DC Ikungi Singida jengeni daraja watu wanakufa

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
133
546
DC WA IKUNGI, SINGIDA JENGENI DARAJA LA MINYUGHE, WATU WANAKUFA, UCHUMI UMESIMAMA, ACHENI UBABE NA JANJA JANJA.

Na: Suphian Juma

Kama Mtanzania niliyezaliwa Mkoa wa Singida na hata kama nisingezaliwa huko, nimefadhaishwa na taarifa kwamba DARAJA LA MTO SAWIA ambalo linaiunganisha Kata ya Minyughe na Kata Kata zingine kama Makilawa na Iyumbu, limevunjika (limekaribia kuzama kabisa) takribani mwezi sasa na kuleta tafrani kwa wananchi isiyo kifani.

Wananchi wa maeneo haya wamelalamika sana kwa viongozi wao wa ngazi ya Kijiji, Kata hadi Wilayani bila mafanikio. Ikumbukwe sasa ni majira ya mvua, ambapo karibia kila siku mto Sawia huwa umejaa, na hivyo kusababisha maelfu ya wananchi kushindwa kusafiri katika pande hizo mbili ambazo kimsingi zina mahusiano makubwa ya kibiashara, kiuchumi na kijamii.

Sio hivyo tu; wananchi pia wanapata wakati mgumu mno hata kwenda Ofisi za Wilaya yao ya Ikungi ama kwenda Ofisi za Mkoa wao wa Singida kupata huduma za kiutawala pale, inapobidi, maana mfano mwananchi wa Mtavira ili afike Halmashauri ya Ikungi au Singida Mjini lazima akatishe Mto huo.

Imagine; majuzi nataarifiwa kuna mtoto wa miaka ipatayo mitano amefariki hapo darajani baada ya wazazi wake waliotokea upande wa Mtavira kukesha hapo na gari bila kupata namna mbadala ya kukatisha ng'ambo ya pili ili wawahi kwenda kwenye matibabu katika Hospitali tegemewa ya Mkoa wa Singida.

Cha pili kinachokera zaidi; Jana baada ya malalamiko ya wananchi ya muda mrefu bila kusikilizwa, vijana waliojiajiri na wengine kuajiriwa katika usafiri wa gari ya aina ya 'Noah' unaotumiwa kuwasafirisha wananchi wa pande hizo mbili; kwa kutaka kupaza sauti zao, walipogoma hapo darajani, Mkuu wa Wilaya ameenda na Polisi badala ya kukisikiliza kilio chao, yeye AKAAGIZA WAKAMATWE na hatimaye kusekwa ndani kwenye kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ikungi.

Yaani Mkuu wa Wilaya unaenda kwa wananchi wako badala utoe mpango mbadala kuwasaidia wananchi wako, unawakamata hao vijana wanne na kuwaweka mahabusu bila dhamana tangu Jana Jan 7, 2020 hadi leo Jan 8, 2020 ndio unawaachia na kuwaagiza wakaripoti Ijumaa ya kesho kutwa, huku ndio kulijenga daraja??

DC tunakuuliza kuwakamata hao vijana ndio njia mbadala ya kulijenga daraja? Kama mmeambiwa mwezi sasa daraja limevunjika, mpo kimya, hakuna suluhu ya dharura, mlitaka wananchi watembee kwa magoti hadi mlipo? Watumie njia gani kuwaeleza maumivu yao?

Yes tunajua mnawatisha hivi ili wao na wananchi wengine wakae kimya, na wakikaa kimya, hamuoni wagonjwa watazidi kukata roho hapo bila msaada? Au wakifa wengi zaidi ndio furaha yenu? Na mnafurahia kazi za kiuchumi zisimame? Maendeleo gani mnayoyataka nyie wawakilishi wa Serikali ya Rais Magufuli?

Halafu mnawachukua vijana mnawasekwa ndani bila dhamana, hivi kugoma hapo kwa jambo nyeti la maisha ya wananchi ndio tuseme imegeuka Uhujumu uchumi ama Ukatatishaji fedha ambao hauna dhamana? Mmetumia Sheria gani? Mtasema ile ya DC ya masaa 24? Kwa kosa hili? Sheria gani tuambieni au ubabe tu dhidi ya wanyonge? Ooops!!

Hold on; hivi Mbunge wangu wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, uko wapi wananchi wako wanateseka bila daraja? Vijana wako wanasekwa rumande 'kiholela holela'? Wewe unamwakilisha nani Bungeni? Rais Magufuli au? Au unasubiri kampeni zifike ukaendeleze stori zako za ahadi hewa kama za mwaka 2015? Come on show your presence, ni wajibu wako, wananchi hawa wanakulipa mshahara, watendee haki.

RAI YANGU;

Mkuu wa Wilaya achana na hao vijana, umeenda Minyughe, umeliona tatizo, tunajua unajua namna ya kufanya na Kiongozi/Viongozi/Mamlaka gani ya kukusaidia utufanyie yafuatayo;

1. Kwa haraka sana, kwa udharura, kwa ajili ya uhai wa wananchi, watengenezeeni njia mbadala ya kukatisha huo mto wakati;

2. Mnafanya utaratibu wa kulijenga upya au kuboresha hilo daraja kwa kiwango vinavyostahili na si vile dhoofu vilivyosababisha dhahama hii.

3. Jengeni daraja la Mto Ntika pia kimesemwa na maji zaidi ya miezi sasa, watu wa Minyughe wanashindwa kwenda Minyughe, msisubiri hadi wananchi wasombwe pia na maji.

4. Chunguzeni zile tuhuma za baadhi ya viongozi wa Kata hizo za Minyughe na Makilawa wanaopokea rushwa na kuruhusu magari makubwa kupita usiku. Ni hatari kwa uhai wa madereva hao na si maadili ya Kiuongozi.

Suphian Juma,

Afisa Habari ACTwazalendo,

Kijiji cha Minyughe,

Januari 08, 2019.

IMG-20200108-WA0085.jpeg
IMG-20200108-WA0077.jpeg
IMG-20200108-WA0063.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Badala ya kujenga madaraja kati yao na Wananchi wanaowaongoza, wao wanajenga ukuta ili kujikinga dhidi ya Wananchi. Itatokea siku isiyojulikana hizo kuta zitadondoshwa na hapo ndio watajua umuhimu wao. Katika picha daraja linaonekana zuri na si ajabu lilifunguliwa kwa mbwembwe. Wahusika wanasita na kuona aibu kujulisha mamlaka iliyo juu kuhusiana na tatizo hili. Inavyoelekea wanaficha ukweli huu. Na siku zote mficha maradhi, kilio kitamuumbua "kibhisabhisa obhurweri ekiriro kirambura" kwa maneno yake Mwalimu.
 
Ndio mbwembwe zilikuwa kubwa balaa
Badala ya kujenga madaraja kati yao na Wananchi wanaowaongoza, wao wanajenga ukuta ili kujikinga dhidi ya Wananchi. Itatokea siku isiyojulikana hizo kuta zitadondoshwa na hapo ndio watajua umuhimu wao. Katika picha daraja linaonekana zuri na si ajabu lilifunguliwa kwa mbwembwe. Wahusika wanasita na kuona aibu kujulisha mamlaka iliyo juu kuhusiana na tatizo hili. Inavyoelekea wanaficha ukweli huu. Na siku zote mficha maradhi, kilio kitamuumbua "kibhisabhisa obhurweri ekiriro kirambura" kwa maneno yake Mwalimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom