DAWASCO Imewakatia Maji Wananchi wa Mbezi Kimara. Mhe. Mnyika Unahitajika Haraka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DAWASCO Imewakatia Maji Wananchi wa Mbezi Kimara. Mhe. Mnyika Unahitajika Haraka!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gosbertgoodluck, Jan 3, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wanaJF,
  Nimehabarishwa na rafiki yangu mmoja anayeishi Mbezi ya Kimara kwamba wananchi wanahaha kutafuta maji baada ya DAWASCO kuamua kukata huduma ya maji kwa wafanyabiashara wanaouza maji kwenye magari (water bowsers). Maeneo yote yaliyokuwa yanatumika kujaza maji kwenye bowsers sasa yamefungwa. Wananchi wengi wanaotegemea huduma hiyo ya magari, sasa wanateseka sana kwani chanzo chao cha maji kimesitishwa. Inawezekana DAWASCO wana malengo yao likiwemo la kuwakomoa wafanyabiashara wa maji lakini wafahamu kuwa wanaoteseka siyo wafanyabiashara bali ni wananchi wanaotegemea huduma hiyo. Hivi sasa wananchi wengi wa maeneo ya Mbezi Mwisho wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji. Lita 1,000 kwa sasa inauzwa Sh. 20,000 mpaka 25,000. Ni mwananchi gani wa hali ya kawaida anayeweza kumudu bei hiyo!! Ndiyo maana wananchi wengi wanateseka sana.

  Najua Mhe. Mnyika ni mwanachama wa JF. Tafadhali sana wasaidie wapiga kura wako kuondokana na adha hiyo kubwa inayowapata wapiga kura wako. Kama kuna wakati mwanachi wa kawaida anamhitaji kiongozi wake, basi huu ndiyo wakati wenyewe. Tafadhali Mhe. Mnyika jaribu kufuatilia kwa ukaribu sana suala hili.
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Oooh! Naomba sera ya 2015 iwe kisima kila nyumba.
   
 3. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  yamekatwa, hilo halina ubishi , mimi pia ni mkazi wa huku, nia njema ni kukomesha ufisadi wa waajiriwa wachache wa dawasco. swali ni kuwa kama maji yanaweza kukufilkia kwa lori kwa bei ya 75,000 kwa lita 10,ooo kwa nini yasimfikie mtumiaji kwa njia ya bomba? wafanyakazi wa dawasco wanaonufanufaika na ufisadi huu wamekuwa ndo kikwazo cha mabomba kuttoamaji. wanalazimisha mgao hata kama bomba kuu lina maji ili wafanye biashara. bomba linapita mbezi kupelekea wahindi maji kule mjini wakati wakazi zaidi ya 40% of dsm wanaishi maeneo haya na hawana maji. bravo mh. mnyika nadhani tuwe wavumilivu tutese kwa muda baadaye tutakuwa na suluhisho. madiwani wa zamani wa cccm walikuwa wadau wakuu wa biashara hii iliyoshamiri sana huku. wana ukwasi wa kutisha
   
 4. c

  cammory Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wagombanapo fahari wawili ziumiazo ni nyika!
  suala na kufunga oulets lingeendana na mikakati ya kulaza mabomba kwa ajili ya wananchi walengwa ambao walikuwa wakipata maji kwa maboza. sasa wananchi tunaumia kwa makusudi mazima kwa nini iwe hivyo.
  tumepandishiwa umeme, leoo kwenye magazeti wanasema watapandisha nauli za mabasi, na hii adha ya maji kulikoni? kwanini huduma muhimu kwa jamii kubwa zinakwenda juu? kwanini tuendelee kuwa na imanai na serikari hii ?:embarassed2:
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Mbunge Mnyika ataka maji yafunguliwe Mbezi

  Mbunge wa Ubungo, John Mnyika amefanya ziara ya ghafla tarehe 3 Januari 2010 ya kutembelea visima na maghati ya maji katika jimbo la Ubungo na kubaini mapungufu katika maghati hayo hususani kuuza maji bei juu tofauti na ile iliyopangwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA).

  Mbunge Mnyika ameeleza kuwa kwa mujibu wa agizo la EWURA na: 10-017 la tarehe 10 Juni 2010 bei ya maji katika mabomba ya jumuiya au maghati ya maji inapaswa kuwa shilingi 20 kwa kila lita 20, sawa na shilingi moja kwa lita lakini maghati mengi yanatoza kati ya mia moja mpaka mia tatu hali inayoongeza gharama za maisha na kusababisha ugumu wa maisha kwa watanzania wa kipato cha chini.

  Mbunge Mnyika ametoa mwito kwa EWURA kukagua visima na maghati yote ili kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa ikiwemo la bei husika kubandikwa kwenye kila eneo ili wananchi watambue haki yao wasitozwe kinyume na viwango vinavyostahili.

  Hata hivyo Mbunge Mnyika amesema kwamba katika kufanya hivyo lazima EWURA iwahusishe kwanza wananchi na viongozi wa kuchaguliwa ili hatua zozote zinazochuliwa ziweze kulinda maslahi ya umma.

  Mbunge Mnyika alisema kwamba amepokea taarifa toka kwa wananchi kwamba yapo maghati yamefungwa kwa maagizo ya EWURA kutokana na mivutano baina ya DAWASCO, DAWASA na wafanyabiashara binafsi wanaoendesha maghati hayo kuhusu bei ya maji hali ambayo imesababisha baadhi ya wananchi kukosa maji kwa takribani wiki moja.

  Mbunge Mnyika ameitaka serikali iingilie kati na kuagiza vioski husika vya maji vifunguliwe ili wananchi waweze kupata huduma hii muhimu ya msingi.

  Mbunge Mnyika amesema wananchi hawapaswi kuhukumiwa kwa kunyimwa maji kwa makosa yasiyokuwa ya kwao hivyo serikali kupitia DAWASA na DAWASCO inapaswa kutuma wafanyakazi wake kusimamia vioski husika ili huduma za msingi za maji zikiendelea kutolewa kwa wananchi wakati suala la ongezeko la bei ya maji kinyemela likiendelea kushughulikiwa.

  Mbunge Mnyika ameeleza kuwa kwa mujibu wa takwimu za Bajeti ya Kaya asilimia 38 ya wananchi wa Jimbo la Ubungo sawa na wastani wa watu wanne katika kila wakazi kumi wanategemea maji ya vioski na maghati hayo hivyo usimamizi mzuri zaidi unahitajika ili wananchi wasikose huduma za msingi na wasipate kwa gharama nafuu kama ilivyopangwa.  Imetolewa na:  Aziz Himbuka-

  Katibu Msaidizi wa Mbunge
   
 6. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  sawa tume ila kupata tatizo jimbo la ubungo linamilikiwa na mbunge wa chadema, watapuuza tu kama kawaida yao
   
Loading...