DC Gondwe saidia hawa wananchi wako wa Kibindu

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,313
12,613
Iko hivi,

Pale kijiji cha Kibindu, Handeni kulitokea ajali ya mtoto mdogo kugongwa hadi kufa na mwendesha pikipiki . Mtoto alikufa mara tu baada ya kufikishwa Hospitali ya Wilaya ya Handeni. Tukio hili lilitokea tarehe 29 Decemba, 2019 na msiba ulimalizwa kijijini hapo siku ya Jumatano trh 01 January 2020 nyumbani kwa babu yake Mzee "Afande".

Issue yenyewe ni kuwa kijana aliyemgonga alitoroshwa eneo ya tukio na kijijini hapo na pikipiki iliyogonga ilitoweka eneo la tukio kwa dhamira ya kuficha tukio lisionekane machoni mwa vyombo vya usalama na vya kutoa haki. Maana inasemekana kuwa familia ya mtoto aliyegongwa na ya aliyegonga ni ndugu hivyo wanataka kufunika kombe ili mwanaharamu apite (eti marehemu hana haki na eti ndiyo ahadi yake hiyo huyo mtoto).

Mzee Godwin Gondwe, DC tafadhali tupia jicho la huruma, kitaaluma yako ya uandishi wa habari na ukuu wa usalama Wilayani kwenye tukio hili ovu lililoyagharimu maisha ya mchanga huyo aliyegongwa wakati akienda kununua maandazi mtaa wa jirani.

Kila mwanakijiji yuko tayari kufanya lolote ili haki ya mtoto huyo isipotee bure hata kwa kufikisha jambo hili ofisi namba 01.
 
ATARUDI UKIMPELEKA MAHAKAMANI?KM WAO WAMEELEWA KUN TATIZO GANI?HAKI YA MAREHEMU NI IPI?ALIPWE?JE AKILIPWA ATAFUFUKA?acheni ushamba,mkalime mvua inanyesha
 
Boda Boda wa kule wako rough sana hasa kona ya kilima cha kushukia pale mjini

Jr
 
Duh Ina maana ndg pande mbili zote wameelewana ila jamii na majirani Mnataka haki itendeke

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamii ya baba ya mtoto na baadhi ya jamii ya mama ya mtoto haikubaliani na makubaliano yanayotaka kufanikishwa, hata hivyo tukio hilo liko polisi hasa baada ya daktari kudai PF3 kabla ya kutoa matibabu
 
ATARUDI UKIMPELEKA MAHAKAMANI?KM WAO WAMEELEWA KUN TATIZO GANI?HAKI YA MAREHEMU NI IPI?ALIPWE?JE AKILIPWA ATAFUFUKA?acheni ushamba,mkalime mvua inanyesha
Ndivyo sheria inavyotaka hivyo? Mbona baba mzazi hakubaliani?
 
Yaani kibindu haya mambo ya kufunika kombe hayajaisha tu inabidi waachane na hii kitu sasa..nakumbuka kuna mwaka Fulani kuna ndugu yangu alimpa mimba mwanafunzi kitendo kilichopelekea mwanafunzi huyo akatishe masomo yake.

Cha ajabu ndugu wa pande mbili wakamalizana juu kwa juu niliwaona wa ajabu sana yaani....tukirudi kwenye suala hilo naungana na Mshana Jr alivyosema bodaboda wa huko wanajiachia sana hasa kushuka kile kilima cha kwenda kisatuni mwaka juzi nilikaa kwa siku kadhaa huko nkajionea mwenyewe na hilo suala niliwahi kulifikiria
 
Gondwe ana uzee gani? Kosa la barabarani unajua adhabu yake? Mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu kila kosa lina adhabu yake kisheria, kugonga mtu ni kosa, kuua mtu ni kosa, kugonga na kukimbia ni kosa, kuendesha speed kwenye makazi ni kosa, kuendesha bila leseni ni kosa, hata kuendesha chombo cha moto kichokuwa na bima ni kosa pia, kumficha mhalifu ni kosa na kutoa hongo kupotosha haki ni kosa pia. Tuiachie mahakama ichambue na kuhukumu na sio kujichukulia sheria mikononi mwetu.

Tunamfahamu Mh. Gondwe, ni mpenda haki na mtu makini sana, kama alikuwa halijui hili basi kupitia hapa jf ahakikishe haki ya mtoto huyu inalindwa ili iwe fundisho kwa wengine Wilayani kwake
 
Back
Top Bottom