DC Hapi atoa zawadi za Xmass kwa watumishi wa ngazi ya chini Kinondoni

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi leo ametoa zawadi ya mchele, nyama, mafuta ya kupikia na maharagwe kwa watumishi wa ngazi za chini wakiwemo madereva, makarani na wahudumu kama shukrani ya utumishi wao katika mwaka huu unaoisha wa 2016 na sikukuu za Xmas na Mwaka mpya ujao.

"Mimi na Mkurugenzi tunawashukuru sana kwa utumishi wenu kwa kipindi chote tangu tulipoteuliwa kuja hapa, hasa nyinyi wafanyakazi wa ngazi za chini. Bila nyinyi tusingefanikiwa. Mna mchango mkubwa katika kuifikisha Kinondoni hapa ilipo sasa. Endeleeni na moyo huo wa upendo. Mungu awabariki sana."

Alisema Mkuu wa Wilaya.

 
Ni jambo jema...je katoa mfukoni mwake?
 
M
Harufu kali ya rushwa!!!!!
Isipokuwa ikikutikana kwenye mwongozo wa majukumu yake ikiungwa mkono na budget
Manake kwa hali ya uchumi ilivyo haiwezekani Mh.akatoa mfukoni kwake.
 
Hongera sana kijana, kwa miaka yangu ya utumishi wa umma sijawahi kuona! Huu utaratibu kwenye NGO za madhehebu ya dini sawa ila serikalini sidhani,
 
Hii Ni hatar, mi sipokei
 
Huyu ndo alienda pale palestina sinza kufanya ziara ya kushtukiza alfajiri ha ha ha ha
 
kwahyo akaita na waandishi wa habari kabisa, duuuuh Santa wa kibongo hatari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…