DC Hai ashtukia wizi wa Million 70

DC Hai ashtukia wizi wa Million 70

Waziri2025

Senior Member
Joined
Sep 2, 2019
Posts
149
Reaction score
380
Wanawake wawili wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wamenusurika kuporwa fedha kiasi cha shilingi Million 70 Mara baada ya Mlinzi Wa Bank kuwauza kwa majambazi.

Tukio ilo limetokea kata ya Masama wilayani Hai mapema tarehe 30 Mwezi November Mara baada ya mlinzi wa kampuni ya Rolling kutoboa siri kwamba kuna wateja wawili kutoka kampuni ya Brack wametoka kuchukua fedha bank ya CRDB.

Mkuu Wa Wilaya Hai Lengai Ole Sabaya pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama walipata taarifa za mlinzi Huyo kutoboa siri ya fedha hizo ambapo simu yake ilikamatwa na kufanyiwa uchunguzi na kukutwa na meseji zaidi ya 20 akiwaelekeza gari yenye namba za usajili T 412 DPA inayo tumika kubeba fedha kutoka bank ya CRDB huko Sanya juu.

Lengai Ole Sabaya amesema kwamba alipata taarifa hizo kupitia kwa interlijinsia ambapo aliweka mtego kwa mlinzi Huyo na kukutwa akiendelea kupanga njama za namna fedha zitakavyo ibiwa na kwamba wanawake hao awakua na ulinzi wowote Mara baada ya kutoka bank

Sabaya amesema kwamba mlinzi huyo Alishawahi kufungwa Jela na baadae kuachiliwa hivyo anauzoefu katika maswala ya ujambazi pia alihagiza wanawake hao kupigwa Risasi na fedha zichukuliwe kwa urahisi .

Mlinzi uyo Mara baada ya mahojiano alikiri kupanga njama ikiwemo pamoja na kuandika jumbe fupi fupi kwa majambazi watakao vamia na kupiga Risasi hewani na kuondoka na kitita cha fedha kiasi cha shilingi Million 70

"Mimi nilikua nipate mgao wangu na endapo tungefanikiwa Mimi nilisha waambia majambazi wanipige eneo la shingo nizimie alfu baada ya muda nitazinduka pesa za mgao nitakuja kuzichukua Alisema mlinzi Huyo akiwa chini ya ulinzi "

Ataivyo Mkurugenzi wa kampuni Hiyo ya Brack anasakwa na jeshi la Polisi kwa kuruhusu Fedha nyingi kusafirishwa bila kuwepo na ulinzi kutoka kwa jeshi la Polisi au kampuni ya ulinzi jambo limeatarisha maisha ya wanawake hao ambao ni watumishi wa kampuni hiyo.

Hivi karibuni wilayani Hai Mji Mdogo wa Boma Gombe kumekuwepo na mtandao wa fedha bandia ambapo kupitia kamati ya ulinzi na usalama walimkamata kijana Richard akiwa na fedha bandia shilingi Million 11 na kutaja mtandao wanao shirikiana kutengeneza fedha hizo na badae kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazo mkabili
..................................
saba22.jpeg
sabayaaaaa.jpeg
 
Kumbe siku hizi habari za intelijensia zinaripotiwa moja kwa moja kwa mkuu wa wilaya.Halafu Mkuu wa Wilaya nae anaingia field saf sana maendeleo yametufikia.
 
jamaa alikutwa na jumbe kama 20 akielekeza kuna wateja wawili toka kampuni ya brack wametoka kuchukua fedha toka CRDB

gari lililobeba mzg huo toka benki ya CRDB ni namba izo.....

baada anahojiwa ana sema niliwaagiza wakija wanipige shingoni nizimie nikiamka ntafata mgao wangu.

maelezo hayaeleweki tukio lingefanyika wapi hapo benki (ili wampige hadi kuzimia ) ama nje ya benki (ndio sababu ya kuwapa maelezo ya gari namba na wahusika )

kabla ya kuiachia kwenye maduka ya filamu, mtengenezaji afanye kuihakiki kdg
 
Back
Top Bottom