DC Handeni apiga kambi msituni

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


[h=2][/h]ALHAMISI, JULAI 12, 2012 04:23 NA MOHAMMED MHINA, HANDENI

muhingo.jpg
Muhingo Rweyemamu

MKUU wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Muhingo Rweyemamu, amepiga kambi kwenye mwambao wa misitu ya Kang'ata, wilayani humo, ili kukagua na kuona athari za uvamizi na ukataji miti ya uoto wa asili unaofanywa na wananchi kwa kisingizio cha kusafisha mashamba kwa ajili ya kilimo.
Akiwa katika msitu huo, Mkuu huyo wa Wilaya ameshuhudia uharibifu mkubwa unaotokana na uvamizi na ukataji wa miti ya asili katika misitu tengefu ya Kang'ata, misitu ambayo ilikuwa ikihifadhi idadi kubwa ya makundi ya nyuki na kuvuta kiasi kikubwa cha mvua.

Kutokana na uharibifu huo mkubwa wa mazingira, DC Muhingo amepiga marufuku utoaji wa vibali vya uvunaji wa miti ya mkaa na mbao hadi hapo kamati maalumu itakapoweka utaratibu mwingine mpya wa utoaji vibali vya uvunaji wa miti wilayani humo.

Akizungumzia uvamizi na uharibifu huo wa uoto wa asili, Muhingo alisema kuanzia sasa, mtu yeyote atakayeomba kibali cha kuvuna miti kwa ajili ya kupasua mbao au mkaa ni lazima aonyeshe kwanza shamba lake la miti kabla ya kufikiriwa kupata kibali husika.

Amesema hata baada ya kupata kibali hicho, mwombaji ambaye ni mwenye shamba ni lazima ukaguzi ufanywe katika shamba la mhusika ili kujiridhisha kama kibali alichopewa amekitumia kwa kuvuna miti iliyopo katika shamba husika na ndipo apatiwe kibali kingine kwa ajili ya kusafirisha mazao hayo kutoka msituni hadi katika eneo la soko.

“Wilaya ya Handeni ina maeneo mengi ya misitu ya uoto wa asili, lakini hivi sasa iko hatarini kugeuka jangwa kama juhudi za makusudi za kukabiliana na wavamizi wa misitu hazitachukuliwa mapema,

Amewataka viongozi wa serikali za vijiji na wananchi wenye maeneo makubwa ya ardhi, kuacha kuyauza kwa wageni wanaodai wanataka maeneo kwa ajili ya kilimo, kwani hata baada ya kupatiwa maeneo hayo wageni hao hukata mikaa na mbao wakijifanya wanasafisha maeneo kwa ajili ya kilimo.

Akiwa katika harakati za kuinusuru misitu wilayani handeni, Mkuu huyo wa Wilaya, hivi karibuni alimkamata mmoja wa watumishi wa Idara ya Misitu akisafirisha kiasi kikubwa cha magogo yaliyovunwa bila kibali, jambo lililopelekea kusimamishwa kazi kwa ofisa huyo wa Handeni.

Aidha Muhingo amewataka watumishi wote wa Idara ya Maliasili na Misitu wilayani humo kuwa waaminifu na waadilifu, kwa sababu kazi waliyonayo ni dhamana ya Watanzania wote, kwa hiyo hawana mamlaka ya kutumia rasilimali hizo kwa manufaa yao.

 
Muhingo hii ni nguvu ya SODA au ndio UWAJIBIAJI WA VIJANA WETU WAPYA?

Baada ya sifa usiwe fisadi...
 
Back
Top Bottom