DC Danny Makanga aumbuliwa mahakamani

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
591
1,000
Shahidi wa nane katika kesi ya kughushi mukhtasari wa serikali ya mtaa wa Levolosi iliyofunguliwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kasulu ,Dahn Makanga dhidi ya mume mwenzake, Mathew Mollel ameieleza mahakama ya kwamba hamfahamu Makanga na wala hajawahi kumwona.

Shahidi huyo,Zawadi Eliezeli ambaye ni ofisa ardhi katika halmashauri ya Jiji la Arusha,akijibu swali lililoulizwa na wakili upande wa utetezi,Ephraim Koisenge, alisema hamtambui Makanga katika muhtasari unaobishaniwa.


Aidha wakili huyo alimwuliza shahidi huyo kwamba je kwa maelezo yake mukhtasari uliopelekwa mbele ya jiji la Arusha endapo umetolewa hadharani mpaka sasa ,shahidi huyo alijibu na kusema kwamba mukhtasari huo haujawahi kutolewa hadharani na hafahamu Makanga aliupata wapi kwa sababu aliyeulera kuombea hati ni Methew Mollel


Akiongozwa na wakili wa serikali,Mary Lucas ,Eliezeli aliulizwa ya kwamba katika ofisi yao ni nani anahusika na utoaji wa nyaraka za kumbukumbu shahidi huyo alijibu kwamba ni mkurugenzi wa jiji au mtumishi yoyote atakayepewa ridhaa na mkurugenzi aitoe kwa niaba yake.

4d1b2e1fab03018288d2165c4c44d597.jpgbc9f3aa8b4d032226dcebab5621c991b.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom