kibarango
Senior Member
- Sep 6, 2014
- 146
- 309
Leo tarehe 03/05/2017 majira saa tatu asubuhi. Mwenyekiti Wa Mtaa wa Mhongolo bw Emanuel Nangale ( CHADEMA) Hapa Kahama mjini kawekwa kizuizini kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Kahama Bw Fadhil Nkulu.
Baada ya kufutilia kosa alilolifanya mwenyekiti huyo nimesikitika sana. Kwa kifupi Mkuu wa wilaya alimuagiza Afisa mtendaji wa kata amtaarifu mwenyekiti wa mtaa aandae mkutano wa hadhara kwa maelekezo kuwa mkuu wa wilaya anahitaji kuzungumza na wananchi wa mtaa huo, kuhusu mambo mbalimbali.
Baada ya mwenyekiti kupataa barua ikimtaka aandae mkutano, nae akaandaa mkutano huo. Wananchi walipofika mkutanoni DC hakutokea ndipo diwani wa kata husika akampigia simu. Cha kushangaza DC huyo akaja mkutanoni na polisi kisha akaamuru mwenyekiti wa mtaa bw Nangale wa CHADEMA awekwe kizuizini Massa 48.
Sababu aliyoisema DC ni kwamba hakuagiza mkutano huo uandaliwe. Cha kushangaza ni kuwa mwenyekiti anayo barua ikimuagiza kuandaa mkutano huo.
My take DC waaacha kutumia madaraka yao vibaya kuumiza wananchi wengine hasa DC huyu anamnyanyasa bwana Nangale Kwa kuwa amepata uenyekiti kwa tiketi ya chadema.
barua ambayo ilimuelekeza kuandaa mkutano huo.