoka kwa wananchi kwani kazi hizo anafanya kwa ajili yao.

Chanzo: IPP Media
 
Atumie social media na vyombo vya habari kutoa taarifa za hiyo miradi siyo kulazimishana kwenda kwenye mikutano.
 
Hivi huyu Tsere ni mtoto wa Mzee Tsere,aligombea Ubunge Jimbo la Karatu 2005 na baadae akawa Mkuu wa Wilaya ya Ilala?
 
Wananchi wanaona bora waende kutafuta kuni porini kuliko kusubiri kuonana na Kiongozi wa kuteuliwa,. Hana manufaa kwao , hao wako kwa manufaa ya aliye wateua. Angeitisha mkutano Mbunge wao wangeenda kumsikiliza maana ndio walio mchagua asikilize kero zao na azipeleke panako husika.
 
watumbukizwe visimani hao..
wanywe maji weeeeeee..
hahahahaaaaaaaa !!!
 
Hii inaonyesha wananchi wameshachoshwa na maCCM. Na hata hao viongozi wanatawala watu ambao hawakuwachagua.

MaCCM yanalazimisha kutawala.
 
Ndio shida ya kuwapa uongozi watu wa aina hii!!
Wewe naye ni kituko kweli wala hujui nchi inavyoongozwa. Toka mmelpgwa na chadema Basi mmekuwa wa kulalamikia watumishi wa serikali hata pale wanapotekeleza majukumu yao
 
Ajipange. Wananchi sio kuku huwezi waita na wakaona unaenda kuongea pumba wakaja tu.

Isitoshe wananchi wana hasira kwasababu watoto wao wameambiwa wasubiri wataajiriwa ila upepo unaonyesha kabisa hakuna ajira.

Vile viwanda vilitangazwa wakajua watoto wao wataajiriwa humo ila viwanda vimepaa. GSM wana-order bidhaa nje wanazipa jina lao wanakuja kutuuzia so, hata vikianzishwa viwanda vya ndani havitaweza kasi.

Wananchi sasa wanadukuliwa, ukisema chochote kile unapandishwa kizimbani.

Nasikia mahospitalini madawa hakuna na hata ya TETANUS nchi nzima hakuna.

Vilevile Serikali imesema haitatoa msaada wa chakula kwa wenye njaa popote nchini, hivyo wananchi wako busy wanafanya shughuli za shamba.
 
Having the authority to take people behind bar for 48hours does not give you the authority to do what he is saying......i pity him because when those people unleash litigation against his action they are going to win as it is not mandatory for the people to attend such meetings
 
Kilimpeleka nini huko. Akamatwe yeye kwanza ni mvamizi was makazi ya watu. Mikutano imekatazwa watu wafanye kazi . Yeye karuhusiwa na nani?
 
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw. Andrea Tsere ametoa agizo la kukamatwa kwa wananchi wa kitongoji cha Ngalawale wilayani humo kwa kususia kikao cha mkuu huyo wa wilaya.

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Andrea Tsere
Akizungumza katika eneo la tukio mkuu huyo wa wilaya ameeleza kusikitishwa kwake na kitendo cha wananchi kususia vikao vya maendeleo vinavyoitishwa na serikali ambapo ikitokea tatizo au mradi ukiwa unafanyika katika eneo lao wanakuwa wa kwanza kulalamika kwamba hawashirikishwi.

“Naagiza wananchi wa kitongoji hiki wakamatwe majumbani hadi walipe faini, haiwezekani tuitishe kikao cha kujadili maendeleo yanayowahusu na wao washindwe kujitokeza hii siyo dalili nzuri katika kuwashirikisha mambo yanayowahusu” Amesema Tsere.

Aidha tangu ateuliwe kushika wadhifa huo wa ukuu wa wilaya , Bw. Tsere amekuwa akifanya ziara katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi jambo ambalo amesisitiza ushirikiano kutoka kwa wananchi kwani kazi hizo anafanya kwa ajili yao.

Chanzo: IPP Media
sasa ikiwa wananchi, wakikosa malipo ya kulipa faini, kwa uwingi wao rumande y LUDEWA itatosha?
 
Wananchi wanaona bora waende kutafuta kuni porini kuliko kusubiri kuonana na Kiongozi wa kuteuliwa,. Hana manufaa kwao , hao wako kwa manufaa ya aliye wateua. Angeitisha mkutano Mbunge wao wangeenda kumsikiliza maana ndio walio mchagua asikilize kero zao na azipeleke panako husika.
Watawala
Ajipange. Wananchi sio kuku huwezi waita na wakaona unaenda kuongea pumba wakaja tu.

Isitoshe wananchi wana hasira kwasababu watoto wao wameambiwa wasubiri wataajiriwa ila upepo unaonyesha kabisa hakuna ajira.

Vile viwanda vilitangazwa wakajua watoto wao wataajiriwa humo ila viwanda vimepaa. GSM wana-order bidhaa nje wanazipa jina lao wanakuja kutuuzia so, hata vikianzishwa viwanda vya ndani havitaweza kasi.

Wananchi sasa wanadukuliwa, ukisema chochote kile unapandishwa kizimbani.

Nasikia mahospitalini madawa hakuna na hata ya TETANUS nchi nzima hakuna.

Vilevile Serikali imesema haitatoa msaada wa chakula kwa wenye njaa popote nchini, hivyo wananchi wako busy wanafanya shughuli za shamba.
Ndio maana wananchi walitaka vyeo hivi vifutwe. Wananchi wanateseka kulipa kodi kwa ajili ya kuwahudumia hawa halafu yeye anakuja kuwaletea vitisho vyake ?
 
Back
Top Bottom