mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,049
- 4,904
Mbeya. Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Rashid Chuachua amepiga marufuku magari yanayofanya matangazo ya misiba jijini hapa baada ya kuchukua miili ya watu waliofariki dunia hospitalini, akisema yamekuwa yakileta hataruki kwa wananchi na kujenga hofu.
Chuachua amesema hayo leo Jumanne Agosti 10, 2021 huku akiiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama kufanya doria na kuwachukulia hatua wamiliki wa magari hayo watakaobainika.
"Kumekuwa na tabia ya familia za watu wanaopoteza maisha kukodi magari ya matangazo na kuanza kutangaza maeneo mbalimbali ya jiji na kutaja majina ya wapendwa wao, sasa kwa niaba ya mkuu wa mkoa nimepiga marufuku rasmi leo Agosti 10 2021,"amesema Dk Chuachua.
"Ikumbukwe agizo hilo la kupiga marufuku hata aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila alikataza lakini sasa suala hilo limeibuka kwa kasi ya ajabu na kila baada ya dakika kadhaa unasikia tangazo la msiba, hivyo kusababisha shughuli za kiuchumi kusimama kwa muda."
Dk Chuachua amesema agizo hilo lianze mara moja na ndugu wanaofikwa na msiba, wawasiliane kifamilia kufanya taratibu za mazishi na kuhusu suala la matangazo kutoka hospitali mpaka kwenye maziko marufuku.
Amesema hata mikusanyiko ya watu haitaruhusiwa kwa kipindi hiki cha Covid -19 awamu ya tatu.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya ,Dourmohamed Issa amesema uamuzi wa mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ni sahihi kwa kuwa kumekuwa na taharuki kubwa kwa jamiii pindi magari ya matangazo na inayobeba miili ya waliopoteza maisha ikipita barabara kuu.
"Hata mimi nimewahi kupata mshtuko nikiwa naendesha gari nilikutana na magari manne yakitangaza na manne yakiwa yamebeba miili ya watu waliopoteaa maisha kimsingi ni hali inayotisha sana kwa Watanzania na hata wagonjwa wanaokuwa wamelazwa kwenye hospitali zetu,” amesema Issa.
Mkazi wa Mbeya, Rehema Mwanjonde amesema uamuzi huo wa Serikali ni sahihi kwa kuwa hata matangazo hayo yamekuwa yakiwarejeshea kumbumbuki watu waliowahi kupoteza ndugu zao.
Source: Mwananchi