DC Kukabidhi zawadi kwa mshindi wa kamari ya Tatu Mzuka

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Niwe mkweli kwa Nchi yangu niliyozaliwa. Jambo hilo pichani ni la kushangaza. Sidhani kuwa hiyo ni kazi ya DC.

Tunadhani si jukumu la DC kutumia muda wake kushuhulika na masuala yenye kunufaisha mtu mmoja mmoja na kwa kupitia kamari za kubeti na kadhalika.

Media yetu siku hizi imegubikwa na matangazo mengi ya mambo haya ya kamari za kubeti na nyinginezo. Hivyo, media kupitia matangazo ya kulipia inatumika kusambaza maradhi haya.

Ni dhihaka kudhani kuwa maisha ya Watanzania yatabadilishwa kwa kuhamasisha michezo ya kubeti kwa maana ya kamari. Tulidhani DC angehangaika na kuwahamasisha watu wake kushiriki kazi za uzalishaji badala ya kucheza kamari.

Vijana wetu wajue kuwa hali zao hazitabadilika na kuwa bora kwa kuacha kufanya kazi na kuendekeza kucheza kamari.

Serikali ni mlezi mkuu wa jamii. Kuna haja ya kuingilia kati na kuweka aina fulani ya udhibiti kwenye hili la kamari. Vinginevyo nguvu kazi ya taifa inakwenda kusiko kwema.

Hakina, tusingependa kuona aina hizi za picha. Tukiacha ikawa mazoea, Mungu pitishilia mbali, tutakuja kuona picha za Ma RC wetu na hata mawaziri wakikabidhi zawadi kwa washindi mmoja mmoja wa michezo ya kubeti, na huku wakihamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuicheza.

Inatuhusu sote. Tupaze sauti.

Maggid Mjengwa

0688 37 36 52 ( Whatsapp)
 

Attachments

  • 02.jpg
    02.jpg
    30.1 KB · Views: 74
Back
Top Bottom